Tetesi: Lissu karibu CCM Upumzike

Akija anapewa na Cheo ambacho sio Cha Kisiasa kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali 🤣🤣🤣🤣
 
Mfumo umefaulu kuwavuruga Chadema, hawana ujanja. Wakae chini wafanye reform kubwa pengine baada ya uchaguzi. Kwa sasa waelekeze nguvu kwenye uchaguzi,wasitolewe kwenye focus. Kama wana taka kuendelea kuwepo. Udhaifu wao umekwisha fahamika,Pesa!

..udhaifu wa Chadema ni pesa.

..majigambo na nguvu ya Ccm ni pesa.
 
Lissu akiishaingia CCM anapewa u-DC wa Mafia huko anatulia zake!
 
Sikubaliani na Mbowe kabisa kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm, lakini hakuna namna nitaendelea kumuunga mkono Lisu akihamia ccm. Hata hivyo huyo Lisu huko ccm iwapo ni kweli atahamia, sio kufuata siasa, bali atakuwa kafuata mlo.
 
nani wa kumpigia kura mbowe hehehe nakumbuka mambo ya 2005 tatizo tamaa tamaa tamaa
 
Acha upoyoyo. Elewa maneno ya Lissu Yana msingi mmoja.
 
Waliompiga risasi Lissu ni akina nani?
Waliotoa camera kwenye makazi ya viongozi ni akina nani?
Ina maana wewe mtoa mada una akili nyingi kuliko wana CCM wenzako wote?
Acha hizo hata kama una njaa sio kwa kuandika mashudu kiasi hiki.
Umemuuliza swali zuri sana.

Hivi mtu aliyeponea chupuchupu kuuawa na hao watesi wake, ndiyo aweze kushawishika ajiunge nao??😚
 
Umemuuliza swali zuri sana.

Hivi mtu aliyeponea chupuchupu kuuawa na hao watesi wake, ndiyo aweze kushawishika ajiunge nao??😚
Kwenye Siasa hakuna Úadui wa kudumu Wala Urafiki wa Kudumu
 
Duuuh
 
Mnataka mumpe pumziko Kama la Makonda sio ?
 
vile vikazi vidogo alivyo ahidiwa safari hii atavikubali?
 
Kwa bandiko lako hili unamaanisha viongozi wako wa CCM na Serikali ni wapumbavu kiasi Mbowe anawatekenya kisha wanamwagia mamilioni? Basi CCM ina viongozi wa hovyo kwa kuingizwa mkenge na Mbowekisha wanampa mamilioni ya kodi zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…