Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Porojo gani mkuu maana kinajadiliwa na kuitishwa hakiusiani na mikataba ya sasa ya ACACIA bali wawekazaji wajao?
Sasa sijui tunawadhibiti vipi ili watulipe yale mamilioni???
Bado ubwabwa wa shingo haujawatoka...waacheni wakubwa zenu wafanye mambo.
 
Nyie mtaendelea ku-suffer intellectual subjugation. Miswad siyo siri, ilisambazwa kwa umma na ofisi ya Bunge siku ya Alhamis Jume 29. Kwa wanaojua kusoma kama mimi tuliisoma (jumla page 110; 68+11+11) na tunajua kilichomo. Hiyo habari ya kucheza ngoma ya Acacia chezeni ninyi na Lissu wenu, siyo wazalendo kama sisi tunaojitambua. Tangu lini makampuni ya kigeni yakawa na viti bungeni katika nchi/dola yenye mamlaka? Inaelekea hata hamjui mnasema nini. Kwenye comment yangu hapo juu miwenukuu hata vifungu mahsusi; chukua mswada husika, soma, siyo kutegemea vijimaneno vya Lissu. Tundu Lissu ni Mwanasheria msomi kwa nini kwenye bandiko lake hanukuu hata kifungu kimoja Zaidi ya blah blah? Kuna mambo mengine ya kufanya siyo huo uwakala wenu kwa Acacia. Mmekwishashindwa!
 
Hakuna mtu anachukiwa na Mzee wa kick kama Lissu!
 

Lissu anaposha umma

Lissu ni mwanasheria
Mimi sio mwanasheria
Ila najua, siku zote sheria ikitungwa mpya
Huwa airudi nyuma
Kwa maana ya kuwa mambo mengine yote yalikubaliwa kabla ya sheria mpya hiyo kutungwa huwa ayahusiki

Kwa mantini ni kweli, mikataba ya huko nyuma haitahusika na sheria hii mpya

Ila pamoja na yote hayo, bado kuna room ya serikali na Barrick gold mine kureview nikataba yote ya huko nyuma
Ili kila mmoja wetu apake kwa jinsi inavyostahiki

Na ndio maana alipokuja mwenyekiti wa Barrick
Walikubaliana serikali na Barrick
Wote wataunda kamati
Then wakae chini wapitie mikataba yote ya nyuma
Kuangalia wapi kuna matatizo

Na ndio sababu kubwa iliyofanya
Miswada hii mitatu kupelekwa bungeni under certificate of urgency

Ili makubaliano hayo watakayokubaliana, ya reflect sheria mpya za madini

Na kwa taarifa tu, kwa mujibu wa tafiti za madini Tanzania

Mpaka sasa ni 4% tu ya madini yote yaliyipo Tanzania ikiwemo mafuta na gas ndio imeshachibwa
96% ya madini nado haijagushwa
Kwa mantini hiyo

Miswada hii ya sheria
Pindi itakapi kuwa sheria
Ni dhahiri ina manufaa makubwa sana kwa taifa letu
 
Tatizo haaminiki na chama tawala!
Hata chama chake kingemuamini wangempa nafasi ya juu zaidi ya halipo sasa, nafikiri kwa akili na elimu yake angefanya mambo makubwa na mazuri zaidi.
 
Wakati tunajadili na kuchukua maoni ya wadau hakuwepo leo hii anatujia na porojo!!

HII NI HABARI NJEMA KWA WAZUNGUSHA MIKONO...LISSU KESHAJUA VILAZA WANARAKA NINI...NA ATAWAPA NA KUENDELEA KUWAPA HIKO MNACHOKITAKA. ..

Namkubali Rugemeleza
Msomi makini hawezi kuitwa na vilaza akaitikia wito. Siku Lissu akianza kuitwa na watu kama nyie na akaitika, atakuwa kafika mwisho kama alivyofika Prof Kabudi!
 
Mkuu umeelewaka vizuri tu ila ndiyo hivyo tena Tundu Lissu ameshaongea hakosolewi.
 
Lissu sijui hakumuelewa Magu au ndo muendelezo wake wa kuponda kila kitu? Rais alisema Acacia na timu ya wataalam wa TZ watakaa warekebishe mkataba ili kuwe na win-win situation, hajasema bunge ndo litafanya kazi hiyo
Wakikataa tutawafanya nini!? Tutatumia nini kuwalazimisha!? Huu ndo mgogoro uliopo kati ya Lisu na Mkuu pamoja na hao anaowaita wapambe. Mimi ndicho nilichoelewa na kweli kinafikirisha kimantiki
 
Ww unayejitambua, mzalendo endelea kulia na makanikia, na sheria yako ya 2017. Hakuna kitu utabadilisha kwa wawekezaji, zaidi endelea kubariki wizi.
 
I like it vision tangu mwanzo wa hii issue#tundu lissu
 
Kwani mmesahau kale kawimbo ketu. ni ileile eee ni ileileeeee
 
Lissu sijui hakumuelewa Magu au ndo muendelezo wake wa kuponda kila kitu? Rais alisema Acacia na timu ya wataalam wa TZ watakaa warekebishe mkataba ili kuwe na win-win situation, hajasema bunge ndo litafanya kazi hiyo
Haya marekebisho ya sheria yametokana na reports 2 za makanikia zilizosomwa kwa mheshimiwa Rais , sasa kama hazihusu makamapuni yaliyopo tayari acacia inclusive ,sasa zina maana gani? Hebu jibu swali, kua mgodi gani tz ambao hakuna mwenyewe? Je hzi zitatumika wapi?
 
Nimemuelewa vizuri, kaongea mantiki ila tunasubiri pia la kushtakiwa na acacia kama alivyoshadadia mwanzo!!
Sasa kama hii miswada haiwahusu hawa Investors wa awali ina maana wao Acacia wataendelea na mambo yao km kawa,kwa mantiki hiyo,hakutakuwa kuwa tena na mashtaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…