Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Chadema na Wakili wa Dkt. Wilbroad Slaa, Tundu Lissu amesikitishwa kushikiliwa kwa muda mrefu mteja wake huyo ambaye ana umri wa miaka 76 bila kupewa dhamana huku akieleza kuwa ni uonevu.
"Hivi inawezekanaje kwa serikali hii, na mapolisi wake na waendesha mashtaka wake kumweka ndani muda wote huu mzee wa miaka 76, mzee Slaa alivyo tu ni tishio kiasi gani? Kama sio kukandamiza watu bure. Hivi ndio vitu ambavyo tunatakiwa tuvipige vita, tutengeneze nchi mpya, tupate sheria mpya, Katiba mpya itakayohakikisha kwamba mambo haya ya uonevu wa aina hii hayatokei tena kwa Wananchi wetu"
Soma, Pia: Mahakama Kuu yaagiza dhamana ya Dkt. Slaa ishughulikiwe haraka