Habari Wakuu!
Nimekutana na picha ya habari toka Voice of Amerika Swahili (VoA Swahili) ikidai kuwa Tundu Lissu amethibitisha kupokea vitisho kutokea kwa Freeman Mbowe.
Je ni kweli? Picha hii hapa Chini
Nimekutana na picha ya habari toka Voice of Amerika Swahili (VoA Swahili) ikidai kuwa Tundu Lissu amethibitisha kupokea vitisho kutokea kwa Freeman Mbowe.
Je ni kweli? Picha hii hapa Chini
- Tunachokijua
- Freeman Mbowe ni Mwenyekiti wa CHADEMA huku Tundu Antipas Lissu akiwa ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024 na Uchaguzi Mkuu mwakani, chama hicho kumekuwa kikijipanga kwa kufanya chaguzi za ndani kwa nafasi za Uongozi katika Nyanda mbalimbali.
Tangu kuanza kwa Uchaguzi wa ndani wa Chama hicho kumekuwa na hoja katika mitandao mbalimbali zikidai kuna mgawanyiko na kutoelewana kati ya Tundu Lissu na Mbowe soma hapa, hapa na hapa.
Tangu tarehe Juni 5, 2024 kumeibuka picha (hiyo hapo juu) kwenye mitandao huu na huu ikionekana imetokea katika ukurasa wa Shirika la Habari la Marekani Voice of Amerika ya Kiswahili (VoA) ikionesha maadishi yanayodai Lissu anasema Mbowe ametoshia Maisha yake.
Upi ukweli wa jambo hili?
JamiiCheck imefuatilia jambo hili na kubaini kuwa picha na taarifa hiyo si ya kweli. Katika kupata uhakika wa taarifa hiyo JamiiCheck imetafuta kwenye kurasa zote rasmi za VoA Swahili na haikukutana na taarifa hiyo kumhusu Tundu Lissu.
Zaidi ya hayo, JamiiCheck imefanya mawasiliano na Muwakililishi wa VoA Tanzania ambaye amekanusha VoA kuhusika na picha hiyo. Mwakilishi huyo anaongeza kuwa, VoA hawajafanya mahojiano na Tundu Lissu hivi karibuni na picha hiyo inayozunguka mitandaoni sio Yao imetengenezwa.
Mwakilishi huyo anasema:
Niliwapatia Ofisini kuwauliza Wakuu, walisea hatujafanya mahojiano yoyote na Lissu na wala hawajapost taarifa ya namna hiyo popote. Nadhani watu watakuwa wametengeneza tu. Na hatujaongea chochote kuhusu taarifa hiyo.
Hivyo, kutokana na ufuatiliaji wa vyanzo hivyo JamiiCheck imejiridhisha kuwa picha na habari iliyoambana nayo ni ya kizushi.