Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,772
- 35,770
Cc jingalaoKuna watu walisema lissu yupo kimya haya kaongea sasa
Cc jingalaoKuna watu walisema lissu yupo kimya haya kaongea sasa
Mwombe dereva wa lori deiwaka.Me nachukiagaa kwahiyoo shule ya udereva tumeendaa buree auu ??????
Hatoagiii anasema ye ndo alichaguliwa kutusombeleaa kwenye Lori lakeee mpakaa kuleeeee !!!!!Mwombe dereva wa lori deiwaka.
Je itaongeza hata kiwanda kimoja?!Yakuwaweka ndani wapinzani
Hata vile vichwa vya treni visivyo na mwenyewe inatosha kuendelezea fani maana kukaa bila noa noma.Hatoagiii anasema ye ndo alichaguliwa kutusombeleaa kwenye Lori lakeee mpakaa kuleeeee !!!!!
Ya kufuga wazunguTumuache Raisi wetu afanye Kazi
Anaandika Mhe. Tundu Lissu
Leo Bunge linajadili Muswada wa marekebisho ya sheria za madini na za kodi katika sekta ya madini.
Makampuni ya kigeni ambayo yametunyonya tangu miaka ya mwisho ya '90, na yanaendelea kutunyonya hadi sasa, hayapo kwenye mjadala huu.
Acacia Mining PLC, ambayo Magufuli na maprofesa wake wamedai imetupiga zaidi ya shilingi trilioni 139 wakati haina hata leseni ya uchimbaji madini, nayo haipo kwenye mjadala huu.
Kama nilivyotabiri mwezi uliopita, Magufuli amesalimu amri mbele ya makampuni haya na mbele ya Acacia Mining PLC.
Naomba kufafanua.
Muswada unaojadiliwa leo umetamka wazi kuwa mikataba ya uendelezaji madini iliyopo sasa itaendelea.
Hii ni pamoja na mikataba ya Acacia Mining PLC kuhusu Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara. Kwa Muswada huu, mikataba hii ni halali.
Kusalimu amri huku kwa Magufuli kuna maana kubwa sana.
Mjadala wa makinikia ya dhahabu sasa ndio umezikwa rasmi.
Kama mikataba ya Acacia Mining PLC ni halali, maana yake ni kwamba usafirishaji wa makinikia ulikuwa halali muda wote. Watayarudishiwa makinikia yao kimya kimya.
Sidhani kama tutamsikia mtukufu Rais wetu akizungumzia makinikia tena. Na mtakaong'ang'ania tuyajadili mtaanza kutishwa ili mnyamaze.
Hayo matrilioni ya akina Prof. Mruma na Prof. Osoro ndio hatutayasikia tena. Yalikuwa ni ya uongo, 'professorial rubbish', tangu mwanzo.
Ndio maana hata wabunge wameambiwa Taarifa za hao wasomi wabobezi ni mali ya Rais peke yake. Wengine haturuhusiwi kuziona.
Kama mikataba ni halali kwa mujibu wa Muswada wa leo, maana yake nyingine ni kuwa waliohusika kuiandaa au kuisaini hawana kosa lolote.
Hoja ya kuwashtaki akina Chenge, Ngeleja, Muhongo na wengineo waliotajwa kwa majina na Kamati ya Prof. Osoro, nayo sasa ni marehemu.
Kama mikataba ni halali watakamatwa na kushtakiwa kwa kosa gani???
Kwa hiyo, kwenye signature issue yake kubwa juu ya rasilmali zetu, huyu anayeitwa mtetezi wa wanyonge na mlinzi wa rasilmali zetu, ameshindwa vibaya. Magufuli ameshindwa, kama nilivyosema atashindwa.
Kwa Muswada huu, Magufuli ameendeleza na kuhalalisha matendo ya watangulizi wake Mkapa na Kikwete ya kugawa rasilmali zetu kwa wageni.
Kwa Muswada huu, waliotunyonya na kutuibia juzi na jana na wanatuibia leo, wataendelea kutunyonya na kutuibia kesho na kesho kutwa.
Muswada wa leo unafanya mabadiliko makubwa ya kisheria kwa makampuni yatakayokuja miaka ijayo.
Sawa kabisa. Lakini naomba Magufuli na wapambe wake watusaidie hili: hivi ni sehemu gani ya nchi yetu ambayo ina madini na hayana mwenyewe tayari???
Ni sehemu ipi ya eneo letu la bahari au eneo maalum la kiuchumi ambalo bado halina mikataba ya kutafuta au kuchimba mafuta au gesi asilia???
Nchi hii ilishagawanywa vipande vipande na kupewa wawekezaji wakati wa Mkapa na Kikwete.
Muswada huu ni mzuri kwenye karatasi, kiuhalisia sheria yake haitatekelezeka kwa sababu mali tayari ilishauzwa na Muswada huu umebariki biashara hiyo.
Magufuli na watu wake hawataki watanzania wajue hili. Ndio maana Muswada unaletwa kwa dharura, ili kusiwe na mjadala wowote wa kuna.
Baadae kidogo nitazungumzia Sheria mpya zilizopitishwa jana kwa mpigo na kwa Hati ya Dharura. Sheria hizo ni uongo mwingine mkubwa kwa watanzania.
Tulimwambia aje kutoa maoni akakimbia sasa hivi anakuja kujivua nguo na porojo zake za MIGA
Ulisema lissu kakaa kimya!!Wakati tunajadili na kuchukua maoni ya wadau hakuwepo leo hii anatujia na porojo!!
HII NI HABARI NJEMA KWA WAZUNGUSHA MIKONO...LISSU KESHAJUA VILAZA WANARAKA NINI...NA ATAWAPA NA KUENDELEA KUWAPA HIKO MNACHOKITAKA. ..
Namkubali Rugemeleza
Si Rais wenu anajitia kujua??? fanyeni hayo wenyewe!Tundu Lissu kuonyesha yuko vizuri angewapa ushauri wa bure na technicalities ya vipi tutanasuka katika hili
Kama ndio hivyo dharula ilihusu kitu gani sasa, kwa nini watanzania wasipewe muda kujadili mustakabari wa mali zao,nasema tena hapakuhitajika dharula katika hili, aissee aah hapana bwanaNilitegemea Tundu Lisu kama Rais wa chama cha wanasheria angeongea tofauti na alivyofanya, amejikita ku-criticize kama kawaida yake. Waziri wa sharia alisema kuwa sharia mpya huanza kuwa applied pale inapotungwa na kupishwa (haiendi nyuma), na kuwa kwa mikataba ya madini iliyokwishaingiwa kabla ya sharia hii (miswada ya madini iliyo ktk mjadala) basi itabidi waongee na hao wawekezaji ili kukubaliana na baadhi ya mambo.
Kwa hiyo Rais wa wanasheria baada ya kuisoma hiyo miswada na kuzingatia kauli ya waziri wengi tulitegemea angekuja na hoja za kisheria (kutokana na weredi wa members wa hicho chama) ambazo zingeonyesha au kuhalalisha sharia mpya kutumika hata kwa mikataba ya huko nyuma. Kwa ufupi angeshauri ni nini cha kufanya ili maoni hayo yahusishwe ndani ya sharia kabla haijapitishwa.
Badala yake amekuja kuongea kama watu wengine wa kawaida tu. Hapo ndo huwa nashindwa kumwelewa kabisa Lisu; anapenda kuonyesha makosa na umbumbu wa wengine akijichukulia kama ndo mwanasheria mahiri pekee hapa nchini.
Mikataba mingapi hapa Tz inasimamiwa na MIGA?au ni acacia tu?kamà iko mingi huoni kuwa ni ujuha kujitoa MIGA kwa ajil ya kampuni moja tu?Wamesema pande mbili zitakaa wafikie muafaka lkn ww bado unakariri MIGA tu.Hii ni vita unapambana na mabepari wa dunia sio mashamba ya mbowe. Mimi nafikiri jpm na kamati yake wanaona mbali mno kuliko mnavodhani.na msijidanganye kwamba hiyo MIGA serikal haiijui zaid ya lisu tu.Tujiondoe kwenye MIGA kwanza ili tufanye yetu pia hamtaki mkidhani Lissu atashinda; zungukeni wee mtarudi palepale kwa Lissu. Akina Paramagamba wanakufa na ushauri kifuani kisa the Boss ataki kusikia yaliyosemwa na Lissu ndo yamechukuliwa.
Muswada wa sheria uliopita kwa hati ya dharura Lisu anautambua, na hapa anasema ..Huyu Bwana ni mwongo. Kama ni mkweli angezungumza haya bungeni badala ya kupiga/kuendesha kampeini binafsi kwenye mitandao ya kijamii. Kwa nini asitumie fursa ya jukwaa rasmi la kujadili sera za serikali (Bunge) kuwasilisha hoja (kama ni hoja kweli) kushawishi wabunge wenzake ili wabadilishe maudhui ya muswada husika?
Lakini tafsiri ya maneno ya kejeli na kutukana yanayosheheni kwenye hoja ya Lissu ni dhahiri kuwa amekata tamaa, sasa anazungumza chochote kinachotokea kinywani mwake.
Kwa mantiki ya kawaida, na hata kwa mtu asiyekuwa mwanasheria lakini amesoma na kuelewa miswada husika anajua kuwa mara baada ya kupitishwa jana na kisha kusainiwa na Rais [hata Prof. Kabudi jana alithibitisha hivyo mara baada ya kupitisha miswada ya jana], Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 (someni vifungu PART III kifungu cha 6 na 7] ikisomwa kwa pamoja na Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali, 2017, ndio itakayotumika ku-review mikataba ili kui-harmonize na sheria hizi mahsusi kwa ajili ya kurekebisha makosa yaliyofanyika huko nyuma katika ulinzi na udhibiti wa rasilimali za nchi.
Pengine kwa faida ya wasomaji na kuthibitisha uongo wa Tundu Lissu, hebu tusome kwa pamoja kifungu cha 10 cha Muswada wa kutungwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali – Sheria ya Madini, Sheria ya Petroli, Sheria ya Kodi ya Mapato, Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, na Sheria ya Bima, 2017 unaojadiliwa Bungeni leo na ambao Lissu ana uzungumzia;
"The principal Act (hapa ni sheria ya madini inayorekebishwa) is amended by repealing sections 11 and 12 and substituting for them the following, [review and renegotiation of development agreements] '11. Notwithstanding the provisions of this Act and any other written law, all development agreements concluded prior to the coming into force of this section shall, subject to the provisions of the Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Renegotiation of Unconscionable Terms) Act 2017, remain in force'"
Tafsiri ya kifungu hiki ni kuwa mikataba ya madini ambayo taifa liliingia huko nyuma na ambayo inaendelea kuishi hadi sasa imewekewa sharti la kufanyiwa marekebisho ili kuendana na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohusu Maliasili za Nchi, 2017 iliyopitishwa bungeni jana. Soma PART III kifungu cha 6 na 7 katika sheria hiyo.
Ni bahati mbaya kuona kuwa rafiki yangu Lissu ameamua kuji-intoxicate, na pengine bila kujali hadhi yake kitaaluma.
Tunataka mikataba iwekwe waz,hzo swaga unazoleta ww ndo zle zle za zaman,hv ww unaamin vp kuwa hlo litafankiwa na hali ya kuwa hlo suala lilianza kwa waz then leo liishe kwa kificho,how come?Lissu sijui hakumuelewa Magu au ndo muendelezo wake wa kuponda kila kitu? Rais alisema Acacia na timu ya wataalam wa TZ watakaa warekebishe mkataba ili kuwe na win-win situation, hajasema bunge ndo litafanya kazi hiyo
yes alikaa kimya wakati kina Rugemeleza wakitoa maoni....yaani lissu ni kama msomi wa kijijini...unapitisha mkutano wa wasomi hatokei lakini kwenye vijiwe vya gahawa yeye ndio mjuaji.Ulisema lissu kakaa kimya!!