Tetesi: Lissu kuhama CHADEMA muda wowote kuanzia sasa


Kama utakuwa umebakiwa na akili japo kidogo sana ya kuelewa ukielekezwa, haraka sana waombe ndugu zako wakupeleke pale hospitali ya rufaa, uwahishwe hospitali maalum ya Milembe. Using'ang'anie kwenda pekee yako hospitali. Unaweza kuzidiwa na ukafanya mambo ya ajabu. Magonjwa ya akili ni vigumu sana kujua nini kitafuata baada ya muda mfupi.
 
Kwa kuwa si dalali...
Kwa kuwa ni nabii...
Itapendeza sana akianzisha Chama chake!
waTanzania wengi watakuwa nyuma yake!
Tafadhali mwambie ahame haraka sana!
Kuanzisha chama kipya from zero ground ni shida,hadi kisajiliwe na kupata wafuasi wanachama na washabiki itachukua muda.
Kama ni kuunganisha vyama vidogo nako kuna mtihani kwanini havitoa tofauti zao hadi leo ni uchu wa madaraka.
Labda Lissu ana tofauti katika muda wa kupata katiba anataka speed iongezwe wakati labda Mbowe anapitia kifungu hadi kifungu kwa imakini zaidi at slow speed.Lakini hayo ni ya kawaida ndani vyama vya siasa.Sioni dalili,za Lissu kuhamia chama kingine.
 
Mlugaluga hapa umepuyanga sana. Hii hadithi yako wameshaisimulia wengi humu sijui ulikuwa wapi hadi leo ndiyo unaileta kama habari. Kama umeamini hii ndiyo kilipuzi cha kuilipua Chadema basi ufahamu wako uko chini sana.
Endelea kuweweseka.moyo wa mtu kichaka.
 
MIMI SI MFUASI WA MTU, CHAMA, DINI, TEAM na takataka nyingine. Ni mfuasi wa Ideas.

Mkuu, kwa hakika uko vizuri:

1. Kwani hakuna aliyesema wewe ni "MFUASI WA MTU, CHAMA, DINI, TEAM na takataka nyingine. Au hata kuwa si mfuasi wa Ideas?"

2. Na pia hayupo aliyesema yeye ni "MFUASI WA MTU, CHAMA, DINI, TEAM na takataka nyingine. Ati kuwa yeye si mfuasi wa Ideas?"

3. Wandugu Mag3, denoo JG na wale wengine si haba kutambua; "kama ilivyo kwa huyu ndugu Chizi Maarifa, uchawa kama trade mark, una wenyewe!"
 
Ende tu akajimalize kisiasa!
 
Tundu Lissu anadai na kusisitiza ya kuwa CCM haipo tayari kuwapa katiba mpya Watanzania na kwamba haiwezi kujikaanga kwa mafuta yake.lakini pia Lissu anadai ya kuwa Mwenyekiti wake ameshatekwa nyara kiakili na CCM
Kwamba CDM inafanana na chapa ya jogoo pale Magomeni usalama!
 
Lissu akihama chadema nitamuona mwehu wa mwaka. Kamiminiwa risasi mbowe ndio aliesimamia matibabu yake.athamini hicho kwanza.
 
Anakuja kwako ndugu Luca au bustani ya kijani🤔
 
Anataka kutumia mbinu gani zaidi ya maandamano? Au anataka kuingia msituni?
 
Endelea kuweweseka.moyo wa mtu kichaka.
Hujui kitu. Hii riwaya iko humu kitambo tu nashangaa wewe kuifanya ni investigative reporting. Hakuna kitu kama hicho, yawezekana wakawa na mawazo tofauti lakini yenye kufikia lengo moja linalofanana. Ulichoandika ni matamanio ya maccm wote.

Punguza ujuaji wa kilugaluga ndiyo maana unapishana na teuzi kila uchao. Unaandika upuuzi mwingi ukiamini unawafurahisha mamlaka za uteuzi kumbe ndiyo unazidi kujianika kuwa wewe ni mweupe kichwani. Ungetulia kidogo hata miezi miwili unaweza kufikiriwa,lakini haya mabandiko yako bandika bandua unaonekana kama dishi limeyumba fulani hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…