Lissu asitake kutufanya kuwa Watanzania wote anatuzidi akili hivyo kutaka tumuamini kila anachokiongea Ni sahihi.
Hivi tukirudi Nyuma wakati wa vita ya MAUMAU Ni mkenya yupi alikuwa amepata access ya kusomea sheria?
Wakati wa kupigania Uhuru Tanzania Ni Mtanzania yupi alikuwa ashapata access ya kusomea sheria mbele ya shule na vyuo vya mkoloni?
Nikweli lissu hajui kuwa wakati huo elimu, Afya na huduma zingine zilitolewa kwa upendeleo wa rangi.
Ni mkoloni yupi alikuwa tayari kumufunza muafrika Sheria ili adai haki yake?
Kwanini TL kashindwa kutolea mifano ya maisha ya kisasa ambayo Kenya na Tanzania imejaa mawakili wasoni akiwemo na yeye?.
Hoja ya TL ningeiona Ina mashiko zaidi Kama mifano yake ingejikita kwenye kipindi Cha Leo na Wala siyo hicho Cha Vita vya MAUMAU.
Mwisho; Ni dhahili kuwa Kuna kila dalili za tundu lissu kutumika na watu wanaosadikika Ni mabeberu kutoka ughaibuni, hii nikutokana na style aliyorudi nayo nchini mwake pamoja na kupenda kuandika kingereza Sana katika account zake za kijamii(twiter) huku Akitag Majina ya watu wa nje angali yeye kwa kinywa chake alisema Watanzania wengi hawajui kingereza.
Zimebaki siku5 tu Watanzania tunaojielewa tutenganishe ngano na magugu.