Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

Uchaguzi 2020 Lissu anaongelea tu Serikali za Majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji zitatoka wapi

..asante.

..lakini pia siyo lazima tuwe na mfumo wa majimbo 100% kama wanavyouelezea CDM.

..vilevile siyo lazima tuwe na mfumo centralized 100% kama huu waliotuletea CCM.

..mimi kuna details ambazo zisipendi ktk mfumo uliopendekezwa na CDM, lakini nakubaliana na malengo makuu na vision ya mfumo huo.

..kwa upande wa CCM naona huu mfumo umepitwa na wakati, ni very un-democratic, na umelenga kukitumia chama tawala kuliko wananchi.

..actually, sipendi kuwaona CDM wakiingia madarakani na kuutumia mfumo huu dhidi ya CCM na vyama vingine.

..tuchukue mazuri yaliyoko ktk mfumo wa sasa, tuchanganye na mazuri yaliyoko ktk mfumo unaopendekezwa, ndipo tupate mfumo utakaotufaa sisi na vizazi vijavyo.
Inshaallah haya yamewekwa mikononi mwetu ili tuyatatue.

Kwa hitimisho lako nadhani tuko mahali salama. Tunapaswa kuzungumza zaidi na kwa uwazi.

Ahsante sana Mkuu.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Gharama za uendeshaji wa serikali za majimbo utakuwa ni sawa kabisa na kama inavyoendeshwa hivi sasa na serikali kuu. Na vyema ikaeleweka ya kuwa, kwa uwepo wa serikali za majimbo, itakuwa si kwamba fedha zote zipatikanazo kutoka katika jimbo husika zitatumika zote hapi hapo tu. La hasha! Kwa yale majimbo yenye mapato zaidi ya mahitaji yao sehemu ya fedha zake zitapelekwa serikali kuu kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli zake, na pia kuyapiga jeki majimbo mengine yenye changamoto zaidi za kifedha. Mfumo huu unatoa fursa nzuri za usimamizi wa rasilimali za taifa vizuri zaidi. Wanaosema kutakuwa na vurugu ni wale wasiotaka viongozi kuwajibika kwa maamuzi wanayofanya yasiokuwa na tija. Nchi kama Nigeria, Kenya, Zambia na Africa Kusini wanafuata mfumo huo na utaifa wao haujaterereka hata kidogo. Tusing'ang'anie mfumo usio na tija kwa watu wote.
 
Back
Top Bottom