Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ametoa kauli yake ya kwanza baada ya Mpinzani wake Freemn Mbowe kukubali matokeo hata kabla hawajafika ukumbini, kwa kutweet.
Lissu amesema wameweka a golden satndard, ambapo chama chochote nchini wameambiwa kama wanawaweza wafikie kiwango cha CHADEMA, wamefanya uchaguzi huru, wa wazi, wa haki na wa kidemokrasia ambao haukuwa na mizengwe. Kila mwenye haki ya kupiga kura na kura yake ilihesabika na kuhesabiwa. Uchaguzi ambao umefatiliwa ndani na nje ya nchi, na marafiki zao wa jumuiya ya kimataifa, asasi za kiraia, vyama vya siasa na serikali kupitia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.
Wamefanya uchaguzi uliokuwa wazi ambao haujawahi kutokea nchini na yote haya yamefanikiwa kama Mbowe alivyoahidi uchaguzi utakuwa na sasa wanaenda kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi.
Pia soma: Pre GE2025 - Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%
Lissu ameongeza kuwa Mbowe ametumikia kwa vipindi 4 ambavyo ni sawa na miaka 20, alipochukua chama kilikuwa na wabunge 5 na kukipeleka mpaka kuwa chama kikuu cha upinzani, kupata kambi upinzani bungeni kulichoongoza kwa miaka 10, aongeza kuwa Mbowe amekifanya chama kuwa kikubwa kuliko CCM sababu CCM si chama cha siasa, bali ni chama dola, amekifanya kuwa chama kikuu cha siasa
Asema historia ikiandikwa watatambua mchango wa Mbowe kwa kufanya siasa za vyama vingi kuwa viable kufikiwa.