Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Tatizo Lissu yuko nje ya mduara, anacho kisema kitabaki kuwa mawazo yake binafsi.
 
Lissu sijui hakumuelewa Magu au ndo muendelezo wake wa kuponda kila kitu? Rais alisema Acacia na timu ya wataalam wa TZ watakaa warekebishe mkataba ili kuwe na win-win situation, hajasema bunge ndo litafanya kazi hiyo
 
Ameandika Tundu Antipas Mughwai Lissu, namuita Profesa wa Sheria.

"Leo Bunge linajadili Muswada wa marekebisho ya sheria za madini na za kodi katika sekta ya madini.

Makampuni ya kigeni ambayo yametunyonya tangu miaka ya mwisho ya '90, na yanaendelea kutunyonya hadi sasa, hayapo kwenye mjadala huu.

Acacia Mining PLC, ambayo Magufuli na maprofesa wake wamedai imetupiga zaidi ya shilingi trilioni 139 wakati haina hata leseni ya uchimbaji madini, nayo haipo kwenye mjadala huu.

Kama nilivyotabiri mwezi uliopita, Magufuli amesalimu amri mbele ya makampuni haya na mbele ya Acacia Mining PLC.

Naomba kufafanua.

Muswada unaojadiliwa leo umetamka wazi kuwa mikataba ya uendelezaji madini iliyopo sasa itaendelea.

Hii ni pamoja na mikataba ya Acacia Mining PLC kuhusu Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara. Kwa Muswada huu, mikataba hii ni halali.

Kusalimu amri huku kwa Magufuli kuna maana kubwa sana.

Mjadala wa makinikia ya dhahabu sasa ndio umezikwa rasmi.

Kama mikataba ya Acacia Mining PLC ni halali, maana yake ni kwamba usafirishaji wa makinikia ulikuwa halali muda wote. Watayarudishiwa makinikia yao kimya kimya.

Sidhani kama tutamsikia mtukufu Rais wetu akizungumzia makinikia tena. Na mtakaong'ang'ania tuyajadili mtaanza kutishwa ili mnyamaze.

Hayo matrilioni ya akina Prof. Mruma na Prof. Osoro ndio hatutayasikia tena. Yalikuwa ni ya uongo, 'professorial rubbish', tangu mwanzo.

Ndio maana hata wabunge wameambiwa Taarifa za hao wasomi wabobezi ni mali ya Rais peke yake. Wengine haturuhusiwi kuziona.

Kama mikataba ni halali kwa mujibu wa Muswada wa leo, maana yake nyingine ni kuwa waliohusika kuiandaa au kuisaini hawana kosa lolote.

Hoja ya kuwashtaki akina Chenge, Ngeleja, Muhongo na wengineo waliotajwa kwa majina na Kamati ya Prof. Osoro, nayo sasa ni marehemu.

Kama mikataba ni halali watakamatwa na kushtakiwa kwa kosa gani???

Kwa hiyo, kwenye signature issue yake kubwa juu ya rasilmali zetu, huyu anayeitwa mtetezi wa wanyonge na mlinzi wa rasilmali zetu, ameshindwa vibaya. Magufuli ameshindwa, kama nilivyosema atashindwa.

Kwa Muswada huu, Magufuli ameendeleza na kuhalalisha matendo ya watangulizi wake Mkapa na Kikwete ya kugawa rasilmali zetu kwa wageni.

Kwa Muswada huu, waliotunyonya na kutuibia juzi na jana na wanatuibia leo, wataendelea kutunyonya na kutuibia kesho na kesho kutwa.

Muswada wa leo unafanya mabadiliko makubwa ya kisheria kwa makampuni yatakayokuja miaka ijayo.

Sawa kabisa. Lakini naomba Magufuli na wapambe wake watusaidie hili: hivi ni sehemu gani ya nchi yetu ambayo ina madini na hayana mwenyewe tayari???

Ni sehemu ipi ya eneo letu la bahari au eneo maalum la kiuchumi ambalo bado halina mikataba ya kutafuta au kuchimba mafuta au gesi asilia???

Nchi hii ilishagawanywa vipande vipande na kupewa wawekezaji wakati wa Mkapa na Kikwete.

Muswada huu ni mzuri kwenye karatasi, kiuhalisia sheria yake haitatekelezeka kwa sababu mali tayari ilishauzwa na Muswada huu umebariki biashara hiyo.

Magufuli na watu wake hawataki watanzania wajue hili. Ndio maana Muswada unaletwa kwa dharura, ili kusiwe na mjadala wowote wa kuna.

Baadae kidogo nitazungumzia Sheria mpya zilizopitishwa jana kwa mpigo na kwa Hati ya Dharura. Sheria hizo ni uongo mwingine mkubwa kwa watanzania....."

Wadanganyika mpooooo? Je mnafahamu kuwa Yule mwanaume alikuja hapa alikubali kutulipa pesa tulizopoteza kwa kipindi chote cha Miaka 18?

Vitoto vidogo vya Lumumba viliandamana kupongeza Magufuli kumponda Lissu. Aya sasa OleIle Sheria haiwahusu wale wanaoendelea kupiga pesa kupitia madini hayo.......
 
Lissu sijui hakumuelewa Magu au ndo muendelezo wake wa kuponda kila kitu? Rais alisema Acacia na timu ya wataalam wa TZ watakaa warekebishe mkataba ili kuwe na win-win situation, hajasema bunge ndo litafanya kazi hiyo
Brother wewe ndiye hukumuelewa, alisema atawaongezea muda wabunge wajadili mikataba na kubadili sheria za madini.
 
Nimemuelewa vizuri, kaongea mantiki ila tunasubiri pia la kushtakiwa na acacia kama alivyoshadadia mwanzo!!
 
watz mshapigwa changa la macho kwa mara nyengine tena kama kawaida yao na usaani wa kisiasa, "hapa kazi tu" umasikini daima
 
Kila siku nasema hivi "kila mwanaCCM ana mapungufu aidha ya elimu, uzalendo ,habari sahihi au akili"
Wapo vijana watakaoandamana kwa kumsapoti rais kwa sheria mpya ya maliasili zetu huku kwa uhalisia haina manufaa makukwa kwa Watanzania.
 
Mimi Nasubiria noah yangu tu hapa,nahofia isije ikafika bandarini ikakosa mwenyewe kama vile vichwa vya treni 13.Msicheze mbali na bandari jamani.
 
Kila siku nasema hivi "kila mwanaCCM ana mapungufu aidha ya elimu, uzalendo ,habari sahihi au akili"
Wapo vijana watakaoandamana kwa kumsapoti rais kwa sheria mpya ya maliasili zetu huku kwa uhalisia haina manufaa makukwa kwa Watanzania.
We don't fit the definition of human being!!
 
lissu haeleweki yupo upande gani kutwa nzima anaongea na CEO wa acacia alafu anajifanya kuishauri serikali,lissu ni kibaraka wa acacia!sioni mashiko yoyote kwenye andiko lake,
 
Back
Top Bottom