Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Tanzania ya leo sio ile ya miaka ya nyuma ambayo watu wengi walikuwa hawawezi kupata habari kwa urahisi kama ilivyo hii ya leo. Miaka ya nyuma radio station ilikuwa moja tu na hata Tv stations hazikuwepo,pia radio stations za watu binafsi nyingi hazikuwepo,hivyo upatikanaji wa habari ulikuwa mgumu na hivyo ilikuwa rahisi kuwapotosha watu
Leo hii utampotosha nani? Karibu kila familia mijini na vijijini ina Tv set na kila mwanafamilia ana simu janja ambayo inauwezo wa kumpatia habari anayoyote anayoitaka. Kipindi hiki cha uchaguzi wananchi wanapata habari kwa urahisi sababu teknolojia imekuwa na hivyo kila hoja na sera za mgombea wananchi wanazipata.
Mgombea urais kwa Chadema, Tundu Lissu amekuwa akisikika kila mahala anapofanya kampeni zake kuwa rais aliyepo madarakani amefifisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani na mataifa ya nje. Kisa tu huwa hafanyi safari za nje mara kwa mara. Hii hoja amekuwa akisisitiza mno kiasi kwamba watu wamekuwa wakimshangaa.
Ziara ya rais wa Burundi ndugu Evarist Ndaishiaye imemuumbua huyu ndugu Tundu Lissu,maana kama nchi haina mahusiano mazuri ya kidiplomasia na majirani au mataifa ya nje rais wa Burundi angekuja leo Tanzania kufanya ziara ya kikazi ambayo ina manufaa makubwa kwa taifa letu? Kama Tanzania ina mahusiano mabaya na majirani zake Burundi ingeweza kufanya makubaliano ya kuanzisha mchakato wa kujenga kinu cha kuchenjulia nickel kwa pamoja na Tanzania? Mbali na ziara ya rais wa Burundi ambae amefanya ziara leo,je ziara ya rais Museveni? Sio uhusiano mzuri wa kidiplomasia na majirani?
Leo bomba la mafuta litapita hapa Tanzania na taifa letu litanufaika kimapato.Biashara baina ya Burundi na Tanzania kwa sasa ni zaidi ya bil 201. Je wakianza kuuza dhahabu mkoani Kigoma kwenye soko la dhahabu itakuwaje?
Mimi binafsi naona ndugu Lissu hakujiandaa kugombea urais vizuri na itakuwa jambo la ajabu wakazi wa mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla kuchagua mtu ambae haoni mahusiano mazuri ya taifa letu na nchi za nje amabayo yanaliletea taifa letu manufaaa makubwa. Hii hoja potofu kuwa JPM amefanya mahusiano ya kimataifa kuwa mabaya ni sababu tosha kumnyima kura huyu mgombea maana ni muongo na mzandiki.