Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewakamata watu wote waliokuwa ofisi za CHADEMA kanda ya Nyasa akiwemo Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu. John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda Joseph Mbilinyi (SUGU) pamoja na viongozi wa BAVICHA.
Pia soma: Jeshi la Polisi lapiga marufuku mkutano wa BAVICHA siku ya vijana duniani
Viongozi hao wamekamatwa mda mfupi baada ya kumaliza kikao cha ndani kwenye ofisi hizo pamoja na viongozi waandamizi wa Bavicha na waandishi wa Habari wa Jambo TV Online waliokuwa wamepiga kambi kwenye ofisi hizo nao wamekamatwa
Lissu aliongea na vyombo vya habari leo ambapo alisema;
Pia soma: Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
1. Kwa vile ofisi ya Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi Leo atazigeuza ofisi hizo kuwa darasa ameliita ni darasa la kufundisha juu ya ukombozi ,yaani Teach in Resistance.
Pia soma: Msajili apiga Marufuku Kongamano la CHADEMA mkoani Mbeya, asema matamko yao yanahusisha vitendo vya uvunjifu wa amani
2. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara Mh LISSU amesema atabaki hapo na ikibidi atalala hapo na amesema na yupo tayari kulala hapo na yeye amesema atakuwa Mwl wa kufundisha Hilo darasa la teach in Resistance. Ila kaomba iwepo namna ya kupasha joto mwili kwa sababu hali ya mbeya ni baridi,amewataka watu wakeshe pale.
3. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zimetekwa nyara basi wataanzia safari Yao kuelekea Ruanda nzovwe kwenye ofisi hizo za Kanda ya Nyasa
4. Kwa vile ofisi za Kanda ya Nyasa zipo mateka amesema wananchi na vijana wasikubali kutishika na Rais Samia, amesema yeye atabaki ofisini hapo kufundisha darasa la teach in Resistance waje wankamatie pale.