Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Akiwa Mgeni wa Heshima katika sherehe za Bawacha jana, Lissu hakuweza kujizuia kumtaja Aida. Alirudia tena madai yake kuwa Aida alipewa ubunge na CCM. Huo ni upotoshaji mkubwa kwa sababu una maanisha kuwa Aida hakushinda uchaguzi bali CCM walifanya figisu figisu na kumpa kura za ushindi.
Anashindwa kukubali kuwa Aida alishinda kihalali na akatangazwa. Swali analoweza kuuliza ni kwa nini CCM walimtangaza yeye tu? Inawezekana Aida alijipanga vizuri yeye na wapiga kura wake kiasi cha CCM kushindwa kudhulumu.
Inawezekana CCM waliisha mchoka mshindani wake na kuona bora aondoke. Na Inawezekana msimamizi wa uchaguzi katika eneo lake alikuwa mtenda haki na nafsi yake ilimzuia kufanya dhulma. Badala ya kulirudia rudia, yeye na wenzake wangekaa nae na kumuomba awaeleze alifanikiwa vipi. Huyu dada ni mpiganaji na ni mfano wa kuigwa.
Lissu pia alisema kuwa huo msimamo wake haukueleweka vizuri ndio maana watu wakamrushia madongo. Alisema haukuwa personal bali ukweli unabidi kusemwa. Hapo tena amejaribu kujikosha. Watu walimrushia madongo kwa kikubwa kutokana na yeye kudai kuwa Aida hachangii lolote. Hilo ndio liliwakera watu maana mchango wa Aida wote tuna uona. Na wenzake wanaouona ndio maana wakampa ngao.
Lissu anapaswa kukiri kuwa alikosea na amuombe radhi.
Amandla...