Lissu: Kikosi Kazi alichounda Rais kimem ‘expose’ Zitto yuko upande gani

dada hapa kuna pande 2 tu. wanaotaka Katiba na wasiotaka. zingine zoote ni means tu. Watu kama nyinyi ndo huwa mnakuja maelezo meengi ya kinafiki kama kinyonga
Achana na huyo hajui analosema. Madhali kiongozi anasimamia ukweli na haki basi huyo huyo ndiye tutakayempa sapoti. Akibadilika wala tusikate tamaa.

Watanzania tu wavivu kusoma ndiyo maana tunakata tamaa mapema au tunavunjika moyo kiongozi anapogeuka na kuwa upande wa CCM. Ukisoma historia za ukombozi duniani kote watu wanaoishia njiani au kubadilika na kuamua kushikamana na wakandamizaji ni wengi. Hata hapa tulipo bado wengi wataishia njiani. Lakini hili lisitukatishe tamaa.

Zitto mimi namfananisha na kiongozi mmoja alikuwa anaitwa Ndabaningi Sithole wa Zimbabwe. Wamefanana sana kitabia. Halafu Zitto ana wivu sana na hataki mtu mwingine au chama kingine kiwe na umaarufu kuliko yeye.

Baada ya kuhangaika na ATC Wazalendo kwa muda mrefu na kukosa waungaji mkono ameona ni bora ajipendekeze kwani hana cha kupoteza. Alidhani kujenga chama ni mchezo.

Ndiyo maana 2020 mgombea wao wa urais bwana Membe alikuwa anahutubia watu watatu tena huko kwao.
 
dada hapa kuna pande 2 tu. wanaotaka Katiba na wasiotaka. zingine zoote ni means tu. Watu kama nyinyi ndo huwa mnakuja maelezo meengi ya kinafiki kama kinyonga
Sidhani kama kuna mtanzania asiyetaka mabadiliko ya katiba ikiwa yana manufaa kwao.

Kutumia nguvu nyingi kuidai, ndio hasa kunatia shaka juu ya kusudi la hao wanaodai!

Na ndio maana maswali yanakuwa mengi na majibu yenye utata; kama katiba mpya ndio suluhusho la changamoto za kimaisha zinazowakabili watanzani walio wengi?

Kwahiyo, viongozi wanaona ni bora kushughulika na maendeleo ya taifa kwanza kisha kama kuna umuhimu wa mabadiliko, bila shaka yatafanyika tu.

Lakini je, hii iliyopo inazingatiwa kwa usahihi? Tuna uhakika gani kama hiyo mpya itazingatiwa ipasavyo?

Mi nadhani watanzania wanahitaji zaidi ukombozi wa kifikra kuliko hata katiba mpya!
 
Kikwete anamtambua na kummudu vyema Zito. Anaweza kumtumia jinsi atakavyo kwa kuwa anautambua udhaifu wake pale dau la fedha ama imani ya dini yake ikiwekwa mbele yake kama kivutio kwake.
Niamini kaka , mtu huwa haruki kati ya mitego ifuatavyo:

Ukabila
Udini
Ukanda

Yaani usipokuwa mdini basi utakuwa mkabila ila ukikosa vyote huwezi kuruka kwenye ukanda
 
Hizo longo longo ndio hatuzitaki sasa. Katiba ni sasa,mchakato wa katiba unazuiaje maendeleo. Huyo Samia alikuwa mjumbe wa katiba ya Kikwete,je mchakato ulizuiaje maendeleo?

Naona unapita mlemle kwenye mistari ya Samia mkijidanganya watu wanahitaji kwanza elimu ya uraia. Niwaulize mlianzaje katiba ya warioba watu wakiwa hawana uelewa?

Msitumie hiyo kama kichaka. Elimu ya uraia itaendelea kutolewa mpaka mwisho wa dunia
 
Umeongea vema sana, na huo ndiyo ukweli.

Kiukweli mi napata mashaka sana na mashambulizi haya kwa zitto kila siku. Tena huwa yanatoka upande wa chadema tu......kuna jambo hapa, si bure. na kwakuwa ndugu zangu hawa ni wa kufuata tu kila litokalo kwa lema au lissu basi ndo hivyo, tutashuhudia matusi mengi sana kwa zitto.

Ninachomsifu zitto ni msimamo na akili kubwa ya kuzikwepa shari za wazi dhidi yake binafsi na chama chake kutoka kwa chadema na wafuasi wake.

Tumeshuhudia mamia ya viongozi wa cdm wakihamia ccm na sasa ni viongozi kabisa wa serikali lakini husikii matusi yoyote kwao,......ila zitto kila uchwao ni kumzushia na kumtukana tu.

Zitto ni akili kubwa kwa wajingawajinga na wenye mihemko ya kilofa km lema na lissu au wafuasi wao walio km mazuzu. Akili pekee niiyonayo chadema kwa sasa ni mbowe tu. Yule jamaa yuko smart kichwani na humsikii akimzungumzia zitto au chama chake kizembezembe.....anajua yule usmart wa zitto na hataki kujichanganya.

Zitto ni nadra kumsikia akiitaja chadema au watu wake, ye yupo na yake tu.

Chama naona kimeishiwa sera na sasa kinatapatapa tu. Kumsakama zitto hakuwezi kukiinua, bali ukweli na mipango thabiti.
 
Kikwete anamtambua na kummudu vyema Zito. Anaweza kumtumia jinsi atakavyo kwa kuwa anautambua udhaifu wake pale dau la fedha ama imani ya dini yake ikiwekwa mbele yake kama kivutio kwake.
Haswa!
Jamaa ni mdini sana lakini aliemuweka kwenye ramani ni mkristu Mbowe
 
Imenilazimu nitoke Kihesa kuja Mwangata nilogin JF ili nicheke vizuri hii post🤣
Usiishie hapo mwangata shuka Hadi mwelewele na ikikupendeza maliza mpaka hoho ukale mapera machanga ili yakupalie unapocheka! Hawajambo wanyalu?
 
Kimsingi Kikosi kazi hicho ni Mali ya mwenyekiti wa ccm
 
Zitto ni mnafiki na mchumia tumbo kama Wewe tu.

Hana u smart wowote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…