Uchaguzi 2020 Lissu, kujaza watu wakati huu usifurahie maana ndivyo unavyochuja

Uchaguzi 2020 Lissu, kujaza watu wakati huu usifurahie maana ndivyo unavyochuja

Japhet Karibu

Member
Joined
Feb 27, 2020
Posts
79
Reaction score
129
Mteuliwa wa CHADEMA Ndugu Tundu Lissu asifurahie sana anapoona wingi wa watu wakijitokeza kumuona kwani endapo atapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa mgombea kamili wa kiti cha Urais akipita tena katika maeneo hayo wingi wa watu utakuwa ni mdogo sana kwa sababu walishamuona mwanzo na hakuwa na hoja ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
 
Wanakwenda kusikilize hoja ama kushangaa. Inakuwaje mtu apigwe risasi 16 apone?

lakini nadhani atapata kura nyingi damu ya kupendwa anayo.
 
Unawaza kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza Kwa-Mtogole Sekondari...

Tundu ana zaidi ya kile unachokiona wewe na hakichuji hata kama atatembea Tanzania hii yote kwa mwaka mzima...!!!

Huyu jamaa ni "Orator" mzuri na ndicho ambacho kinawavutia watu kutaka kumuona na kumsikiliza. Anajua kuhutubia na kuwakuna watu na kutamani kumuona na anapohutubia, mtu hatamani amalize, hutamani aendelee tu kuzungumza...!!

Hata wakati wa Bunge LIVE, watu waliokuwa wanafuatilia matangazo ya bunge wakati huo, kama ikitokea siku hiyo baadhi ya wabunge hawakuongea, hakuna furaha siku hiyo....

Miongoni mwa wabunge hao wenye mvuto kuwatazama na kuwasikiliza alikuwa Tundu Lissu....

By the way, Magufuli katembea na kutangazwa kwa miaka mitano yote. Kwa maana hiyo NEC ikimteua kuwa mgombea na kuanza kutembea kwenye kampeni zake hatapata watu kwa sababu amechuja siyo?
 
HUU UMATI TU WA SASA UMESHAMPA JIWE UJUMBE MZITO NA KUMKOSESHA USINGIZI. KWANI SASA WEWE UNATAKA SAFARI YA PILI AKIPITA TENA WAJAE HIVI ILI MZEE AZIMIE? HALI NI NGUMU KWA MZEE NDUGU YANGU. LISSU NI ANOTHER LEVEL
 
Na aliyekuwa anajaza watu na kusikika yeye tu kwenye vyombo vya habari kwa miaka mitano itakuwaje?
 
Mteuliwa wa Chadema Ndugu Tundu Lissu asifurahie sana anapoona wingi wa watu wakijitokeza kumuona kwani endapo atapitishwa na tume ya uchaguzi kuwa mgombea kamili wa kiti cha Urais akipita tena katika maeneo hayo wingi wa watu utakuwa ni mdogo sana kwa sababu walishamuona mwanzo na hakuwa na hoja ya msingi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
KILA MTU NI TUNDU LISSU, TUNDU LISSU ! Mpaka manabii wa Tundu mnaibuka sasa, hii ni rasharasha ya vuli tu subiri masika yenyewe
 
Back
Top Bottom