Uchaguzi 2020 Lissu anazidi kuumbuka, kila hoja anayoanzisha inaonekana haina mashiko kwa Watanzania

Tanzania ya leo sio ile ya miaka ya nyuma ambayo watu wengi walikuwa hawawezi kupata habari kwa urahisi kama ilivyo hii ya leo. Miaka ya nyuma radio station ilikuwa moja tu na hata Tv stations hazikuwepo,pia radio stations za watu binafsi nyingi hazikuwepo,hivyo upatikanaji wa habari ulikuwa mgumu na hivyo ilikuwa rahisi kuwapotosha watu

Leo hii utampotosha nani? Karibu kila familia mijini na vijijini ina Tv set na kila mwanafamilia ana simu janja ambayo inauwezo wa kumpatia habari anayoyote anayoitaka. Kipindi hiki cha uchaguzi wananchi wanapata habari kwa urahisi sababu teknolojia imekuwa na hivyo kila hoja na sera za mgombea wananchi wanazipata.

Mgombea urais kwa Chadema, Tundu Lissu amekuwa akisikika kila mahala anapofanya kampeni zake kuwa rais aliyepo madarakani amefifisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani na mataifa ya nje. Kisa tu huwa hafanyi safari za nje mara kwa mara. Hii hoja amekuwa akisisitiza mno kiasi kwamba watu wamekuwa wakimshangaa.

Ziara ya rais wa Burundi ndugu Evarist Ndaishiaye imemuumbua huyu ndugu Tundu Lissu,maana kama nchi haina mahusiano mazuri ya kidiplomasia na majirani au mataifa ya nje rais wa Burundi angekuja leo Tanzania kufanya ziara ya kikazi ambayo ina manufaa makubwa kwa taifa letu? Kama Tanzania ina mahusiano mabaya na majirani zake Burundi ingeweza kufanya makubaliano ya kuanzisha mchakato wa kujenga kinu cha kuchenjulia nickel kwa pamoja na Tanzania? Mbali na ziara ya rais wa Burundi ambae amefanya ziara leo,je ziara ya rais Museveni? Sio uhusiano mzuri wa kidiplomasia na majirani?
Leo bomba la mafuta litapita hapa Tanzania na taifa letu litanufaika kimapato.Biashara baina ya Burundi na Tanzania kwa sasa ni zaidi ya bil 201. Je wakianza kuuza dhahabu mkoani Kigoma kwenye soko la dhahabu itakuwaje?

Mimi binafsi naona ndugu Lissu hakujiandaa kugombea urais vizuri na itakuwa jambo la ajabu wakazi wa mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla kuchagua mtu ambae haoni mahusiano mazuri ya taifa letu na nchi za nje amabayo yanaliletea taifa letu manufaaa makubwa. Hii hoja potofu kuwa JPM amefanya mahusiano ya kimataifa kuwa mabaya ni sababu tosha kumnyima kura huyu mgombea maana ni muongo na mzandiki.
Tundu Lissu kawashika MATAGA kunako dadeki!
 
Kama hujui athari katika mahusiano ya kidiplomasia yaliyosababishwa na utawala huu, kiasi cha kuanzisha thread kutetea ukitumia tu ziara ya Rais wa Burundi, suala la elimu ni lazima lihusike hapa!
Nitajie ubalozi au jumuia ya kimataifa iliyovunja uhusiano na Tanzania?
 
Tumbo joto? Ziara ya Ndiashaye ni muhimu sana kwa taifa letu. JPM is the best.

Umuhimu gani kwa Taifa? Ni muhimu kwenye kampeni za ccm na si kwa Taifa. Hawa watu wametokea ukanda mmoja hivyo wana siri nzito
 
Bro mimi la saba tu, ila nimemsikia Lissu akinadi sera zake anadai JPM ameua diplomatic relations ya Tanzania. Lakini sio kweli mfano ni ziara ya Leo ya rais wa Burundi.
Burundi hana msaada wowote kwetu hata ikitokea shida hawezi hata kutushauri.
Tunachotaka ni mahusiano mazuri ya kidiplomasia kimataifa, tuwe huru na hili tusishangilie uwe Ccm au upinzani siyo jambo la kheri kwa taifa letu.
Tukitengeneza taifa la kidikiteta tutaua misingi ya utu na hapa tutaweka matabaka ambayo yataligharimu taifa miaka mingi umwagikaji wa damu.
Tusifike huko Mungu atusaidie Magufuli abadilishe mtazamo wake atengeneze Tanzania ya umoja wa kitaifa na kimataifa.
 
Burundi hawana msaada kwetu? Upo sawa wewe? Mizigo yao 95% inapitia hapa Tanzania. Hiyo nickel ikianza kuchimbwa na kusafishwa,manufaa yake unayajua?
 
Mimi nimezaliwa na kukulia ngara hiyo Nikel yenyewe tangu miaka ya 1990 wanachimba sijui kama bado ipo, mizigo ya Burundi haipiti kwetu, kwasababu ya kuwa na urafiki nao hasha hii ni biashara hata kama tutakuwa hatuna urafiki biashara tutafanya.
Burundi ni Ndg zetu wa damu kule Kagera na Kigoma mipaka ipo wazi tunaingiliana tunaoana na kutembeleana
Mimi kabila langu ni Myango-Mzilankende na nina ndugu wa ukoo Burundi na Rwanda wa ukoo wa Bayango-Bazilankende miaka ya 90 tulikuwa na mikutano kutembeleana ila kwa sasa sijui kwa kuwa siishi huko.
Burundi anatutegemea sisi kwa kiasi kikubwa lakini sisi hatutegemei kwenye uchumi wetu hata 0.01% hachangii.
 
NAWAKUMBUSHA TU WAKUU.

Tanzania ni moja kati ya The Poorest Countries in the World (MASIKINI ZAIDI DUNIANI) inashika nafasi ya 8 kutoka chini. ( Focus economy 2019- 23)
MIAKA 60 YA UHURU.

CCM imetufikisha hapa
Tanzania ni tajiri sana duniani ,tatizo lilikuwa namna ya kuuvuna utajri huo na kuusimamia kwa manufaa ya watu wetu,kapatikana mwenye kufahamu hilo na uwezo wa kulifanyia kazi ,si mwingine bali ni Dr John Pombe Magufuli .
Ziara za kutembeza bakuri ughaibuni na kurudi na vyandarua sio dili tena
 
Kwa hiyo rais wa Burundi kuja hapa ndio umehitimisha jiwe ana mahusiano mazuri kimataifa
 
Kwa lissu mafanikio ya kidplomasia kwa awamu hii ni hadi mfalme wa ubelgiji atue Dar
 
Tanzania ya leo sio ile ya miaka ya nyuma ambayo watu wengi walikuwa hawawezi kupata habari kwa urahisi kama ilivyo hii ya leo. Miaka ya nyuma radio station ilikuwa moja tu na hata Tv stations hazikuwepo,pia radio stations za watu binafsi nyingi hazikuwepo,hivyo upatikanaji wa habari ulikuwa mgumu na hivyo ilikuwa rahisi kuwapotosha watu

Leo hii utampotosha nani? Karibu kila familia mijini na vijijini ina Tv set na kila mwanafamilia ana simu janja ambayo inauwezo wa kumpatia habari anayoyote anayoitaka. Kipindi hiki cha uchaguzi wananchi wanapata habari kwa urahisi sababu teknolojia imekuwa na hivyo kila hoja na sera za mgombea wananchi wanazipata.

Mgombea urais kwa Chadema, Tundu Lissu amekuwa akisikika kila mahala anapofanya kampeni zake kuwa rais aliyepo madarakani amefifisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani na mataifa ya nje. Kisa tu huwa hafanyi safari za nje mara kwa mara. Hii hoja amekuwa akisisitiza mno kiasi kwamba watu wamekuwa wakimshangaa.

Ziara ya rais wa Burundi ndugu Evarist Ndaishiaye imemuumbua huyu ndugu Tundu Lissu,maana kama nchi haina mahusiano mazuri ya kidiplomasia na majirani au mataifa ya nje rais wa Burundi angekuja leo Tanzania kufanya ziara ya kikazi ambayo ina manufaa makubwa kwa taifa letu? Kama Tanzania ina mahusiano mabaya na majirani zake Burundi ingeweza kufanya makubaliano ya kuanzisha mchakato wa kujenga kinu cha kuchenjulia nickel kwa pamoja na Tanzania? Mbali na ziara ya rais wa Burundi ambae amefanya ziara leo,je ziara ya rais Museveni? Sio uhusiano mzuri wa kidiplomasia na majirani?
Leo bomba la mafuta litapita hapa Tanzania na taifa letu litanufaika kimapato.Biashara baina ya Burundi na Tanzania kwa sasa ni zaidi ya bil 201. Je wakianza kuuza dhahabu mkoani Kigoma kwenye soko la dhahabu itakuwaje?

Mimi binafsi naona ndugu Lissu hakujiandaa kugombea urais vizuri na itakuwa jambo la ajabu wakazi wa mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla kuchagua mtu ambae haoni mahusiano mazuri ya taifa letu na nchi za nje amabayo yanaliletea taifa letu manufaaa makubwa. Hii hoja potofu kuwa JPM amefanya mahusiano ya kimataifa kuwa mabaya ni sababu tosha kumnyima kura huyu mgombea maana ni muongo na mzandiki.
Taarifa zenye maelekezo kiandikwe Nini na kisiandikwe Nini kwa malengo ya kuwarubuni watu?
 
Mimi nimezaliwa na kukulia ngara hiyo Nikel yenyewe tangu miaka ya 1990 wanachimba sijui kama bado ipo, mizigo ya Burundi haipiti kwetu, kwasababu ya kuwa na urafiki nao hasha hii ni biashara hata kama tutakuwa hatuna urafiki biashara tutafanya.
Burundi ni Ndg zetu wa damu kule Kagera na Kigoma mipaka ipo wazi tunaingiliana tunaoana na kutembeleana
Mimi kabila langu ni Myango-Mzilankende na nina ndugu wa ukoo Burundi na Rwanda wa ukoo wa Bayango-Bazilankende miaka ya 90 tulikuwa na mikutano kutembeleana ila kwa sasa sijui kwa kuwa siishi huko.
Burundi anatutegemea sisi kwa kiasi kikubwa lakini sisi hatutegemei kwenye uchumi wetu hata 0.01% hachangii.
Mh...! Mradi wa kabanga nickel ulishaaanza? Pale kuna mgodi? Kama biashara kati ya Tanzania na Burundi ni bil 200,unasema hakuna mchangi hapo?
 
Tanzania ya leo sio ile ya miaka ya nyuma ambayo watu wengi walikuwa hawawezi kupata habari kwa urahisi kama ilivyo hii ya leo. Miaka ya nyuma radio station ilikuwa moja tu na hata Tv stations hazikuwepo,pia radio stations za watu binafsi nyingi hazikuwepo,hivyo upatikanaji wa habari ulikuwa mgumu na hivyo ilikuwa rahisi kuwapotosha watu

Leo hii utampotosha nani? Karibu kila familia mijini na vijijini ina Tv set na kila mwanafamilia ana simu janja ambayo inauwezo wa kumpatia habari anayoyote anayoitaka. Kipindi hiki cha uchaguzi wananchi wanapata habari kwa urahisi sababu teknolojia imekuwa na hivyo kila hoja na sera za mgombea wananchi wanazipata.

Mgombea urais kwa Chadema, Tundu Lissu amekuwa akisikika kila mahala anapofanya kampeni zake kuwa rais aliyepo madarakani amefifisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi jirani na mataifa ya nje. Kisa tu huwa hafanyi safari za nje mara kwa mara. Hii hoja amekuwa akisisitiza mno kiasi kwamba watu wamekuwa wakimshangaa.

Ziara ya rais wa Burundi ndugu Evarist Ndaishiaye imemuumbua huyu ndugu Tundu Lissu,maana kama nchi haina mahusiano mazuri ya kidiplomasia na majirani au mataifa ya nje rais wa Burundi angekuja leo Tanzania kufanya ziara ya kikazi ambayo ina manufaa makubwa kwa taifa letu? Kama Tanzania ina mahusiano mabaya na majirani zake Burundi ingeweza kufanya makubaliano ya kuanzisha mchakato wa kujenga kinu cha kuchenjulia nickel kwa pamoja na Tanzania? Mbali na ziara ya rais wa Burundi ambae amefanya ziara leo,je ziara ya rais Museveni? Sio uhusiano mzuri wa kidiplomasia na majirani?
Leo bomba la mafuta litapita hapa Tanzania na taifa letu litanufaika kimapato.Biashara baina ya Burundi na Tanzania kwa sasa ni zaidi ya bil 201. Je wakianza kuuza dhahabu mkoani Kigoma kwenye soko la dhahabu itakuwaje?

Mimi binafsi naona ndugu Lissu hakujiandaa kugombea urais vizuri na itakuwa jambo la ajabu wakazi wa mkoa wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla kuchagua mtu ambae haoni mahusiano mazuri ya taifa letu na nchi za nje amabayo yanaliletea taifa letu manufaaa makubwa. Hii hoja potofu kuwa JPM amefanya mahusiano ya kimataifa kuwa mabaya ni sababu tosha kumnyima kura huyu mgombea maana ni muongo na mzandiki.
Wewe ndiyo muongo na mzandiki ni watanzania gani unawasemea?
 
Mh...! Mradi wa kabanga nickel ulishaaanza? Pale kuna mgodi? Kama biashara kati ya Tanzania na Burundi ni bil 200,unasema hakuna mchangi hapo?
Huna unachokijua zaidi ya kukariri zidumu fikra zisizo sahihi za mwenyekiti wa mtukufu wa CCM
 
Back
Top Bottom