Administer
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 1,271
- 1,604
Hatutaki siasa za kumtumia nguvu tutapoteza maishaNi lini Lissu amewahi kupendekeza kuweka ukomo kwenye uongozi wa chama cha chadema akakataliwa?
Kwanini anaisema katiba kwenye mkutano wa bayana/hadhara badala ya kutumia vikao vya chama?
Kama chadema wanataka chama chao kife, basi wamkumbatie Lissu.
Dunia nzima sasa hivi imekumbatia dialogue badala ya jino kwa jino kama kule Sundani kwa aikna RSF na Jeshi, DRC na M23, Urusi na Ukraine, nk. Lissu anataka nginjangija inayopoteza watu weeeengi na mali zao badala ya dialogue.
Lissu anzisha chama chako uwe mwenyekiti.Vijana wa kisasa mna vichwa vizito sana aisee, hebu nenda kareplay ile lecture utuonyeshe wapi Simba kasema Mwenyekiti Mbowe kavunja katiba au kamtaja tu. Tunajiuliza hizi div zero zinakua zinaongezeka deile wakati watoto wanaenda shule kila siku kwa nini? Kumbe hata kusikiliza tu hamjui sasa mtacompose nini namna hii?
Lissu anahitaji kukumbushwa kwamba chadema ni mali ya mtu binafsi, si kila mtu kwakutumia hotuba majukwaani anaweza kuwa mwenyekiti (engine) ya chadema. Akaanzishe chama chake kama alivyofanya Zitto.🔥🔥🔥🔥😂😂😂😂😂😂
CHADEMA Digital yawakana Wana CHADEMA.
Nimefurahi sana leo. Mamluki na vibaraka wa mabeberu(AKA Chadema Digital) wameanza kujionyesha. Wanawakana wana CHADEMA wa Mbowe na wa Lissu.
Muwashauri wauze sera. Alooo
Siasa za kutumia nguvu ni siasa za kishamba (uncivilized) katika zama hizi. Shida yetu kubwa sio chama tawala bali mifumo inayoruhusu kiongozi kuiba na kubaki salama na mifumo mibaya ya uchumi na masoko ya kidunia. Wapinzani wamepata nafasi ya kutawala kule malawi, Zambia, Kenya, DRC, Burundi, Ethiopia, Libya, Iraq, Afghanistan, nk, lakini hali ya maisha ya wananchi huko imebaki ileile au chini zaidi. Huu ni ushahidi kuwa tatizo sio chama tawala.Hatutaki siasa za kumtumia nguvu tutapoteza maisha
Huu ushujaa wa kwenye key board umeleta matokeo gani?Hiyo dialogue iliyofanyika kwa jina la maridhiano imeleta matokeo gani?
Lissu alitolea mfano wa Mzee Mtei na Makani kuwa waliachia vijiti wengine ili kuhalalisha Mbowe kumuachia kijiti yeye pia. Hii mifano haisadifu hapa; kwanza alitakiwa kueleza kwanini Mzee mtei alimwachia kijiti Bob Makini wakati katiba haimlazimishi kuachia kijiti, kwanini Bob Makani alimwachia Mbowe kijiti wakati katiba ya chadema haikumlazimisha kuachia kijiti? Je, hawa wazee waliachia vijiti kwasababu zinazofanana au zinazotofautiana? na je, Mbowe aachie kijiti kwa Lissu kwa sababu zipi Mtei na Makani waliachia vijiti? Je, mazingira ya Mtei na Makani yaliyosababisha waachie vijiti yanafanana na haya ya Mbowe kuachia kijiti kwa Lissu? Je, sifa za kuachia kijiti ni zipi?Huu ushujaa wa kwenye key board umeleta matokeo gani?
Wapi na lini amewahi kukosoa swala la kutokuwa na ukomo? Sababu kama ni ile kauli aliyoitoa wakati anatangaza nia pale hakukosoa bali alitoa directiin na sababu.Ni lini Lissu amewahi kupendekeza kuweka ukomo kwenye uongozi wa chama cha chadema akakataliwa?
Katiba ni nyaraka ambayo kila mtu anapaswa kuijua na kuwa nayo ndiyo unataka wakaiongelee chumbani? Wewe ni mtu serious kweli au caricature?Kwanini anaisema katiba kwenye mkutano wa bayana/hadhara badala ya kutumia vikao vya chama?
Lissu ameshakuja na comebacks kadhaa abazo zilirudisha CHADEMA kwenye mstari na nyingine zikaipa nguvu zaidi. Mfano wa Karibuni kabisa ni yale maridhiano fake, lile lilikuwa ndiyo kaburi la CHADEMA, ni Lissu ndiye aliyefanya game changing. Wewe tutajie mfano wa kitu alichowahi kukiua au wapi aliiyubisha na kuigharimu CHADEMA?Kama chadema wanataka chama chao kife, basi wamkumbatie Lissu.
Wapi Lissua aliongea habari za jino kwa jino? Kwenu nyie mtu kuwa na msimamo na kutoyumbishwa na chochote ndiyo mnaita 'Jino kwa Jino?' Naona akili zenu zina utoto na ujinga wingi sana.Dunia nzima sasa hivi imekumbatia dialogue badala ya jino kwa jino kama kule Sundani kwa aikna RSF na Jeshi, DRC na M23, Urusi na Ukraine, nk. Lissu anataka nginjangija inayopoteza watu weeeengi na mali zao badala ya dialogue.
Haujaleta matokeo yoyote...Huu ushujaa wa kwenye key board umeleta matokeo gani?
Hoja yako ni dhaifu sana. Kwa hiyo, wewe unaona chama imara chenye sifa ya kuongoza serikali, sifa yake ni kuiba kura ili kishinde na wengine washindwe ili uone hawana sifa ya kuongoza serikali na si ushindani unafanya mshindi halali atangazwe, na anayeshindwa Kwa haki kubali.matokeo? Kwa mambo yanayofanyika dhidi vya vyama vya upinzani ni unfair kuviona kama bado havijajipanga, wakati huwa unaona nguvu inayorumika ya kuvidhibiti, hasa Chadema. Mtu yeyote mwenye akili timamu anaona hasa Chadema inadhibitiwa na CCM haidhibitiwi. Kwa mantiki hiyo, hakuna fair play. Labda hii ndiyo ingekuwa hoja yako kwamba kuwe na fair play ili Chadema na vyama vingine vya upinzani vijijenge zaidi na kuimariaha mfumo wa demokrasia nchini.Tusichoke na dialogue, hata akina Nyerere waliwafukuza wakoloni nchini kwa dialogue huku wakiendelea kuimarisha chama chao cha TANU. Vyama vyetu vya upinzani viko imara kiasi gani kuweza kuiongoza nchi? Tuna viongozi wanaohamahama kila siku kutafuta maslahi binafsi. Chadema ina wabunge wangapi bungeni hata wakichaguliwa kwenda Ikulu leo, au wataishia kutangaza Martial Law kama yule rais wa Korea Kusini? Tuache kudanganya watanzania vyama vyetu vya upinzani haviko tayari kuliongoza taifa, hata ofisi za kueleweka kila mkoa havina, ni kama saccos tu kila kiongozi kujitafutia maisha binafsi.
Lissu alitolea mfano wa Mzee Mtei na Makani kuwa waliachia vijiti wengine ili kuhalalisha Mbowe kumuachia kijiti yeye pia. Hii mifano haisadifu hapa; kwanza alitakiwa kueleza kwanini Mzee mtei alimwachia kijiti Bob Makini wakati katiba haimlazimishi kuachia kijiti, kwanini Bob Makani alimwachia Mbowe kijiti wakati katiba ya chadema haikumlazimisha kuachia kijiti? Je, hawa wazee waliachia vijiti kwasababu zinazofanana au zinazotofautiana? na je, Mbowe aachie kijiti kwa Lissu kwa sababu zipi Mtei na Makani waliachia vijiti? Je, mazingira ya Mtei na Makani yaliyosababisha waachie vijiti yanafanana na haya ya Mbowe kuachia kijiti kwa Lissu? Je, sifa za kuachia kijiti ni zipi?
Kinyume chake nidyo chadema itakufa. Maana kupitia sakata hili ndiyo kila mtu atajiridhisha kuwa "Chadema ni mali ya Mbowe".Kama chadema wanataka chama chao kife, basi wamkumbatie Lissu.
Nimeishaeleza humu mara kadhaa kuwa hapa Tanzania wanasiasa waliokuwa na watu ni wawili tu nao ni Nyerere na Maalim Seif basi. Kwa sasa hakuna hata mwanasiasa mmoja wa upinzani au CCM mwenye watu hivyo Lissu akiwa mmoja wao hana impact yeyote katika kulazimisha jambo. Kenya kila mwanasiasa ana watu ila wanatofautiana idadi tu ndiyo maana wanaweza kuleta impact kwa suala lolote. Uganda Bob Wine ana watu.Haujaleta matokeo yoyote...
Ndyomaana Lisu alionya kuhusu ‘mashujaa wa mtandaoni' kwamba hiyo mbinu haina manufaa na njia sahihi ni kuanzisha na kupambana kwa nguvu ya uma.
Kweli tupu Lisu alikosea snNi lini Lissu amewahi kupendekeza kuweka ukomo kwenye uongozi wa chama cha chadema akakataliwa?
Kwanini anaisema katiba kwenye mkutano wa bayana/hadhara badala ya kutumia vikao vya chama?
Kama chadema wanataka chama chao kife, basi wamkumbatie Lissu.
Dunia nzima sasa hivi imekumbatia dialogue badala ya jino kwa jino kama kule Sundani kwa aikna RSF na Jeshi, DRC na M23, Urusi na Ukraine, nk. Lissu anataka nginjangija inayopoteza watu weeeengi na mali zao badala ya dialogue.
Binadamu ni wepesi wa kusahau snBila Mbowe saa hizi lissu angekuwa shimo la Tewa !
CHADEMA haitakufa na itaendelea kuwa na wanachama na mashabiki; dola iliishashindwa kuiua CHADEMA kwa kutumia mifumo na vyama vibaraka kikiwemo ACT.Kinyume chake nidyo chadema itakufa. Maana kupitia sakata hili ndiyo kila mtu atajiridhisha kuwa "Chadema ni mali ya Mbowe".
Basi sawa. Wacha tuone, muda utaongea mkuu. Hofu yangu ninkwamba Mbowe akishinda tena uenyekiti atabakia mpweke kama Lipumba na CUF yake.CHADEMA haitakufa na itaendelea kuwa na wanachama na mashabiki; dola iliishashindwa kuiua CHADEMA kwa kutumia mifumo na vyama vibaraka kikiwemo ACT.
Baada ya uchaguzi wao wa kitaifa Januari 2025 wagombea uchaguzi maslahi wote watakaokuwa wameshindwa watatimka na Mbowe kwa kuwa atashinda ataendelea kuipaisha zaidi CHADEMA.
CCM itaendelea kuzuia uchaguzi halali usifanyike kwa kuengua zaidi ya asilimia 50 ya wagombea wa CHADEMA na pia kura bandia na kutomtangaza mshindi kwani hapo ndipo salama yake ilipolala.
Iko hivi, kuna mwamba aliwafungia kabisa msifanye siasa na kweli mlikuwa hamfanyi siasa. mara paaaap!! akaja mtu akawafungulia mfanye siasa na bado akaja na 4Rs zake na R moja ikahusu maridhiano na nyingine ikiwa mabadiliko. Mtu wa hivi alipaswa kupokelewa na kukumbatiwa na watu wa upinzani ambao ni smart, wenye akili, wenye maarifa, wenye heshima, wenye uelewa, wazalendo, na wenye nia njema na nchi yao. Kilichotokea ni kwamba baada ya kufunguliwa kufanya siasa basi yalifunguliwa matusi, kejeli, hasira za matukio ya nyuma, vurugu na ujuaji mwingi uliopitiliza kana kwamba hawajui kwamba katiba hii inampa nguvu kubwa Rais aliyeko madarakani ya kufanya yasiyo na idadi bila kuhojiwa wala kuulizwa na chombo chochote ndani ya nchi. Wangekubali kujishusha, kuheshimu, kuwa wasikifu na kukumbatia siasa zenye staha za kuheshimu mamlaka, demokrasi, uchumi, utamaduni wetu na mustakabali wa taifa letu lazima kungetokea a "win-win" and "lose-lose" situation.Huu ushujaa wa kwenye key board umeleta matokeo gani?