Uchaguzi 2020 Lissu: Mimi sio wa kwanza kuwa na wakili Muingereza

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA amesema yeye sio wa kwanza kumtumia mwanasheria au wakili ambaye ni raia wa Uingereza.

Amejibu hivyo alipoulizwa kuhusu kutumia watu wa nje kwa masuala ya ndani. Suala hilo amesema kuwa hata mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliposhitakiwa na wakoloni alitafuta wakili wa Kiingereza.

Pia amesema hata aliyekuwa Rais wa Kenya, Jomo Kenyatta aliposhtakiwa kwa kesi ya MAUMAU pia alitafuta wakili wa kiingereza.

Alijieleza hivyo alipoulizwa na muandishi wa BBC Swahili kuhusu kuonekana kwake anajihusisha na ‘mabeberu’ kwa kuwa na hata wakili wake ni wa kutoka nchi ya kigeni.
 
Lissu.jpg
 
Nadhani Jomo Kenyatta kwenye kesi yake ya maumau maarufu kama The Kapenguria 6..., walitetewa na wakili wa kwanza raia wa Kenya mjaluo aliyesomea sheria huko Uingereza anaitwa Argwings Kodhek.
 
Lissu asitake kutufanya kuwa Watanzania wote anatuzidi akili hivyo kutaka tumuamini kila anachokiongea Ni sahihi.

Hivi tukirudi Nyuma wakati wa vita ya MAUMAU Ni mkenya yupi alikuwa amepata access ya kusomea sheria?

Wakati wa kupigania Uhuru Tanzania Ni Mtanzania yupi alikuwa ashapata access ya kusomea sheria mbele ya shule na vyuo vya mkoloni?

Nikweli lissu hajui kuwa wakati huo elimu, Afya na huduma zingine zilitolewa kwa upendeleo wa rangi.
Ni mkoloni yupi alikuwa tayari kumufunza muafrika Sheria ili adai haki yake?

Kwanini TL kashindwa kutolea mifano ya maisha ya kisasa ambayo Kenya na Tanzania imejaa mawakili wasoni akiwemo na yeye?.

Hoja ya TL ningeiona Ina mashiko zaidi Kama mifano yake ingejikita kwenye kipindi Cha Leo na Wala siyo hicho Cha Vita vya MAUMAU.

Mwisho; Ni dhahili kuwa Kuna kila dalili za tundu lissu kutumika na watu wanaosadikika Ni mabeberu kutoka ughaibuni, hii nikutokana na style aliyorudi nayo nchini mwake pamoja na kupenda kuandika kingereza Sana katika account zake za kijamii(twiter) huku Akitag Majina ya watu wa nje angali yeye kwa kinywa chake alisema Watanzania wengi hawajui kingereza.

Zimebaki siku5 tu Watanzania tunaojielewa tutenganishe ngano na magugu.
 
Wakati Mwl Nyerere na Mzee kenyata walipokuwa wanatumia hao mawakili wa nje kwenye nchi zao yaani Tz na Kenya kulikuwa na mawakili huru? Janja ya Lisu huwa anatumia historia badala ya current situation ,nakumbuka Rais wa marekani bwana Bush aliulizwa sababu ya kuvamia Iraq yeye akajibu kuwa marekani siyo nchi ya kwanza kuvamia nchi nyingine hata Tanzania ilivamia Uganda
 
Lissu asitake kutufanya kuwa Watanzania wote anatuzidi akili hivyo kutaka tumuamini kila anachokiongea Ni sahihi.
Hivi tukirudi Nyuma wakati wa vita ya MAUMAU Ni mkenya yupi alikuwa amepata access ya kusomea sheria?
Wakati wa kupigania Uhuru Tanzania Ni Mtanzania yupi alikuwa ashapata access ya kusomea sheria mbele ya shule na vyuo vya mkoloni?

Nikweli lissu hajui kuwa wakati huo elimu, Afya na huduma zingine zilitolewa kwa upendeleo wa rangi.
Ni mkoloni yupi alikuwa tayari kumufunza muafrika Sheria ili adai haki yake?

Kwanini TL kashindwa kutolea mifano ya maisha ya kisasa ambayo Kenya na Tanzania imejaa mawakili wasoni akiwemo na yeye?.

Hoja ya TL ningeiona Ina mashiko zaidi Kama mifano yake ingejikita kwenye kipindi Cha Leo na Wala siyo hicho Cha Vita vya MAUMAU.

Mwisho; Ni dhahili kuwa Kuna kila dalili za tundu lissu kutumika na watu wanaosadikika Ni mabeberu kutoka ughaibuni, hii nikutokana na style aliyorudi nayo nchini mwake pamoja na kupenda kuandika kingereza Sana katika account zake za kijamii(twiter) huku Akitag Majina ya watu wa nje angali yeye kwa kinywa chake alisema Watanzania wengi hawajui kingereza.

Zimebaki siku5 tu Watanzania tunaojielewa tutenganishe ngano na magugu.

..kwani Mwalimu Nyerere alichukua Mawakili wa Kizungu kwasababu hakukuwa na Mawakili wa Kiafrika / Kitanganyika?

..Au, Mwalimu Nyerere alijali competence ya wakili ktk kumtetea kutokana na shauri lililokuwa mbele yake?

..Badala ya kumlaumu Tundu Lissu, tunapaswa tujiulize hapa Tanzania kuna tatizo gani mpaka alazimike kuchukua wakili toka nje ya nchi?

..Siasa zetu zimekuwa mbaya, za kikatili, na kuumizana, na ndiyo maana leo hii Tundu Lissu ni mlemavu na amelazimika kutafuta mawakili wa kumtetea toka nje ya nchi.
 
Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA amesema yeye sio wa kwanza kumtumia mwanasheria au wakili ambaye ni raia wa Uingereza.

Amejibu hivyo alipoulizwa kuhusu kutumia watu wa nje kwa masuala ya ndani. Suala hilo amesema kuwa hata mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliposhitakiwa na wakoloni alitafuta wakili wa Kiingereza.

Pia amesema hata aliyekuwa Rais wa Kenya, Jomo Kenyatta aliposhtakiwa kwa kesi ya MAUMAU pia alitafuta wakili wa kiingereza.

Alijieleza hivyo alipoulizwa na muandishi wa BBC Swahili kuhusu kuonekana kwake anajihusisha na ‘mabeberu’ kwa kuwa na hata wakili wake ni wa kutoka nchi ya kigeni.
28102020
 
Cha ajabu ni uwanja WA kimataifa WA Chato Tu mengine yote ni ya kawaida na yameshawahi kutokea.
... ha ha ha! Gbadolite kule kijijini alikozaliwa dikteta Mobutu Ssesseko Kuku wa Zabanga kuna magofu ya li-international airport fulani ambalo halikuwahi kutumika tangu lijengwe! Kwa hiyo naomba kupingana na wewe; precedence ipo!
 
Back
Top Bottom