Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Sera ya majimbo ni ya kibepari.

Tanzania limekua katika misingi ya kijamaa, hatutaiweza.

Hii ilipaswa kuanza wakati tunapata uhuru sio leo.
 
Hii hoja ya majimbo ccm imewakamata pabaya sana.Kila siku wanatapa tapa bila kuwa na point mtambuka.
Ukweli ni kwamba mfumo wa majimbo ni mzuri tunataka tuchague gavana ili akizingua tunampiga chini.

Sent from my SM-J730GM using JamiiForums mobile app
 
Mfumo wa majimbo unategemeza Utawala wa Sheria ambao ni takwa muhimu kwa wananchi kuweza kujiletea maendeleo.

Ni wazi kuwa mfumo wa serikali kuu, mikoa na wilaya uliasisiwa na unaungwa mkono na watawala ambao wanaishi na kunufaika na utawala kiimla wa kutoka juu kwenda chini.
 
Wewe pimbi sikiliza soma kwanza USA wanaendeshaje majimbo usiongee ujinga wako hapa
 
Wewe pimbi sikiliza soma kwanza USA wanaendeshaje majimbo usiongee ujinga wako hapa
Kila Jimbo linajitegemea ndio maana Kuna majimbo Marekani yenye umaskini wa kufa mtu na yako mengine matajiri kupita maelezo
 
Ndio maana ilipigwa chini bungeni.
Mkuu, katiba ya Warioba haikupigwa chini bungeni. Kilichofanyika CCM walibadili baadhi ya vipengere ... Wapinzani wakasusia. Pamoja na CCM kuikamilisha wao wenyewe bado wameshindwa kuileta kwa Wananchi waamue!!
 
Suala la majimbo ni cha “kike”, litauvunja nchi vipande vipande.
 
Wewe pimbi sikiliza soma kwanza USA wanaendeshaje majimbo usiongee ujinga wako hapa

USA ilipigana civil war, ni nchi iliyojengwa kwa misingi ya ubaguzi wa rangi.

Huwezi ukayalinganisha majimbo yao na hizi ndoto za alinacha za Lissu.
 
Kwahiyo majimbo ya wapinzani hamna raslimali ndiyo maana ayaendelei?
Mbona ata kwasasa tunajimbulusha tunapotokea...mfano Jembe letu JPM anaongea Kisukuma ili wapate kura za wasukuma wote
 
lissu ni mgombea wa hovyo kabisa kuwahi kutokea toka mfumo wa vyama vingi uanzishwe
 
Kwani gharama za uendeshaji mikoa na wilaya zinatoka wapi
Sasa hivi zinatoka serikali kuu kuhudumia hata Mikoa michovu isiyo na utajiri Kama Singida ambao tegemeo kuu Ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti
 
..kama hiyo ndiyo hofu yako basi tulitakiwa tusiwe na mikoa, wilaya, na hata vijiji.

..mbona mataifa yenye mfumo wa majimbo wananchi wake ni wazalendo na wana moyo wa utaifa?

..Uzalendo ktk nchi yoyote ile unafifishwa na ukosefu wa haki na matumaini kwa wananchi
 
Halima sio kazi yake kuleta maendeleo kawe hilo ni jukumu la mkusanya kodi
 
Serikali za majimbo zitayanyanyapaa baadhi ya majimbo na kuyapandisha hadhi mengine.

Asikudanganye mtu kwamba eti majimbo yatakuwa na uwezo wa kujisimamia na kujiletea maendeleo.
 
Serikali za majimbo zitayanyanyapaa baadhi ya majimbo na kuyapandisha hadhi mengine.

Asikudanganye mtu kwamba eti majimbo yatakuwa na uwezo wa kujisimamia na kujiletea maendeleo.

..mbona sasa hivi kuna mikoa na wilaya?

..Je, kuna mkoa au wilaya unanyanyapaa mkoa au wilaya nyingine?

..Kwa mfano, wilaya ya Kinondoni imewahi kunyanyapaa wilaya ya Ilala?

..Au mkoa wa Geita umewahi kunyanyapaa mkoa wa Shinyanga, au Simiyu?

..hata wakati wa mkoloni na mara baada ya uhuru majimbo hayakuwa na matatizo.

..wananchi waliweza kutoka jimbo moja kwenda lingine kutafuta fursa.

..pia wapo watumishi wa serikali walikuwa wakihamishwa toka jimbo moja kwenda lingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…