Pre GE2025 Lissu aongea baada ya ushindi CHADEMA, asema Mbowe aliahidi uchaguzi wa huru na haki na ametenda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ametoa kauli yake ya kwanza baada ya Mpinzani wake Freemn Mbowe kukubali matokeo hata kabla hawajafika ukumbini, kwa kutweet.

Lissu amesema wameweka a golden satndard, ambapo chama chochote nchini wameambiwa kama wanawaweza wafikie kiwango cha CHADEMA, wamefanya uchaguzi huru, wa wazi, wa haki na wa kidemokrasia ambao haukuwa na mizengwe. Kila mwenye haki ya kupiga kura na kura yake ilihesabika na kuhesabiwa. Uchaguzi ambao umefatiliwa ndani na nje ya nchi, na marafiki zao wa jumuiya ya kimataifa, asasi za kiraia, vyama vya siasa na serikali kupitia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Your browser is not able to display this video.

Wamefanya uchaguzi uliokuwa wazi ambao haujawahi kutokea nchini na yote haya yamefanikiwa kama Mbowe alivyoahidi uchaguzi utakuwa na sasa wanaenda kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi.

Pia soma: Pre GE2025 - Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Lissu ameongeza kuwa Mbowe ametumikia kwa vipindi 4 ambavyo ni sawa na miaka 20, alipochukua chama kilikuwa na wabunge 5 na kukipeleka mpaka kuwa chama kikuu cha upinzani, kupata kambi upinzani bungeni kulichoongoza kwa miaka 10, aongeza kuwa Mbowe amekifanya chama kuwa kikubwa kuliko CCM sababu CCM si chama cha siasa, bali ni chama dola, amekifanya kuwa chama kikuu cha siasa

Asema historia ikiandikwa watatambua mchango wa Mbowe kwa kufanya siasa za vyama vingi kuwa viable kufikiwa.

Your browser is not able to display this video.

 
Hakuna ubishi kuwa Lissu ni msomi wa kiwango cha juu kabisa. Kutokana na majukumu mapya aliyopewa na wanachama wa CDM, anatakiwa awe kiongozi anaeamini katika;
1. Aache kutuhumu bila kuwepo kwa ushaidi.
2. Amwombe Mzee Mbowe Msamaha hadharani kwa kumwita mla rushwa.
 
Wacha uchochezi,uchaguzi umekwisha salama tofauti na nyie maccm mlivyopanga. Lissu hajawahi kumuita Mbowe mla rushwa,na hivi wewe Makupa unapata wapi moral authority ya kuyasema haya hivi kuna mtu alikuwa anamtukana Mbowe hadi matusi ya nguoni kuliko wewe? Wacheni hizo mlitegemea Chadema ipasuke na haikuwa hivyo.
 
Mkuu ,Lissu alikuwa ni kinara wa kusema chaguzi ndani ya cdm zilitawaliwa na rushwa ,je mkuu wa cdm alikuwa ni nani kwa wakati wa hizi tuhuma?
 
Wajumbe siyo watuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜†
Mziki wote ule alikodi, pamoja na viti na vinywaji
Ila wamemgeuka
 
Siku za nyuma watani wetu CCM hapa jukwaani walituchana ukweli kuwa CHADEMA ni mali ya Mbowe na familia yake, CHADEMA ni mali ya wachaga. Sisi kwa mapenzi ya chama tulipinga sana.
Kauli za Mh. Mbowe kipindi cha kuelekea uchaguzi uliomalizika leo alfajiri zilithibitisha kuwa CHADEMA kilikuwa chama chake binafsi. Hata baadhi ya viongozi na wadau kama akina Yericko Nyerere walimuunga mkono Mbowe kwakuwa walijua Mbowe yuko CHADEMA milele hivyo walijipendekeza ili wakumbukwe kwenye nafasi za ubunge.
Sasa CHADEMA ni mali ya Watanzania.
Kituo kinachofuata ni kuigeuza Tanzania kuwa mali ya Watanzania wote.
Ile Tanzania ya Rais anatembeza na mabulungutu ya pesa anagawa kila anakokwenda inakwenda kukomeshwa .
Watanzania wote watafaidi rasilimali za nchi yao.
Mimi ni miongoni mwa wachache ambao nanufaika na rasilimali za nchi hii ila si mbinafsi , natamani kilTaifa nzania afurahie rasilimali zetu .
Mambo ya kuchukua mamia ya wasanii kwenda nao Dodoma na kuwalipa pesa kizembe yanakwenda kuisha.
Lissu mdau mkubwa wa haki.
Haki uinua Taifa
 
Kwa hiyo asipofanya hivyo chama kinakufaje?
 
CDM inaenda kufa chini ya Uongozi wa Lissu na Heche.
 
Mbona mambo ya CHADEMA yanakutesa sana? Hata kama wakijiunga na CCM tatizo liko wapi?
 
Hauchoki wala haupoi gentleman πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…