Pre GE2025 Lissu: Mbowe ni muongo, tulifanya kikao cha siri kwa siku 3. Alikataa nisigombee Urais na Uenyekiti huku yeye akisema hajaamua

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lengo la pesa za Abdul na Mama yake ni kwamba kusiwepo mgombea wa urais na mama apite bila kupingwa na yeye atawachia kupingana fair kwenye ubunge ila urais mama apite bila kupingwa hilo deal Mbowe amekubali ila tatizo ni huyu Lissu. Na kwasababu Mbowe kala dili kuna uwezekano Lissu akafukuzwa uanachama au akubali akagombee Ubunge na umakamu Mwenyekiti. Mama anamwogopa sana Lissu, Mama anajua watamwibia lissu , lakina mama anataka kupita njia nyepesi.
 
Amesema Leo, mbowe alikua anamzunguka akaona ngoja akambili. Kuthibitisha hayo mbowe alifanya umafia mkubwa sana kupitisha wenyeviti wa Kanda ambao anawataka yeye na kuondoa wote waliokua karibu na lissu. Kamshughulikia heche Kanda ya Victoria, kamshughulikia lema Kanda ya kaskazini, kamshughulikia msigwa Kanda ya nyanda za juu, n.k
 
Kumbe naye Lissu kabadilika kama alivyobadilika Mwenyekiti wake! Mabadiliko yaendelee CHADEMA wapate Mwenyekiti mpya
 
..labda ni biashara kwa maana wenye pesa zao wanafika dau?

..kwamba wanachadema wanateseka kupigania na kujenga chama halafu analetwa mtu mwenye dau kubwa ananunua nafasi ya kugombea Uraisi?
Kama ni hivyo basi lazima kutakuwa na mnada wa nafasi ya kugombea urais. Kama aliweza kuiuza kwa Lowassa basi hata Lissu aliuziwa. Na inawezekana kweli maana inasemekana Nyalandu alishinda lakini nafasi hiyo akapewa Lissu. Dau la Lissu lazima lilikuwa kubwa sana maana Nyalandu alikuwa na uwezo mkubwa wa kipesa. Na kama kugombea uenyekiti unauzwa basi nafasi zote za uongozi CDM zinapatikana kulingana na dau lililopo mezani! Wagombea ubunge, udiwani, n.k. wote wananunua haki hiyo.

Lowassa alipokelewa kwa strategic reasons. Idadi kubwa ya wabunge walioingia bungeni iliipa CDM nafasi ya kuwa kambi rasmi ya upinzani na Lissu kuwa Chief Whip. Kura walizopata wagombea wa CDM ndio zilikifanya kuweza kujijenga kiasi ya kuwa tishio kubwa kwa serikali na chama tawala. Kibaya zaidi ni kuwa aliyetarajiwa kugombea alitimkia upande wa pili na alitumika vizuri tu kuichafua CDM. Fikiria ingekuwaje kama Slaa angeunga mkono juhudi wa uchaguzi.

Hivyo kama Mbowe alinunuliwa na Lowassa basi chama chake kilifaidika sana.

Amandla..
 
CHADEMA imepasuka mapande mawili,
 

..mimi kwa mtizamo wangu nadhani kura alizopata Lowassa zilitokana na jasho la wanachadema wenyewe, wakiongozwa na Dr.Slaa.

NB.

..Lazaro Nyalanda alishindwa na Tundu Lissu hilo halihitaji mjadala.
 
Busara na hekima vitumike kuna maisha baada ya uchaguzi.
 
Watu wanasema lisu mropokaji, hana siri, ninachojua mm Lisu kwanza huwa wanamchokoza, akiwajibu wanasema hana siri, lakin pia Lisu anasiri nyingi sana, za chadema na ccm , kwa sbb ya exposure yake, tar 18 kuelekea uchaguzi anasema mengi sana Juu ya Mbowe hamtaamini kabisa, ngoja tusubili
 
Kwa kauli hii ina maana Mbowe alikuwa anatafuta mgombea Urais nje ya Chadema kama alivyotuletea Lowasa 2015. Lissu gombea uenyekiti na Urais pia tutakupa kupeperusha bendera yetu. Mwache Sultan ajipindue pindue
 
Wandugu aliyekaribu na Mbowe amshauri amuachie Lisu. Hizi aibu za reja reja si sawa kabisa
Amuachie lissu Nini 😂😂,
Kwa mambo yalivyo ivi mbowe watamuua tu,hamuachi Iko kit lisu hata akishinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…