Lissu: Msigwa alienda kumsubiria Mwenyekiti Mahakama ya Kisutu alipoachiwa huru lakini hakumkuta, akashangaa kumuona kwenye TV yupo Ikulu

H
View attachment 3203344
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu anasema siku ambayo Freeman Mbowe anaachiwa huru Mchungaji Peter Msigwa alienda na wanachama wa CHADEMA kumsubiria katika Mahakama ya Kisutu lakini cha kushangaza hawakumuona na baadaye walishituka kumuona akiwa ikulu na Rais Samia. Tundu Lissu anasema baada ya Msigwa kuhoji imekuaje ameenda ikulu bila kuwafahamisha viongozi wengine na nini walichozungumza Mbowe aliaanza kumuona Msigwa kama adui na kushughulika naye hali iliyompelekea kuondoka CHADEMA.

Amesema hayo alipokuwa anahojiwa na Clouds TV
Hivi hii ni seheme ya kampeni ya kuwania Uwenyekiti?!
 
Hii ni kampeni ya kumsema vibaya mwenyekiti wao,na anaona hajafanya chochote.Ila Dunia ina watu waliokosa shukrani
 
Kwa hiyo ilikuwa ni kosa kwa Mbowe kuitikia wito wa Rais wa nchi.

Hakuna hoja hapo. Wajumbe kazi yenu ni moja tu kuyaondoa mazombi ndani ya chama chenu tarehe 21.
kosa lake kwani hakuwahusisha wanachama wenzake kuwa anamualiko na Mh Samia? hapa Mbowe ajeakanushe haya maelezo tumpe kura zetu.
 
View attachment 3203344
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu anasema siku ambayo Freeman Mbowe anaachiwa huru Mchungaji Peter Msigwa alienda na wanachama wa CHADEMA kumsubiria katika Mahakama ya Kisutu lakini cha kushangaza hawakumuona na baadaye walishituka kumuona akiwa ikulu na Rais Samia. Tundu Lissu anasema baada ya Msigwa kuhoji imekuaje ameenda ikulu bila kuwafahamisha viongozi wengine na nini walichozungumza Mbowe aliaanza kumuona Msigwa kama adui na kushughulika naye hali iliyompelekea kuondoka CHADEMA.

Amesema hayo alipokuwa anahojiwa na Clouds TV
Hii sio habari.

Kesi ya Mbowe ilikuwa mahakama kuu sio kisutu.

Pia sio kila kitu anachofanya mtu lazima awataarifu watu kabla hata Lisu kuna mambo anafanya lakini wapambe wake hawaambii kabla.

Otherwise one will be foolish if he/she reveals everything.
 
Kawaida Mtu huachiliwa pale mahakamani

Lisu ana pweinti 😂😂😂🔥
Kama aliachiwa Mahakamani, itakuwaje Umati wote wasimuone alivyoondoka? Au alipanda ungo kwenda Ikulu?
Na seriously Lissu anataka kutuaminisha kuwa chuki ya Mbowe kwa Msigwa ilitokana na Msigwa kumuuliza uliendaje vipi Ikulu bila kututaarifu? Kama ni hivyo Mbowe atakuwa ana ngozi nyembamba sana.
Lissu hapa anamtetea tu rafiki yake. Mbowe hawezi kuchukizwa kwa hilo swali tu. Labda kama liliambatana na shutuma za kuwa alienda kulamba asali.

Amandla...
 
Kwa hiyo ilikuwa ni kosa kwa Mbowe kuitikia wito wa Rais wa nchi.

Hakuna hoja hapo. Wajumbe kazi yenu ni moja tu kuyaondoa mazombi ndani ya chama chenu tarehe 21.
Mbowe alimtii kiongozi wake kama biblia inavyotutaka.....

Waebrania 13:17-24​

17 Watiini viongozi wenu na kufanya wanavyowaagiza. Wao wanachunga roho zenu, kama watu ambao watatoa ripoti ya huduma yao. Watiini kusudi wafanye kazi yao kwa furaha, na wala si kama mzigo, maana hiyo haitakuwa na faida kwenu.
 
Kwa hiyo ilikuwa ni kosa kwa Mbowe kuitikia wito wa Rais wa nchi.

Hakuna hoja hapo. Wajumbe kazi yenu ni moja tu kuyaondoa mazombi ndani ya chama chenu tarehe 21.
Kwani ni kosa au dhambi kuwafahamisha wanachama na viongozi wenzake kuhusu hicho kikao chake na Rais?
Agenda za kikao hicho zilihusu taasisi ya CHADEMA au mambo binafsi ya kifamilia?
 
Kwa nini huyo Msigwa na hao viherehere wengine walienda Kisutu tu siku huyo Mbowe anaachiwa huru na sio siku za nyuma wakati Mbowe bado hajaachiwa huru miezi yote 8 huko jela. Huo ni unafiki pasee. Halafu ni nani alishawahi kuitwa ikulu akakataa kwenda? Acheni nongwa za kijinga
kwani ni dhambi kuwajuza wanachama na viongozi wenzake kuhusu hicho kikao chake na Rais?
Je, agenda za kikao hicho zilihusu taasisi ya CHADEMA au mambo yake binafsi ya kifamilia?
Ikumbukwe kikao hicho ndicho kilicholeta maridhiano haya uchwara
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu anasema siku ambayo Freeman Mbowe anaachiwa huru Mchungaji Peter Msigwa alienda na wanachama wa CHADEMA kumsubiria katika Mahakama ya Kisutu lakini cha kushangaza hawakumuona na baadaye walishituka kumuona akiwa ikulu na Rais Samia.
Kuna vitu vingine inabidi Lissu aache kusikiliza kwa watu, maana kila kitu anaongea kutegemea alivyosimuliwa. Sasa wewe Msigwa hajafika mahakamani, waliofika wanapata habari kuwa kesi imefutwa, na wanaanza kushangilia. Sasa Msigwa alitaka Mbowe aendelee kumsubiri yeye mahakamani? Kwa nini hakuwapo tangu mwanzo?
Yaani niachiwe huru halafu nibaki mahakamani kumsubiri Msigwa wakati nina watu nje wanasubiri tufurahie uhuru? By the way, Msigwa yupo CCM

Kama aliachiwa Mahakamani, itakuwaje Umati wote wasimuone alivyoondoka? Au alipanda ungo kwenda Ikulu?
Na seriously Lissu anataka kutuaminisha kuwa chuki ya Mbowe kwa Msigwa ilitokana na Msigwa kumuuliza uliendaje vipi Ikulu bila kututaarifu? Kama ni hivyo Mbowe atakuwa ana ngozi nyembamba sana.
Lissu hapa anamtetea tu rafiki yake. Mbowe hawezi kuchukizwa kwa hilo swali tu. Labda kama liliambatana na shutuma za kuwa alienda kulamba asali.

Amandla...
Kwenye KESI ya Akwilina Mwenyekiti Mbowe alitolewa Jela Kwa kulipiwa faini na family ya Msigwa akiwemo Shujaa Magufuli 😂
 
Kwa hiyo ilikuwa ni kosa kwa Mbowe kuitikia wito wa mkuu wa nchi.

Hakuna hoja hapo. Wajumbe kazi yenu ni moja tu kuyaondoa mazombi ndani ya chama chenu tarehe 21.
"Tundu Lissu anasema baada ya Msigwa
kuhoji imekuaje ameenda Ikulu bila
kuwafahamisha viongozi wengine na nini
walichozungumza?"
 
Kwa hiyo ilikuwa ni kosa kwa Mbowe kuitikia wito wa mkuu wa nchi.

Hakuna hoja hapo. Wajumbe kazi yenu ni moja tu kuyaondoa mazombi ndani ya chama chenu tarehe 21.

..sio kosa Mbowe kwenda Ikulu.

..lakini alipaswa kwanza kwenda kwa wanachama na viongozi wenzake waliompigania mpaka akaachiwa.

..baada ya kukaa ya kupata baraka na nasaha za chama ndipo Mwenyekiti alipaswa kwenda Ikulu kuonana na Raisi.

..Mimi ningependa Mbowe atoke gerezani kwa maandamano mpaka Ufipa. Baada ya hapo ndipo angekwenda Ikulu.
 
Lissu alivyokutana na Mkuu wa nchi Belgium aliwajulisha wanachama kwanza ili wamruhusu kufanya hivyo.
Nani alimtuma Lissu kuongelea wafungwa wa kisiasa na maridhiano na mkuu wa nchi kwamba waachiwe?
Nani alimruhusu Lissu kumwomba Mkuu wa nchi malipo yake wakati sheria zipo wazi? Je ilishindikana vipi yeye Lissu kuja TZ kuwahamasisha wana CDM waandamane hadi Hazina kudai fidia za matibabu yake kama Seikali ilikuwa inasua sua kumfidia?
 
Nikiunganisha dot siku mwenyekiti anatoa hotuba kalewa baada ya maridhiano.
 
Lissu alivyokutana na Mkuu wa nchi Belgium aliwajulisha wanachama kwanza ili wamruhusu kufanya hivyo.
Nani alimtuma Lissu kuongelea wafungwa wa kisiasa na maridhiano na mkuu wa nchi kwamba waachiwe?
Nani alimruhusu Lissu kumwomba Mkuu wa nchi malipo yake wakati sheria zipo wazi? Je ilishindikana vipi yeye Lissu kuja TZ kuwahamasisha wana CDM waandamane hadi Hazina kudai fidia za matibabu yake kama Seikali ilikuwa inasua sua kumfidia?

..kabla ya Makamu wa Mwenyekiti Tundu Lissu kukutana na Raisi Ubelgiji aliwasiliana na Katibu Mkuu Mnyika na kukawa na mkakati wa pamoja wa chama kumuelekeza Makamu hoja za kuwasilisha kwa Raisi.
 
View attachment 3203344

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu anasema siku ambayo Freeman Mbowe anaachiwa huru Mchungaji Peter Msigwa alienda na wanachama wa CHADEMA kumsubiria katika Mahakama ya Kisutu lakini cha kushangaza hawakumuona na baadaye walishituka kumuona akiwa ikulu na Rais Samia. Tundu Lissu anasema baada ya Msigwa kuhoji imekuaje ameenda Ikulu bila kuwafahamisha viongozi wengine na nini walichozungumza Mbowe aliaanza kumuona Msigwa kama adui na kushughulika naye hali iliyompelekea kuondoka CHADEMA.

Amesema hayo alipokuwa anahojiwa na Clouds TV
Lissu huwa nyakati nyingine anazungumza very irrelevant things.
 
Back
Top Bottom