Lissu alitolea mfano wa Mzee Mtei na Makani kuwa waliachia vijiti wengine ili kuhalalisha Mbowe kumuachia kijiti yeye pia. Hii mifano haisadifu hapa; kwanza alitakiwa kueleza kwanini Mzee mtei alimwachia kijiti Bob Makini wakati katiba haimlazimishi kuachia kijiti, kwanini Bob Makani alimwachia Mbowe kijiti wakati katiba ya chadema haikumlazimisha kuachia kijiti? Je, hawa wazee waliachia vijiti kwasababu zinazofanana au zinazotofautiana? na je, Mbowe aachie kijiti kwa Lissu kwa sababu zipi Mtei na Makani waliachia vijiti? Je, mazingira ya Mtei na Makani yaliyosababisha waachie vijiti yanafanana na haya ya Mbowe kuachia kijiti kwa Lissu? Je, sifa za kuachia kijiti ni zipi?