Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Amesema Leo, mbowe alikua anamzunguka akaona ngoja akambili. Kuthibitisha hayo mbowe alifanya umafia mkubwa sana kupitisha wenyeviti wa Kanda ambao anawataka yeye na kuondoa wote waliokua karibu na lissu. Kamshughulikia heche Kanda ya Victoria, kamshughulikia lema Kanda ya kaskazini, kamshughulikia msigwa Kanda ya nyanda za juu, n.k
Mbowe tatizo hujifanya mtoto wa mjini ,sasa amekutana na watoto wa mjini tena dam mpya
 
Taaisi yoyote Duniani ina kitu kinaitwa Siri - sasa kama ni mkutano wa siri wewe unaanza kubwabwaja hadharani ili tukujuie wewe ni mkweli sana ama? Upo wapi uugwana wako?

Je unabakizaje sifa za kuwa kiongozi bora, Leo umetoa siri za mkutano wako na Mbowe na viongozi wa dini kesho utatoa za kamati kuu CDM na kesho kutwa utatoa za nchi.
Hata Serikali ina mambo ya siri ambayo hata ukifukuzwa hutakiwi kuita press na kuanza kubwabwaja, yanabakia yako ili kuilinda taasisi.
Usifikiri unamshambulia Mbowe, unaishambukia Taasisi mzima, yaani nyumba unayotegemea kuishi unaipopoa mawe.

CDM angalieni sana hii kitu.
Hapa kuna siri gani ,kukaa na kusuruhishwa nayo ni siri tena katika kugombea nafasi ya urais au uwenyekiti ?
Neno siri litumike vizuri vinginezo itaonesha akili zimefungiwa kwenye kabati.

Nakubali zipo siri ila sio ujinga ujinga wa namna hii.

Mbowe akatubu alichofanya sio sahii
 
Back
Top Bottom