Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Wakati tunajadili na kuchukua maoni ya wadau hakuwepo leo hii anatujia na porojo!!

HII NI HABARI NJEMA KWA WAZUNGUSHA MIKONO...LISSU KESHAJUA VILAZA WANARAKA NINI...NA ATAWAPA NA KUENDELEA KUWAPA HIKO MNACHOKITAKA. ..

Namkubali Rugemeleza
Mimi sijawahi kuzungusha mikono yangu popote wala kuitika ndio mahali popote,Lakini maoni haya ya Lisu yameniingia barabara kama mwenye nchi yangu,sasa wewe unaejaribu kutetea tumbo lako utaniambia nini nisiye zungusha mikono alaf nimuelewa.
 
"itaendelea kutambuliwa kwa sharti la kufanyiwa marekebisho"

Hiyo tafsiri unaipata wapi?
haya soma sheria hizo kisha tupatie tafsiri sahihi ya vifungu husika kuhusiana na suala hili.
 
Makampuni ya madini kama Barrick na mtoto wao Acacia walishaingia mkataba na Tanzania.Ili Tanzania iweze kubadili mikataba iliyosainiwa huko nyuma ni lazima kwanza ubadili baadhi ya vifungu vya sheria inayosimamia sekta ya madini. Hiki ndicho kitachofuata baada ya muswada kuwa sheria, kwamba Tanzania itaanza majadiliano na makampuni ya madini kuhusu TERMS OF BUSINESS. Huwezi kufanya mazungumzo - negotiate new terms of business - kama sheria zako hazikupigi wigo wa kufanya hivyo.

Wakati mwingine inatia kinyaa kuona arrogance ya Lissu so publicly displayed. Ni kwanini Lissu anakosa mipaka ya kudharau Watanzania (kwa ujumla wao) kwa kujiona kuwa yeye ndiye anayelewa mambo zaidi ya wengine.

Kama kweli alikuwa mwerevu, ni kwanini tangu ashike usukani CHADEMA, kama Chama kimekosa mwelekeo? Zitto pamoja na mapungufu yake bado ameweza kuongoza ADC kuchambua miswada na kuwasilisha michango yao. CHADEMA na huyo 'learned brother' wao wamebakia kubuni rangi ya mavazi ya kuvaa bungeni! Very unfortunate. Hata kwenye hili?
 
Tundu Lisu nakushauri utunge Kitabu kuhusu sakata LA wizi wa maliasili za Tanzania hususan wizi wa madini! Utakuwa umeitendea haki sana nchi yetu na utakuwa ni mchango uliotukuka utakaodumu milele!
 
Tundu Lissu kuonyesha yuko vizuri angewapa ushauri wa bure na technicalities ya vipi tutanasuka katika hili

Alishafanya hivyo kwa kutumia mfano wa Hugo Chavez pia Bolivia
 
IMG-20170704-WA0004.jpg
 
Lissu sijui hakumuelewa Magu au ndo muendelezo wake wa kuponda kila kitu? Rais alisema Acacia na timu ya wataalam wa TZ watakaa warekebishe mkataba ili kuwe na win-win situation, hajasema bunge ndo litafanya kazi hiyo
Taarifa iliyotoka siku ile ni kulipwa mwekezaji alitubu na kukiri kutuibia au hajapewa A/C ya malipo?
 
Swali. ACACIA wakitaka kuchimba kwenye mgodi mwingine, let say, upo Kigoma, ina maana mabadiliko haya hayatawagusa??
Wenzio walishamaliza maeneo yenye mashapo makubwa ya dhahabu iliyobaki ni maeneo ambayo tutachimba sisi wadogo na vikampuni vidogo
Kwenye sheria wameruhusu mchimbaji ndogo kuajiri kampuni la kigeni kwa maana ya kuchimba na kwenye mikataba hayataguswa kwani mwenye leseni ni mchimbaji mdogo
 
Nimemuelewa vizuri, kaongea mantiki ila tunasubiri pia la kushtakiwa na acacia kama alivyoshadadia mwanzo!!

Watashitakiwa vp wakat umesikia mikataba yao haitaguswa?....maana yake tumeacha waendelee kutunyonya kama awal.
 
Sheria zinatumika kinyume kinyume?

Alafu unatumia neno "shall" wakati huo huo unategemea majadiliano kati ya wewe na muwekezaji ndio yaamue hatima ya sheria na mikataba hiyo?Wakigoma utawabana kwa lipi?

No wonder mumeileta kwa hati ya dharura na kutoa nafsi finyu za wapinzani kuchangia ili watu wasipate nafasi ya kuibua mapungufu haya.

Hiizi cosmetic language hazitatufikisha popote.
 
Nimeamini Magufuli anatafuta kiki za 2020 bahati mbaya hazita msaidia kwa lolote.
 
upuuzi tu..mtu unajidai msomi unashusha mistari ya kibongo fleva kumkejeli rais mzalendo kama magufuli. kibarua acacia wanakulipa bei gani..mtu mzima ovyoooo.
Imekuingia kisawasawa, mzalendo asiyetumia mikakati sahihi ni mtu anayepoteza muda. Tunao wazalendo wengi nchi hii ila shida ni pale tunapotaka mzalendo na kiongozi. Poor magu! Alitakiwa aongoze familia yake pekee lakin sasa ni rais
 
~~~>>> CCM~ Chama cha Makinikia
 
Mimi nilidhani, kwasababu Lissu ni mbunge angetoa huo mchango wake kwanza kule bungeni. Kama hawakumsikiliza ndio aje huku. Nafikiri ndio ingekuwa busara.
Walishaweka pamba skioni, hawataki kuskia yanayotoka kwa lissu, hawataki hata kidogo, wanaamin atapata promo kisiasa
 
Narudia kusema,watu aina ya Tundu Lissu hakupaswa kuzaliwa katika nchi kama hii bali walipaswa kuzaliwa katika nchi za wenzetu ambako bila shaka wangekuwa wameshapata recognition.

Bahati mbaya sana maoni haya ya kina Lissu yanaishia tu mitandaoni ila ya bwana yule ndio yanatangazwa dunia muzima na bahati mbaya sana sisi binadamu wengi hatutafuti habari za siasa na wanasiasa kama tunavyotafuta habari zinazohusu gossip,sex,soccer,jokes,etc na badala yake tunasubiri kuletewa/kutangaziwa habari hizi na bahati mbaya zaidi kwa hapa kwetu habari zinazotangazwa zaidi na media ni zile za watawala na sio hizi za kina Lissu tunazopaswa kuzitafuta mitandaoni na kwingineko.

Angalieni hata magazeti yetu siku hizi yalivyojaa ushabiki.

Tundu Lissu nakushauri angalia uwezekano wa kuongea na wahariri wa vyombo vya habari ili wakusaidie kufikisha kwa wananchi haya unayosema na kuyaandika mitandaoni maana wengi hayawafikii.
Ndugu yangu usisumbuke bure, Watanzania hawana sababu ya kutafuta ukweli au weledi wa kujua kinachoendelea ndani ya Taifa lao, Watanzania wamebakia kuwa washangiliaji hata kwa yale ambayo yanawaumiza direct, kwa sababu wengi ya Watz ni MENTAL DISORDERS.
 
Back
Top Bottom