Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 984
- 1,179
Mh. Lissu wewe mwenyewe unaelewa kuwa ukiwa mwenyekiti wa chama inakunyima nafasi ya kuwa mgombea nafasi ya Urais. Wafuasi wengi hawaelewi hilo. Ombi langu kwako, badili upepo wa kisiasa ndani ya chama na nje.
Mkakati uwe ni kufanya mambo ya ustawi zaidi za jamii. Watanzania ni werevu sana na kwa hali ya sasa wamekata tamaa ni uchaguzi.
Tunaweza irejesha hali hiyo nawe ukiwa dereva. Kwa kuwaonyesha watanzania vipaumbele vyako ni mini ukiwa Rais. Kwa maana vipaumbele vyako katika matumizi ya kodi ni kugawa pesa katika mambo ya anasa au zitakwenda kuboresha huduma za kijamii kama Afya.
Pia soma: Mimi binafsi, siwezi kumsikiliza rais Samia
Hivyo ushauri wangu kwako, Badili upepo wa kisiasa.
Tembelea maeneo au taasisi tunazotoa huduma za kijamii na kwa kuanzia Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kuwa na taratibu za kuwatembelea wagonjwa. Anza na wodi ya magonjwa ya saratani. Pitia vitanda kadhaa na uwahoji kupatikana wa huduma. Kutaja wa ndugu za wagonjwa. Tembelea idara ya Ustawi wa jamii. Waulize ni wagonjwa gani wanastahili kupata msamaha. Na kwanini hawapati hata baada ya kuhitimiza taratibu.
Kuwa mfariji wa Watanzania, weka program maalum ya kuhamasisha watanzania kuchangia damu. Kuna kundi kubwa litakuelewa na kukufata yakiwemo viongozi wa dini vijana Tanzania nzima. Nakupa ushauri huu kwa kuwa mfariji mkuu si katika vipaumbele vyake.
Onyesha utofauti. Wakati yeye kipaumbele chake ni matumizi ya anasa kwa serikali yake, wewe jikite katika kuhamasisha na kuboreswa huduma za kijamii.
Kuna bibi ambaye pamoja na madaktari kumruhusu arudi nyumbani, lakini waliendelea kuzuiliwa wodini kwa kuwa alikuwa anadaiwa. Fikiria Lissu, senior citizen kama huyu ambaye katika umri wake wote alikuwa ni mlipa kodi katika mfariji mkuu amemzuia na kumdai.
Mh Lissu hawa ndio wanaohitaji faraja kutoka kwako na watanzania watakuunga mkono kama kweli lengo lako ni kubeba dhima ya kuinua ustawi wa jamii.
Shukria.