- Source #1
- View Source #1
======
wakuu
Ni kweli kwamba Tundu Lissu amewaita mawakili wake wasaliti?
wakuu
Ni kweli kwamba Tundu Lissu amewaita mawakili wake wasaliti?
- Tunachokijua
- Tundu Lissu ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambaye anakabiliwa na makosa ya uhaini na uchochezi. Juni 16, 2025 Kesi yake ya uhaini iliitwa tena na kusikilizwa ambapo mtuhumiwa aliomba kujitetea mwenyewe. Kesi hiyo imehairishwa tena hadi Julai 1, 2025.
Madai
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Facebook amesambaza grafiki yenye nembo ya Millard Ayo huku ikiwa na picha ya Tundu Lissu akiwa mahakamani pamoja na ujumbe unaosomeka kuwa
“LISSU HANA IMANI NA MAWKILI WAKE, AWAITA WASALITI”
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa inapotosha uhalisia. Katika kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu iliyoendele Juni 16, 2025 mtuhumiwa aliaiimbia mahakama atajitetea mwenyewe kutoka na sababu mbalimbali alizozitaja ikiwemo kukosa faragha ya kuzungumza na mawakili wake.
Ufuatiliaji umebaini kuwa wakati akizungumza mahakamani hapo Lissu hakusema kuwa hana imani na mawakili wake na kuwaita wasaliti na badala yake wakati akiwasilisha hoja hiyo alisema kuwa;
“Nina mawakili zaidi ya 30, na mawakili hao mheshimiwa hakimu niliwachagua mimi mwenyewe. Ni mawakili wangu, na niliwachagua kwa sababu nina imani, nina full confidence na uwezo wao wa kuniwakilisha katika mashauri hay, katika kesi hii. Wengi wao nimefanya nao kazi.”
Ufuatiliaji pia umebaini grafiki inayotumika kusambaza taarifa hiyo haijachapishwa na chanzo hiko cha habari kama inavyoonekana. Grafiki hiyo pia ina baadhi ya makosa mathalani tarehe imeandikwa ‘Juni’ wakati Millard Ayo katika grafiki zake halisi anatumia ‘June’