PreGE2025 Lissu na kauli mbiu ya “No Reforms, No Election” ni mipango ya Mungu au ya Shetani kutusambaratisha?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Anayekusambatisha ni binadamu mwenzio sababu ya greed aliyonayo ya kutawala wenzake na si vinginevyo
 
Si kwamba sijui. Najua. Nilichokataa na kuendelea kukataa ni kudai ni mpango wa Mungu. Hayo mengine hayakuibuliwa kwenye madai niliyojaribu kukanusha
Una register ya mipango ya Mungu tuipitie kama reference? Inaonekana unajua sana mipango ya muheshimiwa, hebu iweke hapa tujiridhishe kama huu haupo among the list
 
Mkuu Pasco, Natamani kupata maoni yako, No reform No election inazidi kuchanja mbuga kwa mtizamo wangu. Idadi kubwa ya watu wanazidi kung'amua kuwa ni rasmi wameporwa haki yao ya kuchagua kiongozi wanayemtaka. Nawaza Je kutakua na Reforms kabla ya uchaguzi? na kama uchaguzi ukifanyika bila Reforms? Je No Reform No election itaendelea au ndio itakua mwisho wake.
 
Mkuu paschal Malaya mkoloni mweusi hakupi uhuru mpaka uupiganie Kwa jasho na damu,
No reforms no election ⚒️ 💯
Tutakuwepo 😎
 
Kwa hivyo na wewe ni Mzee wa kukinukisha? Si kiongozi wenu aliapa kama hakuna reform atakinukisha . Sasa na Sisi tumeamiwa kukinukisha . Tunakujua side gani upo. Na VP inakuwa double face!
Karibu mitaa hii
P
 
.
 
Mkuu Pascal Mayalla kilichotokea design nikama huamini hivii 🤣🤣

Neno la kushika #Lissu siyo muumini wa machawa ,walau sasa utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuitumia taaluma yako kwa usahihi.
 

Tuliwaambia Machawa sasa toeni pin za location tuwatume vijana kuja kuwasalimu! Tumewaonya vya kutosha. Kuweni wanaume njooni tupambane sasa barabarani
 
Sometimes I don't think you are serious brother
Mkuu Mshana Jr , I'm very serious!, lile ni bandiko la kauli umba kumuumbia mema huyu mtu!.
Mtu mwema kabisa, ukimuita shetani, kama wewe una kauli umba, hiyo kauli inamuumbia ushetani na anageuka shetani kweli!, vivyo hivyo mtu akiwa ni shetani, ukimuita malaika, kama una nguvu ya kauli, kauli yako inamuumbia umalaika, hivyo shetani anageuka malaika!, Malaika akijiunga na mashetani, anageuka shetani? Shetani akijiunga na malaika anageuka malaika?!

Huu umalaika na ushetani kwenye nchi yetu upo!, mimi niliubaini mapema kabla na nikauandikia humu, PreGE2025 - Uchaguzi Wetu ni Umungu/Ushetani? Anayekinukisha kuuzuia Uchaguzi wa Kimungu ni Shetani, ila Kama ni wa Kishetani, anayeuzuia Afanya Kazi ya Mungu au?

Kilichotokea October 29, ni ushetani!, mkiendelea kuuhubiri huu ushetani, kesho kutwa tarehe 7, kama kuna vijana wetu ni vichaa, with nothing to loose, wanaweza kuingia kweli tena mtaani, hivyo msipo mnenea kauli njema za umalaika, shetani anaweza kuingia tena kazini, vijana wetu wakachinjwa kama wale 518!

Tumuumbie umalaika kwa kauli njema ili ageuke malaika, ule ushetani wa October 29, usijirudie.

P
 

Waandamanaji/wapinzani wasio na silaha hawawezi kushinda kwa nguvu dhidi ya dola yenye majeshi. Kwa hiyo hawalengi kushinda kimabavu, wanalenga kumfanya mtawala atumie nguvu kupita kiasi mbele ya mashahidi, ili nguvu hiyo ijigeuze dhidi yake.

Vijana wakitoka kwenye maandamano ya 7/7 lazima waandamae sehemu ambayo wataonekana, ili Watawala wakitumia nguvu, madhara lazima yaonekane na hadhira inayojali.

CCM wameamua kutumia Dola kubaki madarakani na siyo ridhaa ya wananchi, basi inabidi itolewe kwa njia mbadala.

CCM imechagua kutolewa kwa nguvu na si vinginevyo
 
Mwisho kabisa ningependa kukujulisha Lissu ni mpango wa Mungu kwa Watanganyika wengi tunaojitambua.
Mkuu Shemeji Tate, Tate Mkuu, asante kwa kunijulisha kuwa Lissu ni mpango wa Mungu.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…