Pre GE2025 Lissu: Hatuhitaji tena ubunge wa viti maalumu, sio suala la ukomo tena, wanawake sasa wana uwezo

Pre GE2025 Lissu: Hatuhitaji tena ubunge wa viti maalumu, sio suala la ukomo tena, wanawake sasa wana uwezo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Tundu Lissu pamoja na kupendekeza ukomo wa viongozi katika chama cha CHADEMA amependekeza suala la ukomo wa ubunge na udiwani, Viti maalum CHADEMA.

Lissu anasema ubunge wa viti maalum ilikuwa kuwajengea uwezo wanawake wa kushiriki katika siasa lakini kwa ubovu wa katiba yetu haikuweka ukomo katika ubunge wa viti maalum na kupoteza maana nzima ya jambo hilo.

Ubunge wa viti maalum ulikuwa kuwajengea wanawake uwezo wa kushiriki katika uongozi wa maamuzi, wakati huu tuna Rais, Spika, na viongozi wengine wengi wanawake, ni wakti sasa wa kudai sualla la ubunge na udiwani wa viti maalum kuondolewa kabisa katika katiba ya nchi.

Ubunge na udiwani wa kuteuliwa hauna tena uhitaji au mashiko katika Tanzania ya leo, kuwepo kwake ni kuongeza gharama tu zisizo za msingi kwa matumizi ya kodi za raia.
 
Hata ubunge wa kuteuliwa na Rais na wenyewe ni 🚮 tu. Futilia mbali huko! Vyeo vya wakuu w Mikoa, Wilaya, nk! Na vyenyewe ni 🚮 tu! Futilia mbali huko ili kuokoa kodi zetu.
 
Back
Top Bottom