Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
Kwanza nitangaze Mgongano wa Maslahi kwamba mimi pia ni Shabiki wa Lissu, naheshimu mchango wake katika kupigania mabadiliko ya nchi hii na natambua na kuheshimu gharama alizolipa kwa kwa kazi hiyo kwa ajili ya Taifa hili.
Ila siku za Karibuni ameanza kufanya Siasa fulani hivi za kutuhumu Viongozi wake hadharani masuala ya Rushwa bila ushahidi wa moja kwa moja jambo ambalo nadhani kisiasa lilipaswa kushughulikiwa katika Vikao vya ndani vya Chama.Ninajua Lissu anafahamu kuwa maneno yake yanaharibu taswira ya Viongozi wenzake na Chama chake ingawa yanamjenga yeye Binafsi.
Ninafahamu CCM kwa muda mrefu wanafanya jitihada za kumuondoa Mbowe bila mafanikio na ni kwasababu wanajua Nguvu ya Mbowe katika Uimara wa CHADEMA, na inaeleweka Propaganda nyingi wanaanzisha wao ikiwemo ya kuwagonganisha Lissu na Mbowe kutengeneza Mpasuko na kuisambaratisha CHADEMA.
Tukumbushane CCM imechokwa CHADEMA haijipangi ila tunahitaji Upinzani imara,kuanguka kwa CHADEMA ni hasara kwetu wote siyo kwa Lissu na Mbowe tu kwasababu ndiyo Voice ya Voiceless pekee iliyobaki.
Naomba walioko Karibu na Lissu wamshauri atumie Vikao vya ndani kuepuka kuimarisha Propaganda za CCM na kukidhoofisha Chama chake.
Yanga Bingwa.