Ashampoo burning
JF-Expert Member
- May 12, 2023
- 593
- 2,219
Unajua Lissu anajitia hajui kuwa hali iko hivi, Rais Samia 2025 hataki kabisa upinzani mkali, sasa Lissu yeye anakomaa. Mambo tayari yako mezani pale Mbeya, wataka jimbo Sugu apate na Tulia apate.
Ukija Arusha wataka jimbo pia Lema apate alipe madeni yake na Gambo apate. Kule iringa Msigwa nae watamuonea tu huruma.
Sasa Lissu yeye anajifanya kichwa ngumu ndio maana wenzie wataanza kumpiga nyundo, maana wamechoka kukaa mitaani.
Lissu yeye anataka Katiba ndio mambo mengine yafuate, wakati wenzie wako tayari kwa lolote warudi Bungeni.
Mfano Sugu hela ya kujenga hotel angepata wapi kama sio Ubunge? Sasa sasa hivi kashaaambiwa njia nyeupe utarudi, hujimsikia akipiga kelele.
Lissu bora tu ukae kimya unaingiza nzi kwenye togwa, kina Lema watakupiga makofi. 😀😀😀😀
Lissu hela anayo ndio maana ana misimamo.