Tetesi: Lissu kuhama CHADEMA muda wowote kuanzia sasa

Kwa tangazo hili umeingiza maokoto kiasi gani kwenye akaunti yako.
Hata akihama bado atakuwa anawatumikia watanzania wasiowapenda viongozi wezi, labda akienda nje ya nchi tutaikosa huduma yake.
 
Lisu hamna kitu tena, kaisha kisiasa.
 
Kwa kuwa si dalali...
Kwa kuwa ni nabii...
Itapendeza sana akianzisha Chama chake!
waTanzania wengi watakuwa nyuma yake!
Tafadhali mwambie ahame haraka sana!
 
Mnaokoteza tu habari ili iweje ? au ndio mupate hizi point wanazogawa jf ?
Licha ya kutokuziamini sana hizi habari, lakini ipo hoja ndani yake kwa huyu mwandishi nisiyempenda

👇👇
Habari ni kuwa ndugu Lissu anatarajia kuondoka na kuihama CHADEMA muda wowote kuanzia sasa.hii ni baada ya kutoridhika na mwenendo na aina ya siasa zinazoendeshwa na ndugu Mbowe. Lissu anaamini kuwa masuala mbalimbali ambayo CHADEMA inayahitaji hasa suala la katiba mpya hayawezi kufanikiwa wala kupatikana kwa kufanya mazungumzo muda wote na CCM au kwa njia ya vikao vya maridhiano ambavyo vimekuwa vikifanywa kati ya CHADEMA na CCM.

Tundu Lissu anadai na kusisitiza ya kuwa CCM haipo tayari kuwapa katiba mpya Watanzania na kwamba haiwezi kujikaanga kwa mafuta yake.lakini pia Lissu anadai ya kuwa Mwenyekiti wake ameshatekwa nyara kiakili na CCM na kwa sasa hana nguvu wala uwezo wa kusimamia misimamo ya chama na ile ya awali.Lissu anadai ya kuwa kwa sasa Mbowe hawezi kuivusha CHADEMA katika kuwaongoza wanachama kupigania kile wanachama wanachohitaji.anasema Mbowe amekipotezea mvuto na ushawishi chama kwa wananchi kwa maamuzi yake ya tamaa na faida za muda mfupi.

Hizo siyo hoja za kubeza mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…