Lissu anaipenda sana Zanzibar lakini hawajitambui

Lissu anaipenda sana Zanzibar lakini hawajitambui

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Hebu tumsikilize hapo akiwa Zanzibar Mheshimiwa Lissu, ni dhahiri anaipenda Zanzibar ijitambue na kupata uhuru wake wa kweli badala ya kukubali kutawaliwa na Tanganyika (Dodoma) na kuveshwa kilemba cha ukoka.

Wazenji wamuunge mkono ndio ukombozi wao uko hapo.

PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?
 
Wazanzibari udini umefifisha upeo wa akili zao, hivyo nakupelekea ubaguzi.

Watanganyika ni weziwezi sana. Barozi wa nyumba 10 hadi kwenye serikali kuu.
 
Inasikitisha...

Kadiri siku Zinavyotaradadi...

Ndivyo Upinzani unavyozidi kudorora...
 
Inasikitisha...

Kadiri siku Zinavyotaradadi...

Ndivyo Upinzani unavyozidi kudorora...
Upinzani unadorora? Labda ukizungumzia matumizi ya nguvu maanabwao hawana dola, lakini kama ni matumizi ya hoja basi hata wewe hujitambui!
Umemsikia mzee Kinana akijibu hoja za Lissu? Ni kama kijana wa form two B wakati yeye ni mkongwe na hiyo maana yake "Kinana amedorora kisiasa"
 
Mnakubalije kuwekewa watawala kutokea Dodoma? Na watokeapo wanao wasemea kuhusu haki zenu za kimsingi mbawaona hawafai?
Jee huko ni kujitambua?
kwa hivyo ni wazanzibari kutojitambua au ni mfumo uliopo? Unakumbuka January 27 mwaka 2001 nini kilitokea?
 
Hebu tumsikilize hapo akiwa Zanzibar Mheshimiwa Lissu, ni dhahiri anaipenda Zanzibar ijitambue na kupata uhuru wake wa kweli badala ya kukubali kutawaliwa na Tanganyika (Dodoma) na kuveshwa kilemba cha ukoka.
Wazenji wamuunge mkono ndio ukombozi wao uko hapo.
Zanzibar wanatunyonya haswa
 
Upinzani unadorora? Labda ukizungumzia matumizi ya nguvu maanabwao hawana dola, lakini kama ni matumizi ya hoja basi hata wewe hujitambui!
Umemsikia mzee Kinana akijibu hoja za Lissu? Ni kama kijana wa form two B wakati yeye ni mkongwe na hiyo maana yake "Kinana amedorora kisiasa"
Kinana anatuhuma nyingi hivyo hawezi kuwa na hoja ya msingi yoyote
 
Upinzani unadorora? Labda ukizungumzia matumizi ya nguvu maanabwao hawana dola, lakini kama ni matumizi ya hoja basi hata wewe hujitambui!
Umemsikia mzee Kinana akijibu hoja za Lissu? Ni kama kijana wa form two B wakati yeye ni mkongwe na hiyo maana yake "Kinana amedorora kisiasa"

Upinzani Kama Upinzani unaenda Ukisinzia...

Unaweza Kulinganisha Vipindi vilivyopita enzi za Katibu CDM Wilbroad Silaa..

Kipindi cha E.Lowasa( Japo huyu aliingia Kwa gea Ya Angani)

Na Kipindi cha sasa...!

Japo Maandamano yameruhusiwa Lkn tunafanya kustukizwa utasikia ' Jana watu waliandamana'..!

CCM wamejua jinsi ya Kuwatuliza Viongozi wetu,kuwarambisha Asali.Hakuna Vibe..
 
Hebu tumsikilize hapo akiwa Zanzibar Mheshimiwa Lissu, ni dhahiri anaipenda Zanzibar ijitambue na kupata uhuru wake wa kweli badala ya kukubali kutawaliwa na Tanganyika (Dodoma) na kuveshwa kilemba cha ukoka.

Wazenji wamuunge mkono ndio ukombozi wao uko hapo.
View attachment 2982250
Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.

1. Wazanzibar wengi sana wanamiliki ardhi na majengo bara, kama raia. ila Wabara wanachukiwa wakienda kule, wanaitwa chogo, na katiba yao inazuia watu wa bara kumiliki ardhi. Juzi nilikuwa Dodoma, kwenda benjamin Mkapa kwenye kona ya Udom, kuna migorofa fulani hivi imejengwa, wanasema karibu na vile vijengo vya majaji, wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni nini?

2. kwenye ajira, hii ni kero, wazanzibar maelfu na maelfu wameajiriwa bara, hata kwenye mambo yasiyo ya muungano, wameajiriwa bara ambayo kiukweli ipo bara kwasababu zanzibar kuna utawala wao, lakini wabara hawaruhusiwi kabisa kuajiriwa zanzibaar, hii ni kero, inatakiwa iondolewe, ama la kila mtu abaki kwake.

3. wazanzibar wanakuwa wabunge kule kwao, na huku. akiwa mbunge kule kwao, atakula masurufu ya kule na atakuja kula masurufu ya bara kwa kodi za watu wa bara. tuambieni, yale mipesa wanaku wabunge 50 wa zanzibar wanakiula, zanzibar huwa imechangia bei gani? ni pesa za walipa kodi wa bara. na hao hao wakifika huku wakishiba, wanasenma twende kule kwa passport, kwa msiojua, kile ameongea yule mbunge wa zanzibar kwamba wabara twende kwa passport kwao ndicho kilichopo kwenye mioyo ya wazanzibari wote hata wenye mamlaka huku na hata walioajiriwa huku na hata wanaomiliki ardhi huku, amesema kilichopo kwenye mioyo ya wengi. wala hatakiwi kulaumiwa. kwa waliofika zanzibar wanajua kuwa hicho ndio huwa matamanio yao.

4. mzanzibar anaweza kuwa Mkuu wa wilaya, mkoa, na waziri bara, ila sisi kule marufuku. kwanini?

nimeongea hayo kwa uchache tu, lakini ukweli mwingi hata wanaopinga wanaujua, kama tunataka muungano uwepo, ondoeni kero hizi kwa watu wa bara, ama la, kila mtu achukue hamsini zake kwasababu hakuna kitu wabara wanafaidika nacho as of now. na hawajawahi kufaidika. watu wasioelewa watasema huu ni uchochezi, ila jibuni kwa hoja kama mnazo.
 
Upinzani Kama Upinzani unaenda Ukisinzia...

Unaweza Kulinganisha Vipindi vilivyopita enzi za Katibu CDM Wilbroad Silaa..

Kipindi cha E.Lowasa( Japo huyu aliingia Kwa gea Ya Angani)

Na Kipindi cha sasa...!

Japo Maandamano yameruhusiwa Lkn tunafanya kustukizwa utasikia ' Jana watu waliandamana'..!

CCM wamejua jinsi ya Kuwatuliza Viongozi wetu,kuwarambisha Asali.Hakuna Vibe..
upinzan sio kupiga kelele majukwaani , kwasasa upinzan ni mkubwa sema umegubikwa na hofu tu , siku hofu ikiondoka hatutokaa kuiona amani haki za wananchi zipatikane
 
Back
Top Bottom