Lissu apotosha mwananchi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Mpanda-Katavi

Lissu apotosha mwananchi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Mpanda-Katavi

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
305
Reaction score
728
Tundu Lissu ameishiwa sera ni bora akae kimya kuliko kuongea uongo na upotoshaji pindi anapoomba kura kwa wananchi katika kampeni zake.

Leo akiwa katika kampeni zake Makambako, Mkoani Iringa amewaeeleza wananchi kuwa uwanja wa ndege wa Mpanda kwa sasa haufanyi kazi kwamba ulijengwa kwasababu Mizengo Pinda alikuwa Waziri Mkuu kuwa Sasa sio Waziri Mkuu anaishi Zuzu Dodoma, Uwanja wa Ndege wa Mpanda watu wanalishia Mbuzi na Ng'ombe, jambo ambalo siyo kweli.

Ukweli ni kwamba mpaka sasa ndege za Air Tanzania zinafanya safari za kwenda mpanda, ushahidi huo hapo chini, unaoonesha kuwa kesho Tarehe 15/09/2020
Air Tanzania inaenda MPANDA na SEATS zimebaki 5 tu, hata Lissu anaweza kuziwahi kama unataka kwenda.

1600098980567.png

Watanzania tuwe makini na huyu Lissu kwa maneno anayoyatoa kwenye kampeni zake katika maeneo yenu, tuyatafakari na kuyatahimini kwani mtu ambaye analopoka mambo ambayo hayajui kiundani. NI MUONGO MPOTOSHAJI, HANA SERA.

Tuendelee kuunga mkono Rais Magufuli ili tuendelee kupata maendeleo
 
Uwanja wa ndege wa mpanda unaweza kutua ndege moja kwa wiki tena kwa msimu. Gharama zilizotumika kuujenga na kuuendesha ni kubwa kuliko uhalisia wa matumizi yake. Ulijengwa kwa msukumo wa Pinda wakati Pinda akiwa waziri mkuu, wakati huo mpanda ni wilaya katika mkoa wa Rukwa.

Nawaza tu hawa mawaziri wakuu kama Malecella (Mtera), Cleopa Msuya (Mwanga), Sumaye (Hanang), Sokoine na Lowassa (Monduli) hivi nao wangukuwa wabinafsi na washamba wa ndege, hivi wasingeweza kujenga viwanja vya ndege kule walikotokea?
 
Tundu Lissu kama ameishiwa sera ni bora akie kimya kuliko kuongea uongo na upotoshaji pindi anapoomba kura kwa wananchi katika kampeni zake...

Mfumo kuonyesha kuwa siti tatu zimebaki haina maana kuwa kweli siti tatu zimebaki, ujanja huu hufanyika sana hata kwa makampuni ya nje ili kutamanisha abiria kukata tiketi. Nenda pale ofisini kwo utakuta ndege iko wazi zaidi ya asilimia 80
 
Mwisho wa siku mnaodhani wengine tunabeza tunaposema apatiwe psychological help jipeni muda tu na nyie mtafikia hitimisho hilo hilo.

Tundu Lissu hayupo sawa kichwani baada ya uchaguzi ndio ili swala litakuwa dhahiri. We unadhani kwanini viongozi wajuu wa CDM hawana shughuli nae.
 
Tundu ametumwa na wahuni huko nje kuja kupinga maendeleo ambayo sisi watanzania tumejitafutia .

Atajuta kugombea irais
Acheni kuropoka! Maendwleo ni kujenga uwanja wa Ndege wa kimataifa nyumbani kwake?

Umewahi kuwaza endapo hizi hela alizotumia kuujenga huo uwanja usio na faida angeweza kujenga shule ngapi za kisaaa?
 
Kama unaamini ulichokiona kwenye hiyo booking website, wapigie simu na kuwaambia "....sasa itakuwaje wakati mpo watu 12 na inaonesha zimebaki siti 2 peke yake" kisha leta mrejesho hapa!!

Hivi hao ATCL si ndo walituambia eti wanatengeneza faida lakini kinyume chake hadi kesho pesa za kununua ndege zingine zinatoka Hazina?
 
Uwanja wa ndege wa mpanda unaweza kutua ndege moja kwa wiki tena kwa msimu. Gharama zilizotumika kuujenga na kuuendesha ni kubwa kuliko uhalisia wa matumizi yake. Ulijengwa kwa msukumo wa Pinda wakati Pinda akiwa waziri mkuu, wakati huo mpanda ni wilaya katika mkoa wa Rukwa.

Nawaza tu hawa mawaziri wakuu kama Malecella (Mtera), Cleopa Msuya (Mwanga), Sumaye (Hanang), Sokoine na Lowassa (Monduli) hivi nao wangukuwa wabinafsi na washamba wa ndege, hivi wasingeweza kujenga viwanja vya ndege kule walikotokea?
Mkoa mmoja viwanja vya ndege viwili wakati ule wa Msoma kwa baba wa taifa ni uwanja wa vumbi(hauna rami). Kama angefanya upanuzi wa uwanja wa Sumbawanga au kuuboresha, angalau ingeeleweka kidogo na si kujenga uwanja huu wa Mpanda. Mtu mwerevu anaelewa kuwa ni ubinafsi wetu sisi binadamu wa kujipendelea kwetu pasipo kuangalia maslahi ya umma.
 
Tundu Lissu kama ameishiwa sera ni bora akie kimya kuliko kuongea uongo na upotoshaji pindi anapoomba kura kwa wananchi katika kampeni zake.

Leo akiwa katika kampeni zake Makambako amewaeeleza wananchi kuwa uwanja wa ndege wa Mpanda kwa sasa haufanyi kazi kwamba ulijengwa kwasababu Mizengo Pinda alikuwa Waziri Mkuu kuwa Sasa sio Waziri Mkuu anaishi Zuzu Dodoma, Uwanja wa Ndege wa Mpanda watu wanalishia Mbuzi na Ng'ombe, jambo ambalo siyo kweli.

Ukweli ni kwamba mpaka sasa ndege za Air Tanzania zinafanya safari za kwenda mpanda, ushahidi huo hapo chini, unaoonesha kuwa kesho Tarehe 15/09/2020
Air Tanzania inaenda MPANDA na SEATS zimebaki 5 tu, hata Lissu anaweza kuziwahi kama unataka kwenda.

View attachment 1569840

Watanzania tuwe makini na huyu Lissu na maneno anayoyatoa kwenye kampeni zake katika maeneo yenu, tuyatafakari na kuyatahimini kwani mtu ambaye analopoka mambo amabayo hayajui kiundani. NI MUONGO MPOTOSHAJI, HANA SERA.

Tuendelee kuunga mkono Rais Magufuli ili tuendelee kupata maendeleo
Nilidhani imeshaenda..!!! Kumbe itaenda kesho..!! Haya toka leo na kurudi nyuma unaweza ukaleta safari yoyote iliyokwishafanyika..!?? Kama kaongea leo basi yupo sahihi... maana anayasema yaliyokwishatomea na si ya kesho
 
Air Tanzania ya kwenda mpanda ni Mara ngapi kwa mwezi?
Je kuna economic potential yeyote ya kuweka airport?
SASA tunapoelekea watanzania mtaanza kuhojiwa kwanini mnajenga nyumba ya vyumba vitatu wakati unatumia chumba kimoja tuu...vitu kujengwa sio tatizo, la msingi tuendelee kuwasapoti watu tuliowapa dhamana waendelee kufanya Mambo mengi makubwa instead of demoralising them.. sidhani kama ni Sawa.. actually sioni tatizo kila Mkoa ukiwa na kiwanja cha ndege kizuri.
 
Mbona nyie mnatwambia tupo uchumi wa Kati Hali watz dhoofu Hali wengi hata chai awaijui waliacha kunywa miaka,wanashindia mihogo tu mlo mmoja sababu ya sera zenu mbovu za kuwasomesha watz namba ili wawe wanyonge kusudi wakuabuduni.
 
Air Tanzania ya kwenda mpanda ni Mara ngapi kwa mwezi?
Je kuna economic potential yeyote ya kuweka airport?

What do you mean by saying there is no economic potential in Katavi? Do we take time to research on the issues we comment?

Helium gas, copper, coal, and other food stuff we eat, come from Katavi. And yet, because we want to hear what we would like listening, we dare make such an informed comment
Wanasiasa wanatujulia sana sababu process nzima ya kufikiria kama individuals, mayor tumeibinafsha kwao. Poor us!
 
SASA tunapoelekea watanzania mtaanza kuhojiwa kwanini mnajenga nyumba ya vyumba vitatu wakati unatumia chumba kimoja tuu...vitu kujengwa sio tatizo, la msingi tuendelee kuwasapoti watu tuliowapa dhamana waendelee kufanya Mambo mengi makubwa instead of demoralising them.. sidhani kama ni Sawa.. actually sioni tatizo kila Mkoa ukiwa na kiwanja cha ndege kizuri.

Picha Ni kwamba vipaumbele vya watawala sio vipaumbele vya wananchi, watawala wasikilize wananchi wanataka nini Kisha ndo wawapelekee na sio wao kuwapelekea kile kisicho na ulazima kwao
 
Back
Top Bottom