Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Lissu: Makampuni yaliyotunyonya tangu 90's hayapo kwenye sheria ya madini

Mi nasubiria tutangaziwe kuwa sasa zile trilioni 108 zimeshatumbukizwa hazina na tayari zianze kutuika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo kama kujenga reli ya kati SGR hadi Kigoma, Mwanza na Karema. Pia kukarababati na kujenga barabara zote zinazounganisha mikoa na wilaya zetu. Kuweka sawa miundombinu ya hospitali zetu kwa ngazi zote, etc...

But somehow, picha hii iko hafifu sana akilini kwangu, na iliyo angavu ni ile inayoonyesha mjadala wa makinikia ukipigwa stop kama ule wa Faru Joni. Tayari tumeshaambiwa kuwa ripoti za maprofesa ni siri ya raisi japo tulisomewa hadharani. Huo ni mwanzo tu.

Mungu ibariki Tanzania.
Mradi unaosubiriwa kwa hamu kubwa na watanzania wote ni "Noah kwa kila mtanzania"
 
Kwa hiyo mnamuamini sana Lissu kuwa mikataba iliyopo haitarekebishwa? Duu! watanzania tumerogwa sana
 
Anaandika Mhe. Tundu Lissu

Leo Bunge linajadili Muswada wa marekebisho ya sheria za madini na za kodi katika sekta ya madini.

Makampuni ya kigeni ambayo yametunyonya tangu miaka ya mwisho ya '90, na yanaendelea kutunyonya hadi sasa, hayapo kwenye mjadala huu.

Acacia Mining PLC, ambayo Magufuli na maprofesa wake wamedai imetupiga zaidi ya shilingi trilioni 139 wakati haina hata leseni ya uchimbaji madini, nayo haipo kwenye mjadala huu.

Kama nilivyotabiri mwezi uliopita, Magufuli amesalimu amri mbele ya makampuni haya na mbele ya Acacia Mining PLC.

Naomba kufafanua.

Muswada unaojadiliwa leo umetamka wazi kuwa mikataba ya uendelezaji madini iliyopo sasa itaendelea.

Hii ni pamoja na mikataba ya Acacia Mining PLC kuhusu Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara. Kwa Muswada huu, mikataba hii ni halali.

Kusalimu amri huku kwa Magufuli kuna maana kubwa sana.

Mjadala wa makinikia ya dhahabu sasa ndio umezikwa rasmi.

Kama mikataba ya Acacia Mining PLC ni halali, maana yake ni kwamba usafirishaji wa makinikia ulikuwa halali muda wote. Watayarudishiwa makinikia yao kimya kimya.

Sidhani kama tutamsikia mtukufu Rais wetu akizungumzia makinikia tena. Na mtakaong'ang'ania tuyajadili mtaanza kutishwa ili mnyamaze.

Hayo matrilioni ya akina Prof. Mruma na Prof. Osoro ndio hatutayasikia tena. Yalikuwa ni ya uongo, 'professorial rubbish', tangu mwanzo.

Ndio maana hata wabunge wameambiwa Taarifa za hao wasomi wabobezi ni mali ya Rais peke yake. Wengine haturuhusiwi kuziona.

Kama mikataba ni halali kwa mujibu wa Muswada wa leo, maana yake nyingine ni kuwa waliohusika kuiandaa au kuisaini hawana kosa lolote.

Hoja ya kuwashtaki akina Chenge, Ngeleja, Muhongo na wengineo waliotajwa kwa majina na Kamati ya Prof. Osoro, nayo sasa ni marehemu.

Kama mikataba ni halali watakamatwa na kushtakiwa kwa kosa gani???

Kwa hiyo, kwenye signature issue yake kubwa juu ya rasilmali zetu, huyu anayeitwa mtetezi wa wanyonge na mlinzi wa rasilmali zetu, ameshindwa vibaya. Magufuli ameshindwa, kama nilivyosema atashindwa.

Kwa Muswada huu, Magufuli ameendeleza na kuhalalisha matendo ya watangulizi wake Mkapa na Kikwete ya kugawa rasilmali zetu kwa wageni.

Kwa Muswada huu, waliotunyonya na kutuibia juzi na jana na wanatuibia leo, wataendelea kutunyonya na kutuibia kesho na kesho kutwa.

Muswada wa leo unafanya mabadiliko makubwa ya kisheria kwa makampuni yatakayokuja miaka ijayo.

Sawa kabisa. Lakini naomba Magufuli na wapambe wake watusaidie hili: hivi ni sehemu gani ya nchi yetu ambayo ina madini na hayana mwenyewe tayari???

Ni sehemu ipi ya eneo letu la bahari au eneo maalum la kiuchumi ambalo bado halina mikataba ya kutafuta au kuchimba mafuta au gesi asilia???

Nchi hii ilishagawanywa vipande vipande na kupewa wawekezaji wakati wa Mkapa na Kikwete.

Muswada huu ni mzuri kwenye karatasi, kiuhalisia sheria yake haitatekelezeka kwa sababu mali tayari ilishauzwa na Muswada huu umebariki biashara hiyo.

Magufuli na watu wake hawataki watanzania wajue hili. Ndio maana Muswada unaletwa kwa dharura, ili kusiwe na mjadala wowote wa kuna.

Baadae kidogo nitazungumzia Sheria mpya zilizopitishwa jana kwa mpigo na kwa Hati ya Dharura. Sheria hizo ni uongo mwingine mkubwa kwa watanzania.
upuuzi tu..mtu unajidai msomi unashusha mistari ya kibongo fleva kumkejeli rais mzalendo kama magufuli. kibarua acacia wanakulipa bei gani..mtu mzima ovyoooo.
 
Nimemuelewa vizuri, kaongea mantiki ila tunasubiri pia la kushtakiwa na acacia kama alivyoshadadia mwanzo!!
Hisa za mkapa au za kikwete au za wote hao zimepewa Pombe na zinamilikiwa na yohana!
Kuna mashtaka tena hapo!
 
upuuzi tu..mtu unajidai msomi unashusha mistari ya kibongo fleva kumkejeli rais mzalendo kama magufuli. kibarua acacia wanakulipa bei gani..mtu mzima ovyoooo.
Asante "mzee yusufu"

Tuachie lisu wetu nyie hangaikeni na makinikia.
 
Hii nchi mbona wanaifanya kuwa ngumu, kila siku tunaambiwa hii nchi ni tajiri mbona utajiri wanachukua wengine kiulaini tu na sheria laini tunawatungia sisi
We angalia shambani kwako Kama kuna madini au mafuta chimba uuze huko kwingine yalishafanyiwa booking
 
CCM wamechezeshea watanzania the biggest comedy kama taarifa za Tundu Lissu ziko sahihi.
 
Mimi nilidhani, kwasababu Lissu ni mbunge angetoa huo mchango wake kwanza kule bungeni. Kama hawakumsikiliza ndio aje huku. Nafikiri ndio ingekuwa busara.
 
Huyu Bwana ni mwongo. Kama ni mkweli angezungumza haya bungeni badala ya kupiga/kuendesha kampeini binafsi kwenye mitandao ya kijamii. Kwa nini asitumie fursa ya jukwaa rasmi la kujadili sera za serikali (Bunge) kuwasilisha hoja (kama ni hoja kweli) kushawishi wabunge wenzake ili wabadilishe maudhui ya muswada husika?


Lakini tafsiri ya maneno ya kejeli na kutukana yanayosheheni kwenye hoja ya Lissu ni dhahiri kuwa amekata tamaa, sasa anazungumza chochote kinachotokea kinywani mwake.


Kwa mantiki ya kawaida, na hata kwa mtu asiyekuwa mwanasheria lakini amesoma na kuelewa miswada husika anajua kuwa mara baada ya kupitishwa jana na kisha kusainiwa na Rais [hata Prof. Kabudi jana alithibitisha hivyo mara baada ya kupitisha miswada ya jana], Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 (someni vifungu PART III kifungu cha 6 na 7] ikisomwa kwa pamoja na Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali, 2017, ndio itakayotumika ku-review mikataba ili kui-harmonize na sheria hizi mahsusi kwa ajili ya kurekebisha makosa yaliyofanyika huko nyuma katika ulinzi na udhibiti wa rasilimali za nchi.


Pengine kwa faida ya wasomaji na kuthibitisha uongo wa Tundu Lissu, hebu tusome kwa pamoja kifungu cha 10 cha Muswada wa kutungwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali – Sheria ya Madini, Sheria ya Petroli, Sheria ya Kodi ya Mapato, Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, na Sheria ya Bima, 2017 unaojadiliwa Bungeni leo na ambao Lissu ana uzungumzia;

"The principal Act (hapa ni sheria ya madini inayorekebishwa) is amended by repealing sections 11 and 12 and substituting for them the following, [review and renegotiation of development agreements] '11. Notwithstanding the provisions of this Act and any other written law, all development agreements concluded prior to the coming into force of this section shall, subject to the provisions of the Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Renegotiation of Unconscionable Terms) Act 2017, remain in force'"


Tafsiri ya kifungu hiki ni kuwa mikataba ya madini ambayo taifa liliingia huko nyuma na ambayo inaendelea kuishi hadi sasa imewekewa sharti la kufanyiwa marekebisho ili kuendana na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 iliyopitishwa bungeni jana. Soma PART III kifungu cha 6 na 7 katika sheria hiyo.


Ni bahati mbaya kuona kuwa rafiki yangu Lissu ameamua kuji-intoxicate, na pengine bila kujali hadhi yake kitaaluma.
 
lissu haeleweki yupo upande gani kutwa nzima anaongea na CEO wa acacia alafu anajifanya kuishauri serikali,lissu ni kibaraka wa acacia!sioni mashiko yoyote kwenye andiko lake,
When do you get time?
 
Huyu Bwana ni mwongo. Kama ni mkweli angezungumza haya bungeni badala ya kupiga/kuendesha kampeini binafsi kwenye mitandao ya kijamii. Kwa nini asitunie fursa ya jukwaa rasmi la serikali (Bunge) kuwasilisha hoja (kama ni hoja kweli) kushawishi wabunge wenzake wasite kupitisha/wabadilishe maudhui ya muswada husika?

Lakini tafsiri ya maneno ya kejeli na kutukana yanayosheheni kwenye hoja yake ni dhahiri Lissu amekata tamaa, sasa anazungumza chochote kinachotokea kinywani mwake.

Kwa mantiki ya kawaida, na hata kwa mtu asiyekuwa mwanasheria anajua kuwa mara baada ya kupitishwa jana na zikiisha sainiwa na Rais [hata Prof. Kabudi jana alithibitisha hivyo mara baada ya kupitisha miswada ya jana], Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 (someni vifungu PART III kifungu cha 6 na 7] ikisomwa kwa pamoja na Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali, 2017, ndio itakayotumika ku-review mikataba ili kui-harmonize na sheria hizi mahsusi kwa ajili ya kurekebisha makosa yaliyofanyika huko nyuma.

Pengine kwa faida ya wasomaji na kuthibitisha uongo wa Tundu Lissu, hebu tusome kwa pamoja kifungu cha 10 cha Muswada wa kutungwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali – Sheria ya Madini, Sheria ya Petroli, Sheria ya Kodi ya Mapato, Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, na Sheria ya Bima, 2017 unaojadiliwa Bungeni leo na ambo Lissu anauzungumzia;
"The principal Act (sheria ya madini inayorekebishwa) is amended by repealing sections 11 and 12 and substituting for them the following, [review and renegotiation of development agreements] '11. Notwithstanding the provisions of this Act and any other written law, all development agreements concluded prior to the coming into force of this section shall, subject to the provisions of the Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Renegotiation of Unconscionable Terms) Act 2017, remain in force'"

Tafsiri ya kifungu hiki ni kuwa mikataba ya madini ambayo taifa liliingia huko nyuma itaendelea kutambuliwa kwa sharti la kufanyiwa marekebisho kwa mujibu wa sheria ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 iliyopitishwa bungei jana. Soma PART III kifungu cha 6 na 7 katika sheria hiyo.

Ni bahati mbaya rafiki yangu Lissu ameamua kuji-intoxicate, pengine na hadhi yake kitaaluma.

"itaendelea kutambuliwa kwa sharti la kufanyiwa marekebisho"

Hiyo tafsiri unaipata wapi?
 
Back
Top Bottom