Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna haja ya kufichaficha Style ya Lissu ndio tunayoitaka UVUNDO huwa haifichwi hata ukiuwashia UBANI baadae utaanza kunuka tu.
Taaisi yoyote Duniani ina kitu kinaitwa Siri - sasa kama ni mkutano wa siri wewe unaanza kubwabwaja hadharani ili tukujuie wewe ni mkweli sana ama? Upo wapi uugwana wako?

Je unabakizaje sifa za kuwa kiongozi bora, Leo umetoa siri za mkutano wako na Mbowe na viongozi wa dini kesho utatoa za kamati kuu CDM na kesho kutwa utatoa za nchi.
Hata Serikali ina mambo ya siri ambayo hata ukifukuzwa hutakiwi kuita press na kuanza kubwabwaja, yanabakia yako ili kuilinda taasisi.
Usifikiri unamshambulia Mbowe, unaishambukia Taasisi mzima, yaani nyumba unayotegemea kuishi unaipopoa mawe.

CDM angalieni sana hii kitu.
 
Taaisi yoyote Duniani ina kitu kinaitwa Siri - sasa kama ni mkutano wa siri wewe unaanza kubwabwaja hadharani ili tukujuie wewe ni mkweli sana ama?
RUSHWA ikiingia kwenye Taasisi yeyote inatakiwa iwekwe wazi Taasisi ikifanya RUSHWA kuwa ndio siri hiyo Taasisi INAOZA.

Style ya Lissu ya UWAZI ndio tunayoitaka Magufuli mwenyewe alipewa za Uso ndio ije Mbowe na wala RUSHWA wake.

CHADEMA kama taasisi kama imeamua kuhalisha RUSHWA nayo INAOZA mbele ya macho yetu.

Corruption can severely damage institutions by eroding trust, undermining their effectiveness, and compromising their integrity.
 
Habari ya kukataa kugombea uenyekiti ni ya lini, wakati ashachukua fomu ya kugombea kitambo kabla ya Mbowe?

Mbona kama mnatulisha matango pori nyie?
 
..mimi kwa mtizamo wangu nadhani kura alizopata Lowassa zilitokana na jasho la wanachadema wenyewe, wakiongozwa na Dr.Slaa.

NB.

..Lazaro Nyalanda alishindwa na Tundu Lissu hilo halihitaji mjadala.
Lowassa alikuja na constituency yake. Kama Slaa alihusika katika kampeni za Lowassa kwa nini alihamia upande wa pili?

Kila kitu kinaweza kujadiliwa. Nyalandu anadai aliibiwa na kuna watu wanaweza kumuamini. Shida ninayoiona mimi ni kuwa wengi hamko tayari hata uwezekano wa Lissu kushindwa. Hivyo Mbowe akimshinda mtasema ameibiwa hata kama uchaguzi utakuwa wa wazi kama mnavyotaka uwe. Hiyo sio demokrasi.

Amandla...
 
Ameufanya kwa mihemuko sasa anaenda kuaibishwa
Hawezi kuaibishwa. Angemkacha Lissu ndio angeaibishwa. Unadhani Mbowe angesema ameamua kustaafu ndio wangeacha kumtupia madogo. Tofauti ni kuwa wangemuongezea sifa ya kuwa coward.

Mbowe ashinde au ashindwe hatakuwa na kitu chochote cha kuonea aibu. Siku historia ya nchi hii itakapoandikwa atakuwa na nafasi yake ambayo wewe na mimi hatutakuwa nayo.

Amandla...
 
Sio" kumkacha" Mbowe angelionesha ukomavu wa kisiasa kwa kusema "20yrs Imetosha" tungemheshimu sana.
Mlianza kumsakama hata kabla hajasema lolote kuhusu kugombea. Na angesema "inatosha" mngetamba sana huku kuwa mmemlazimisha kubadilisha mipango yake ya kugombea.

Mimi nangojea tu wimbo mtakayokuwa mnaimba mwaka kesho kama mtu wenu atashinda.

Amandla...
 
..mimi kwa mtizamo wangu naona Chadema ndio ilimbeba Lowassa, na si vinginevyo.

..Lowassa alikuwa mgonjwa na kampeni zilikuwa za kumsitiri asionekane alivyodhoofika.

..Na nilivyokuwa naangalia kampeni zile nilikuwa naona jinsi Lowassa, na Chadema, walivyokuwa wakipoteza mvuto na kura kadiri muda ulivyokuwa unakwenda.

..Kikubwa zaidi, uwepo wa Lowassa katika Chadema ulikinyima chama kauli dhabiti dhidi ya ufisadi, ambayo ndio ilikuwa hoja kuu katika kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi.

NB:

..Nafahamu kwamba Tundu Lissu anaweza kushindwa ktk uchaguzi wa Mwenyekiti.

..Na kwa maoni yangu akishindwa chama kitakuwa kimepungukiwa mtu muhimu katika harakati za kudai Katiba mpya.

..Dr.Slaa alipoondoka watu wengi walivunjika moyo na Chadema. Sasa chama kinakwenda kumtoa na Tundu Lissu.

..Nasikitika kusema kwamba Chadema inajimaliza yenyewe.
 
Mimi nangojea tu wimbo mtakayokuwa mnaimba mwaka kesho kama mtu wenu atashinda.
Lissu akishinda ni siku ya mapumziko kwangu Konyagi na ubavu wa Mbuzi kama ile siku ya ushindi wa Mwabukusi.

Akikubali kushindwa nitampongeza ila asiwe tu yule aliyeshindwa kule TLS.
 
Lissu Mwenyekiti, Heche Makamu Mwenyekiti, Lemma Katibu Mkuu.
 
Lissu Mwenyekiti, Heche Makamu Mwenyekiti, Lemma Katibu Mkuu.
Lema kashakimbia nchi...yupo na ze wife wake anakula bata batani.

Heche kawakataza kumkashifu mwenyekiti Mbowe.

Lissu anakwenda TLP.
 
Lema kashakimbia nchi...yupo na ze wife wake anakula bata batani.

Heche kawakataza kumkashifu mwenyekiti Mbowe.

Lissu anakwenda TLP.
Lissu ndiye mwenyekiti ajaye,wamachame hamtaki kabisa ukweli huu.
 
..mimi kwa mtizamo wangu naona Chadema ndio ilimbeba Lowassa, na si vinginevyo.
Huo ni mtizamo wako. Mimi siamini kama Chadema ingemsimamisha Slaa ingepata mafanikio waliyopata walipomsimamisha Lowassa. Nakubali kuwa nae Lowassa alisaidiwa kwa kupata platform ya kugombea. Wote walifaidika ingawa Lowassa aliumia zaidi kwa sababu alitaka sana awe rais.
..Lowassa alikuwa mgonjwa na kampeni zilikuwa za kumsitiri asionekane alivyodhoofika.

..Na nilivyokuwa naangalia kampeni zile nilikuwa naona jinsi Lowassa, na Chadema, walivyokuwa wakipoteza mvuto na kura kadiri muda ulivyokuwa unakwenda.
Inawezekana uko sahihi. Lakini kama nilivyosema, Lowassa alikuwa na extensive network nchini ya watu waliomkubali toka alipokuwa Waziri Mkuu. Kulikuwa na watu wengi tuu CCM ambao waliamini kuwa alionewa kwa kunyimwa nafasi ya kugombea urais. Watu hawa hata siku moja wasingeweza kumpigia debe na hatimae kumpigia kura Slaa lakini kwa Lowassa waliweza.
..Kikubwa zaidi, uwepo wa Lowassa katika Chadema ulikinyima chama kauli dhabiti dhidi ya ufisadi, ambayo ndio ilikuwa hoja kuu katika kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi.
Hoja ya ufisadi kweli ilikuwa hoja kuu lakini sidhani kama wananchi wengi wa kawaida waliijali sana. Ni kama vile humu ndani watu wamepiga kelele sana kuhusu kuuzwa kwa Bandari lakini mwananchi wa kawaida anachotaka kujua ni kuhusu kula yake ya kesho. Bread and butter issues kwa maneno mengine.
NB:

..Nafahamu kwamba Tundu Lissu anaweza kushindwa ktk uchaguzi wa Mwenyekiti.

..Na kwa maoni yangu akishindwa chama kitakuwa kimepungukiwa mtu muhimu katika harakati za kudai Katiba mpya.
Kwani ataachana na hizo harakati akishindwa kwenye uchaguzi? Yaani hawezi kuchangia asipokuwa Mwenyekiti? Hata kama Heche atamrithi nafasi ya Makamu Mwenyekiti? Hapa si atakuwa ameweka mbele ego yake?
..Dr.Slaa alipoondoka watu wengi walivunjika moyo na Chadema. Sasa chama kinakwenda kumtoa na Tundu Lissu.
Tundu Lissu atajitoa mwenyewe. Kwa hulka ya Mbowe ya pragmatism, kama atashinda atajaribu kumtumia kikamilifu. Lissu ni tofauti. Akishindwa anaweza kususa. Akishinda anaweza kuwa mtu wa visasi. Si umemsikia leo anahoji utajiri wa Mbowe! Leo anaweza kudai kuwa biashara za Mbowe hazina TIN number? Sitashangaa kama kesho atadai kuwa Mbowe hakuwemo hata katika ndege iliyompeleka Nairobi! Aliisha anza kwa kudai kuwa ni Msigwa ndie aliyeshika chupa ya drip sio Mbowe. Kinachofuata ni kumshushia mzigo wa kuhusika kwa watu wa Chadema kuuawa, kupotea na yeye kupigwa risasi. Amaisha muingiza kinamna Marehemu Kibao. Lissu sio huyo mnaemdhania kuwa atawafikisha katika nchi ya ahadi.
..Nasikitika kusema kwamba Chadema inajimaliza yenyewe.

Nasikitika kuwa Lissu amechangia sana kwenye hili. Historia itamhukumu vibaya.

Amandla...
 
Lissu akishinda ni siku ya mapumziko kwangu Konyagi na ubavu wa Mbuzi kama ile siku ya ushindi wa Mwabukusi.

Akikubali kushindwa nitampongeza ila asiwe tu yule aliyeshindwa kule TLS.
Itakuwa jambo jema ikiwa hivyo. Ila mimi simuoni kama ni mtu atayekubali kushindwa maana tayari anapanda mbegu za kuhoji uhalali wa uchaguzi.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…