SI KWELI Lissu amesema wahariri walipewa fedha kuiharibia CHADEMA uchaguzi

SI KWELI Lissu amesema wahariri walipewa fedha kuiharibia CHADEMA uchaguzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu wa JamiiCheck ni kweli Lissu amesema wahariri walipewa fedha kuiharibia CHADEMA uchaguzi?
JamiiCheck Template_20250305_194530_0000.jpg
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mnamo tarehe 02 Machi 2025 pamoja na viongozi wengine wa chama hicho walifanya mkutano na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) makao makuu ya Chama.

Madai
Kumekuwapo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kuchapishwa na Jambo TV kuwa kupitia mkutano huo Lissu alisema wahariri walipewa fedha kuiharibia CHADEMA uchaguzi.

Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa Taarifa hiyo Si ya Kweli kwani Lissu hakutoa kauli hiyo, pia haijachapishwa na Jambo TV.

Akizungumza katika mkutano huo kuhusu kupigania mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi aliwataja wahariri kama sehemu ya wadau wakubwa ambao wanaweza kuchochea kufanikiwa kwa mapambano hayo.

"Hapa hatutazungumza sera zingine tutazungumza habari ya uchaguzi kwasababu tunatekeleza maamuzi ya chama chetu (CHADEMA), tunataka (Wahariri) mtuelewe, tunataka mkituelewa kama mnakubaliana na sisi na nyinyi muwe sehemu ya mapambano haya,"

"Vyombo vya habari ni sehemu muhimu sana ya mapambano haya na ni sehemu muhimu vilevile ya ukandamizaji, kwasababu wanaokandamiza si tu wanakandamiza vyombo vya habari lakini vilevile wanataka kuweka vyombo vya habari viwasaidie katika ukandamizaji wao."

"Vyombo vya habari vinaweza kutumika kama daraja la ukombozi na vinaweza kutumika na vimetumika katika historia kama vyombo vya ukandamizaji. Tunataka vyombo vya habari vya Tanzania vichague upande wa kuwa vyombo vya ukombozi, vyombo vya kuleta demokrasia katika nchi ya Tanzania."

Attachments

  • 1741153908911.png
    1741153908911.png
    402.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom