Pre GE2025 Lissu ashauriwe apunguze kutuhumu wenzie bila Ushahidi, anagharimu Chama chake kwa kucheza ngoma ya CCM bila kujijua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu anataka kupimana nguvu na Freeman Mbowe, ajue tu sumu haijaribiwi kwa kulambwa
 
Watanzania huwa mnataka msemu kweli au mnataka mnafiki. Mnataka chama ambacho ni tofauti na ccm ambacho viongozi hawavumilii uovu au mnataka tu mbadara wa CCM.
Kuna muda huwa siwaelewi watanzania mnataka mabadiliko kweli au tu chama kingine ikulu haijalishi ni kama ccm au worse than ccm.
 
Si kosa kuwa na mawazo mbadala ndani ya chama, sidhani CDM inaogopa hoja hapana, itapokea na kuzifanyia kazi kama kweli kuna pesa zimetoka nje kujaribu kuvuruga chaguzi basi zitakuwa addresed katika vikao husika na riport tutapewa.

Otherwise CDM is safe - chama kinachoogopa wanachama wake ku rise issues za ndani nje - hicho ni chama mfu.

CDM wanachama wake wapo huru kutoa maoni yao juu ya threat yoyote inayokinyatia chama hii ndiyo afya.
 
KUNA MABO UKIYASEMA HADHARANI UNAJIUA MWENYEWE. SASA AKISEMA CHADEMA KUNA RUSHWA HADHARANI ANAKUWA AMEKIJENGA CHAMA AU AMEKIUA? UNAKEMEA RUSHWA NDANI KWENYE VIKAO VYENU. MTU AKIKAIDI NA KULA RUSHWA MNAMFUKUZA, TOKA KABISA. THEN HAPO MNAWEZA KUTOKA HADHARANI NA KUSEMA FULANI AMEFUKUZWA CHAMA KWA VILE AMEKULA/AMEONESHA VITENDO VYA RUSHWA. THAT IS ACCEPTABLE IN ALL SPHERES!
 
Kasema ukweli mimi kama mwananchi nafurahi maana sitaki chama ambacho kitakuja kugeuka kuwa kama ccm. Tunataka chama ambacho viongozi sio wanafiki nyeupe wanaisema ni nyeupe na nyeusi wanaisema kuwa ni nyeusi.
Sasa inanishangaza kuona mwananchi anachukia hilo ndio maana najiuliza, watanzania mantaka mabadiliko kweli au mabadiliko tu ya chama cha siasa.
 
Uko sahihi.kusema ofisi ina matatizo nawewe ni sehemu ya uongozi unayepaswa kuyashughulikia ila ufanyi hivyo alafu unaenda kuyaongea uko nje huo ni ujinga pro max.Uongozi maana yake nikushughulika na changamoto za ofisi yako sio kuzitaja tu hadharani bila kuzitatua.Lissu anatakiwa ajue wajibu wa kiongozi ni kuchukua hatua sio kulalamika kwa maneno na akiona anashindwa maana yake hautoshi kwenye hiyo nafasi.
 
Tanzania tuna viongozi wachache sana aina ya Lissu, hiki unachoshauri ndio siasa za CCM miaka yote kulindana...huwezi kumshinda adui kama utawaza na kufanya kama yeye.

Maneno ya lisu ni dawa ila sema ni chungu mno...

Acha tuendelee kuamini bila Mbowe hakuna Chadema
 
Umenena vyema.. alafunaona shida kwa lissu kujiona yy perfect kuliko yoyote.
Ajifunze busara kwa mbowe.
Out of that hana tofauti na magufuli tunaemshutumu daily
Ila mkuu inawezekana vipi wabunge wanaapishwa bila baraka za chama chao ,jambo la ajabu kuna wake wa viongozi wakubwa wa chama halafu wanasema walikua hawajui..

Lissu anaweza kua ametumia approach mbaya kwa mtazamo wa watu wenye siasa za unafki lakini ,mimi naona amefanya jambo zuri ukizingatia siasa za CHADEMA chama kinachotegemea kwa mabadiliko nacho kimekua cha nusu mkate kama chama kile cha dhambarau.
 
 
Anajua anachofanya na anafikiri aweza kuwa maarufu popote.
 
Lisu ameamua kumwaga ugali
 
Bnafsi namuona lissu akileta mpasuko na akikimbilia dhambarau next election.
Kuna vikao anafanya mzee wa mwandiga akiwajilisha jumba jeupe
 
Tuwe wakweli tu, tatizo ni Mbowe, kwa mazingira yalivyo unaweza kuweka kikao cha kumjadili mwenyekiti kula rushwa? Inawezekana njia ya Lisu kuweka ukweli hadharani sio nzuri, lakini ndio njia pekee. Mbowe akubali tu wakati ukuta, apishe wengine kwa sasa.
 
Bnafsi namuona lissu akileta mpasuko na akikimbilia dhambarau next election.
Kuna vikao anafanya mzee wa mwandiga akiwajilisha jumba jeupe
Ni sawa tu, kama Mbowe ataendelea kulazimisha kuwa mwenyekiti, huku akiwa anakula hela za Samia ni bora iwe hivyo.
 
Mimi nataka mtu muwazi na mkweli kama Lissu.
Chadema wanafikiri kulindana kutastawisha chama kumbe wanakiua.

Benson aliyeropoka leo ni chawa wa Mbowe tu.

Lissu najua amepasua jipu sio bure bali ana shabaha yake mahsusi
 
Ni sawa tu, kama Mbowe ataendelea kulazimisha kuwa mwenyekiti, huku akiwa anakula hela za Samia ni bora iwe hivyo.
Chadema ikiendelea kuboronga ina tofauti gani na ccm?

Mbowe hataki kabisa kuacha siasa biashara tena kwa akili sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…