SI KWELI Lissu alikiri kuwa yeye na Mbowe walipatanishwa na Padre Kitima

SI KWELI Lissu alikiri kuwa yeye na Mbowe walipatanishwa na Padre Kitima

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu

Nimekutana na hii taarifa ikiambata na video na kudai kuwa ni ushuhuda wa kwamba Lissu alieleza kuwa walikutanishwa na Padri kitima kwa lengo la kupatanishwa. Je ni kweli Lissu alisema maneno hayo?

===
OGOPA MUNGU na TEKNOLOJIA amewahi kusema marehemu Ruge Mutahaba. Huyu hapa Tundu Lissu anaeleza wazi namna walivyoitwa na Padri Kitima kupatanishwa yeye na Mbowe Kama alivyonukuliwa @habibu_mchange hapo Jana akihojiwa na Edwin Odemba.

1766382287561.png

 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa sasa yupo gerezani kutokana na mashtaka anayotuhumiwa nayo ya uhaini.

Padri Charles Kitima ni katibu Mkuu wa baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambaye amekuwa akionekana pia mara kadhaa akikosoa mambo anayoyaona si sahihi yanapotokea nchini.

Madai

Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook mtumiaji mmoja alichapisha Taarifa akieleza kuwa Lissu likiri ama kueleza kuwa Padi Kitima aliwakutanisha yeye na Freeman Mbowe (Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA) ili kupatanishwa.

Uhalisia wa Madai hayo

JamiiCheck imefuatilia madai hayo pamoja na video na kubaini kuwa yanapotosha uhalisia.

Madai haya yameibuka mara baada ya kada wa Chama cha mapinduzi (CCM) Habibu Mchange ambaye awali alikuwa kada wa CHADEMA kueleza kuwa Padri Kitima ni mshauri wa CHADEMA. Mchange aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na mtangazaji Chief Odemba Disemba 20, 2025.

Uhalisia ni kuwa katika mahojiano aliyoyafanya na waandishi wa habari Januari 2025, wakati akiwa katika harakati za kampeni za kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Lissu alieleza kuwa walikutanishwa na kiongozi wa kidini ili kupatanishwa ila hakumtaja kwa jina.

Hivyo hakuna uthibitisho kuwa Lissu alimtaja Padri Kitima ama kiongozi yeyote wa kidini kwa jina ambaye walikuwa nao siku hiyo ya upatanisho.
Thanks JamiiCheck kwa kazi nzuri na kuweka sawa kumbukumbu na kuwaumbua vipotoshi na wapotoshaji
 
Wakuu

Nimekutana na hii taarifa ikiambata na video na kudai kuwa ni ushuhuda wa kwamba Lissu alieleza kuwa walikutanishwa na Padri kitima kwa lengo la kupatanishwa. Je ni kweli Lissu alisema maneno hayo?

===
OGOPA MUNGU na TEKNOLOJIA amewahi kusema marehemu Ruge Mutahaba. Huyu hapa Tundu Lissu anaeleza wazi namna walivyoitwa na Padri Kitima kupatanishwa yeye na Mbowe Kama alivyonukuliwa @habibu_mchange hapo Jana akihojiwa na Edwin Odemba.
View attachment 3518907
brainrot clicker
View attachment 3518905
Kwa maelezo yaliyopo, ni muhimu kuwa waangalifu kabla ya kukubali madai hayo kama ukweli kamili. Video au nukuu zinazozungushwa mtandaoni mara nyingi hukatwa au hutolewa nje ya muktadha wake halisi. Hadi sasa, sijaona tamko rasmi au rejea kamili kutoka kwa Tundu Lissu mwenyewe linalothibitisha wazi kuwa alisema maneno hayo kwa maana inayosambazwa.
 
Back
Top Bottom