Kama Taifa tusingeabolish Uchifu leo tungekuwa na vijiserikali vingiii ambavyo vingekuwa na maoni tofauti tofauti na huenda hili la majimbo lingewezekana... Maana haya huja ku hamornize co-existance kunapokuwa na more than one group of unified interest. Haina tofauti na kuwa na serikali ya mseto.
Majimbo kwa sasa sioni mantiki yake. Hakuna mpasuko wa kitaifa, wachanga wamewekeza kwa wagogo na Wahehe wanafanya kazi na wasukuma wajita wako na wabondei. Kwa namna fulani kwa sasa watanzania ni wamoja.
Kwa rasilimali chache zilizopo zikielekezwa Mbeya wapo wasukuma wanaonufaika zikielekezwa mwanza wapo wagogo na wazaramo wanaonufaika zikiwekwa DSM wako wachaga na wabena wananufaika.
Kuondoa chuki, tamaa, sioni kwann watu watake rasilimali zao pekee ziwanufaishe wao pekee ikiwa tumeamua kuwa wamoja!?! Kuna dhana ya majimbo tajiri kuyasaidia masikini ..hili haliwezekani.. pesa haijawahi kujaa hata siku moja na matatizo hayakomi... Ingekuwa ni rahisi kusingekuwa na majimbo masikini USA.
Mie nadhani haya ni mawazo ya kuweka mbali kabisa kwa mustakabali wa Taifa. Kama haridhiki na muundo wa jamhuri yetu, tuangazie hapo na tulete mapendekezo ya maboresho. Sio turudi tena kuanza kujigawa .. Maumivu ya kichwa huanza taratibu hiki tunachokililia kitatuchoma tutashangaa.
Kuna watu wanaizungumzia Kenya Kenya zilikuwemo serikali za kikabila.. na zinalinda interest za kikabila. Ziliachwa na zikakua sasa hapo hawana namna zaidi ya kuzitambua kwao serikali ya kijimbo ni solutions maana nchi msingi wake ni Umimi. Mkikuyu hataki kutawaliwa na Mkisii, Mluhya hataki kuwaliwa na Mkamba. Hakuna namna zaidi ya kuwaachaa wajitawale chini ya mwamvuli mmoja wa Kenya..
Lakini hata hivyo inapokuja kuwa head of state bado unaona clashes.. kwa sababu kila moja ataka kuwa mkubwa. Hii sio approach bora kwa matarajio ya muda mrefu ya taifa imara na lenye umoja. Tusijitumbukize huko.. dhambi ya kujitenga hauishii hapo kwenye majimbo... Huko mbele watu wataulizana we ni wa ukoo gani.
Asubuhi Njema.
Sent from my Infinix X650 using
JamiiForums mobile app