Uchaguzi 2020 Lissu anakatwa na NEC kwa kipengele kipi cha Sheria?

Uchaguzi 2020 Lissu anakatwa na NEC kwa kipengele kipi cha Sheria?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Tuacheni propaganda rahisi kiasi hicho zisizokua na kichwa wala miguu. Unapolalamika kua Lissu anakatwa na NEC kwa kipengele kipi cha Sheria? Taja hicho kifungu hapa hapa usiwe muongo muongo na mpotoshaji.

Kwa wanaodai kuwa alianza kampeni mapema hawajui sheria wanafanya propaganda. Hakuna kitu kinachoitwa kampeni kabla ya kampeni. Alichofanya Mhe Lissu ni mikutano ya kawaida tu wakati anatafuta wadhamini wake. Labda msema kafanya mkutano kinyume na sheria kama kuna kifungu kinazuia kufanya mikutano ya hadhara kitu ambacho hakipo.

Niwatoe hofu kuwa Lissu hawezi kukatwa na hakuna sababu ya kufanya hivyo na siyo kwa sababu eti NEC wanamuogopa au wanaogopa kutokea vurugu, yatakatwa kwa sababu hajavunja Sheria ya Uchaguzi. Ataachwa apambane kama walivyo wagombea wengine.
 
...true, hawezi katwa.

original plan ilikuwa akatwe but political landscape ilivyobadilika ndani ya hizi siku 10 imelazimisha mipango yote ipinduke kichwa chini miguu juu!
 
...true, hawezi katwa.

original plan ilikuwa akatwe but political landscape ilivyobadilika ndani ya hizi siku 10 imelazimisha mipango yote ipinduke kichwa chini miguu juu!
Wanamuogopa mwanasheria wake chezea the Hague
 
Bahati mbaya sana Mkuu Tanzania HAKUNA SHERIA kama tungekuwa na sheria MAOVU na UDHALIMU mbali mbali tangu 2015 ambao umewaumiza Watanzania wengi sana USINGETOKEA.
 
Magufuli amezoea KUKIMBIA washindani wake tangu akiwa Mbunge, safari asijaribu kutuletea michezo yake hiyo ni lazima AKUBALI KUJIPIMA na washindani wake akiwemo Lissu.
 
Akishakatwa ni lazima watataja sababu na hicho kifungu, hivyo subiri na usiwe na papara mpaka sasa hivi hajakatwa bado, labda anaweza kuwa na bahati akapita au asiwe na bahati wakakata, ...
 
Lisu atapigwa mbele na nyuma hata amini yeye na yule beberu wake amsterdam watavuna aibu ya miaka 5.

Watz siyo wajinga kama walivyo wana chadema
Yawekeni sawa na wazi ili washindwe kihalali bila figisu coz uhakika wa ushindi upo sababu mmefanya makubwa kuliko hata aliyofanya mkoloni tangu nchi hii kuumbwa.Hadi tumefika uchumi wa Kati toka mlo mmoja kwa siku Hadi tunasaza Milo 4 kwa siku
 
Akishakatwa ni lazima watataja sababu na hicho kifungu, hivyo subiri na usiwe na papara mpaka sasa hivi hajakatwa bado, labda anaweza kuwa na bahati akapita au asiwe na bahati wakakata, ...
Kesho sio mbali hofu ya nn
 
Issue ni kuwa Lipumba na Shibuda watatoa mapingamizi ambayo inabidi ayajibu and he will not be available to respond to them. Hivyo kukatwa kwa kushindwa to respond to accusations raised against him

Atakuwa segelea hahaha
 
Back
Top Bottom