Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Wanabodi,
Leo nimepata fursa ya kuifanyia PNA hotuba ya Rais Samia siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA ambayo yamekwenda sambamba na utoaji wa tuzo ya rais kwa mlipa kodi bora, ambayo ameitwa Mzee Saidi Salim Bakheresa
Kwa wasiojua PNA anzia hapa PNA: Makamo wa Rais Dr Nchimbi, atamsaidia sana Rais Samia na Taifa, Ni Mkweli Anayeweza Kumweleza Rais Ukweli!. Ili Kumsaidia Aomba Rais Aombewe!
Viongozi wetu ni binadamu na sio malaika, they are only human, na binadamu wote ni sawa, na wanamahitaji sawa ya kibinadamu, kula, kuishi na mwisho kwake kurejea.
Binadamu wote wana yale mahitaji ya kawaida ya binadamu, kuvuta hewa, kula, kunywa, shelter etc, binadamu wote wanastahili heshima kuheshimu utu wake, and all human beings wanafanya makosa, no one is perfect, hakuna mkamilifu, hivyo anaweza kukosea makosa ya kawaida ya kibinadamu, tusimfanyie nongwa!
Miongoni mwa mahitaji muhimu sana ya viumbe wote is to love and be loved!, akifanya vema apongezwe as encouragement aendelee kufanya mema, na akifanya makosa, akosolewe kwa heshima kwa kutumia lugha ya staha, kistaarabu na kiungwana, na ukosoaji wenyewe ufanywe constructively kwa nia njema ya kujenga, sio kuzodoa au kubagaza!,
Mimi mwenzenu, huyu mtu, nilimnote siku nyingi kabla, kwanza mimi ndiye mtu wa kwanza kumtambulisha humu jf, ilikuwa ni 2010 New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa! Kisha ni mimi nikaweka list ya high profile women wa Tanzania ambao ni presidential material, ni yeye alishika number 1!. Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?
Ile mwaka 2017 nilimzungumzia Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na kumshauri yule Blaza wangu, ampishe huyu Mama awamu yake ya pili.
Hivyo baada ya kutokea kile kilichotokea, na yeye kuwa rais wa Tanzania by default, kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, ni mimi tena nikawa lobby Watanzania, PreGE2025 - Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Hivyo nikawathibitishia kuwa Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
Baada ya kuwa rais kuna siku alisema mwenyewe, mkinizengua, tutazenguana!, hivyo hapo juzi kati kuna vijana wetu wakazengua, wakazenguliwa!. Nawaombeni vijana wetu, mistake kutuzengua tena!, msimtibue mkazenguliwa tena!.
Alianza vema, baada ya kuzenguliwa kuna wakati alikuwa kila akihutubia sisi wanahabari pia alitupa zetu kuwa waandishi wakimkuna, atawakuna vizuri, ila waandishi wapara, wakimpara, atawaparua!, mtu anayeparua ni yule mwenye makucha!, hivyo nikashauri Kauli ya Rais kwa waandishi 'Wapara' kuwa wakimpara "Atawaparua", Je Rais Samia ni katili?, Soma Jinsi ya kuwabaini makatili!. Ni kutumia macho tu!.
Baada ya kuwa rais wa JMT, ile humbleness yake aliyokuwa nayo mwanzo wakati akiwa VP, kama ilianza kutoweka toweka, nilimfanyia Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila... hata mimi nikaanza kujiuliza maswali Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?
But as times go by, she is changing for better, akifanya vema opongezwe as encouragement to encourage her to keep on doing better and better, kuna wakati hotuba zake zilikuwa ndefu, lakini hotuba yake juzi pale Mlimani City kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 30 ya TRA, is one of the best ya hotuba zake!, it is short, less than 20 min, it's clear & concise!, Big Up Sana for this!
Nimeifanyia PNA hotuba hiyo ila kwanza msikilize mwenyewe
View: https://youtu.be/KXN3XzMx69o?si=6zD9VjC1F5j2YyhL
Naanza na transcription
Kwa vile amezungumza mambo mengi, kwenye PNA yangu, nitachagua machache na kukuwekea
SSH = Samia Suluhu Hassan
PNA = PPR News Analysis
Kwa vile katiba yetu imetoa msamaha kwa baadhi ya viongozi kutolipa kodi kwenye mishahara yao, viongozi hawa, wanapohimiza watu walipe kodi, huku wao hawakatwi kodi, hii inakuwa ni just like paying lip services only, hivyo nimeshauri Kuepuka Double Standards ya Kodi, Nashauri Rais Uongezwe Mshahara, Ili Alipe Kodi, Wote Tulipe Kodi!
Kauli huumba, angalia jinsi kauli zinavyoumba
Sasa kufuatio kilichotokea, kimetokea, tusifute mema yake yote kwasababu ya tukio moja la October 29, no matter how bad, our situation was, mtu huyo huyo anayeongewa kwa ubaya, akibadilika na kufanya vema, apongezwe, ili kumu encourage aendelee kufanya mema, Mimi Pascal Mayalla Sipongezi Kutafuta Uteuzi Wowote!. Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine Kumtia Moyo Kwa Mazuri ya Kweli! hivyo nawaomba wana jf, tumnenee mema ili wema umvae!.
Hotuba fupi, short, clear and concise, are the best!
Big Up Sana!,
Paskali

Kisha nakuja kwenye PNA yangu kwanini hotuba hii ni one of the best!.Transcript
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi na utu >> TRA hoyee >> kwanza nami niungane na walionitangulia kusema kumshukuru Mwenyezi Mungu tujalie kukutana hapa leo katika siku hii muhimu ya maadhimisho ya safari ya miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania , pamoja na kutambua na kuenzi mchangowa lipa kodi katika maendeleo wa taifa letu.
Natoa shukrani za dhati kwa Waziri wa Fedha na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kunipa heshima ya kuwa mgeni rasmi katika shughulihii pamoja na kwamba inaitwa Tunzo ya Rais kufanywa tu na mgeni rasmi mwingine lakini mmenipa heshima hii, asanteni sana. Nakupongeza kamishna mkuu wa TR,Bodi, menej na watumishi wote wa mamlaka ya mapato Tanzania kwa maandalizi mazuri ya tukio hili.
Hakika shughuli hii imefana.Hongereni sana.Nitumie nafasi hii pia kutoa pongezi na shukrani zangu kwa walipa kodi wote nchini kwa uzalendo na ushirikiano wenu mnaoendelea kuutoa katika kutimiza wajibuwa kulipa kodi kwa hiari.Nawashukuru sana.Nyinyi ni sehemu muhimu ya safari hii ya mafanikio tunayoyadhimisha leo.Kwa namna ya kipekee niwapongeze sana walipa kodi bora waliotambuliwa na kutunukiwa tuzo ya rais kwa mwaka huu.
Hapa nawiwa kuwashukuru.Nawiwa kuwashukuru mamlaka ya mapato Tanzania kwa kukubali pendekezo langu la kukuza hadhi ya tuzo hizi zilizokuwa zikitolewa na mamlaka na sasa zinakuwa tuzoza rais.Wafanyabiashara wanaotekeleza wajibu wao wa kisheria na kizalendo wa kulipa kodi kwa uaminifu na kwa wakati wamejijengea heshima hii nami sikuwa na budi kuwapa
heshima hii.Tuzo hii inatolewa kwa mara ya kwanza ikiitwa tuzo ya rais kwa mlipaji kodi bora.Hivyo basi tunapowatunuku walipa kodi bora leo tunatuma ujumbe kwa walipa kodi wengine wote nchini kwamba serikali inatambua,inadhamini na kuheshimu mchango wenu katika kulijenga taifa letu.Ndugu viongozi na wananchi wenzangu, miaka 30 ya mamlaka ya mapato Tanzania imebeba safari ya mageuzi katika kujenga uwezo wa nchi kujitegemea.
Tumemsikia hapa kamishna ametueleza tulipoanzisha mamlaka hii miaka 30 iliyopita dhamira yetu haikuwa kukusanya kodi tu bali kuiwezesha serikali kujisimamia kiuendeshaji kwa mapato yakeya ndani ya nchi.Pamoja na kwamba tunapata mapato ya nje ya nchi lakini yale tunayoyakusanya ndani tuyasimamie wenyewe tufanye maamuzi wenyewe jinsi ya kujipangia matumizi.
Wenzetu katika nchi nyingine ndani ya bara hili la Afrika leo wanakusanya mapato ndani ya nchi na wanayapeleka kwenye benki kuu za nje yanchi kuwekewa mapato yale.Kwa Tanzania hilo halipo.Kwao tujipongeze.Safari hii ya miaka 30 imeakisi uwezo wetu kama nchi katika kujenga uchumi na kuimarisha huduma kwa wananchi.Pamoja na safari hii ya mafanikio bado hatujafika tunakokwenda.
Miongo hii mitatu ni kipindi kilichopita kimetupa uzoefu lakini kimetupa fursa kujitathmini.Kujipanga upya na kuimarisha zaidi taasisi yetu ya mamlaka ya mapato Tanzania.Uchumi wetu unakuwa kwa kasi, biashara zinazidi kufunguka na kwa namna hiyo hiyo mfumo wetu wa kodi hauna budi kubadilika kuendana na wakati tulionnao.
Tunahitaji mfumo wa kisasa unaotenda haki na unaoeleweka.Akumbuka kuwa mwezi Julai mwaka juzi 2024 tuli tume ya kufanya tathmini ya mfumo wa kodi nchini ambayo imetoa mapendekezo kadhaa ambayo yakitekelezwa tutaundamfumo unaohamasisha na kurahisisha ulipaji wa kodi na kuwafanya walipa kodi kutambua kwamba kulipa kodi ni wajibu,
Ni uzalendo na ni kutunza heshima ya taifa letu yaani kuelekea kwenye kujitegemea Taifa lolote ili liwe na nguvu ya kupanga,kuamua na kutekeleza mipango ya maendeleo yake halina budi kujenga mfumo imara wa kodi na mapato ya ndani kwenye ufanisi na unaoaminika.Na hivi ndivyo wenzetu walioendelea walivyofikia hatua ile.Sisi sote ni mashahidi wa mabadiliko na mwelekeo wa siasa za dunia kila kukicha.
Mabadiliko haya yanaathiri nyanja zote za maisha ikiwemo kushuka kwa uchumi kunakoonekana katika mataifa mengi duniani kwa wakati huu.Tunaishi katika zama za mataifa kukubaliana katika biashara na kwa kiasi kikubwa kupungua kwa misaada.Tunaishi kwenye zama za kuongezeka kwa mashati ya mikopo.Wakati huo huo kuna ongezeko la mahitaji ya wananchi.Kwa msingi huo hatuna budi kujenga uwezo wetu wa ndani kwa kuimarisha ukusanyaji wa mapato ili kujenga uchumi unaojitegemea kwa kiasi kikubwa.
Hatutaweza kwenda 100% kujitegemea lakini kwa kiasi kikubwa tunaweza kujitegemea kwa mapato yetu ya ndani.Kwa mantik hiyo kodi hizi tunazokusanya sambamba na vyanzo vingine vya mapato ya serikali ndizo zitazotuwezesha kuendelea kuendesha huduma za jamii na kwa kiasifulani kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.Katika mnasaba huo nadhubutu kusema kuwa kulipa kodi ni wajibu wa kila mmoja wetu katika kujenga taifa linalojitegemea.
Na hapa nataka nikubaliane na kauli mbiu ya tukio hili inayosema kulipa kodi ni uzalendo na ushujaa kwa maendeleo na kujitegemea kwa taifa letu.Ila uzalendo huu lazima uwe wa pande zote.Mwananchi au mfanyabiashara au mwekezaji alipe kodi kwa uaminifu.Mamlaka ya mapato ikusanye kwa haki na serikali itumie kodi hiyo kwa uadilifu.
Hapo ndipo kodi inakuwa ni nguzo imara ya maendeleo na kujitegemea kama ambavyo kauli mbio hii inatuambia.Kuna msemo unaosema imani huzaa imani.Hapa nataka nisitize kwamba mamlaka ya mapato Tanzania ikijenga imani na kumhudumia mlipa kodi kwa haki, heshima na weledi.Vivo hivyo itajenga imani ya mlipa kodi kwa TRA.Na serikali inapotumia kodi hizo kuwaletea maendeleo wananchi wake inajenga imani kwa wananchi hao kuendelea kulipa kodi.
Kwa hiyo imani huzaa imani.Ndugu viongozi na wananchi wenzangu tumemsikia kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania ndugu Yusuf Mwenda akiwasilisha mafanikio ya TRA hatua walizopiga katika kuongezamakusanyo na kupanua ugo wa walipa kodi na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa kodi nchini.Niseme kwa dhati tumepiga hatua kubwa na tujipongeze wote.
Kama alivyosema rais wa Zanzibar, sifa hizi zisitufanye tubweteke bali tuongeze nguvu katika ukusanyaji wa mapato na si nguvu ya kwenda kuwa nyanyasa nakutia harakati kwa wafanyabiashara nguvu ya maarifa na teknolojia,Weledi na uadilifu katika kusanya mapato.Tunapoanza utekelezaji wa dira ya maendeleo ya miaka 25 ijayo tujipange na utekelezaji wa mikakati itakaotuletea mfumo imara na endelevu wa ukusanyaji wa mapato
yetu nchini.Natamani sana tuwe na wigo mpana wa walipa kodi wazalendo na wanaojua wajibu wao.Natamani sana tukuze mifumo iliyorahisishwa na inayosomana ya ukusanyaji wa mapato nchini.Na natamani sana watendaji wetu wazidishe ueledi ubunifu na uadilifu.Hii itakuwa zawadi tosha mtakayonipa wakati nikimaliza muda wangu wa uongozi.
Nikiacha TRA yenye sifa hizi, mamlaka ya mapato yenye sifa hizi na inayokusanya kwa kiasi kikubwa kuelekea kujitegemea.Ndugu viongozi na wananchi wenzangu, kwa upande wetu serikali tutaendelea kujenga mazingira bora ya kufanya biashara ili tuweze kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wengi kutokanje na ndani ya nchi.Tutaendelea na hatua za kuzikuza na kuzirazimisha biashara ndogo na za kati ili kuongeza wigo wa walipa kodi.
Tutaendelea kuijengea uwezo mamlaka ya mapato Tanzania ili iweze kufanya kazi zake kwa umakini na ubora zaidi.Nimefurahi kusikia kuwa TRA inaanza utekelezaji wa mpango mkakati wa saba wa kuimarisha taasisi na kukuza tija.Nawapongeza kwa hatua hii.Rai yangu kwenu kwamba mpango huu usipimwe kwa ujenzi wa ofisi mpya za mamlaka ya mapato Tanzania nchi nzima au magari na makompyuta mtakayoyanunua
bali kwa matokeo yanayomgusa mlipa kodi.Vile vile mpimwe kwa ongezeko la mapato ya taifa letu.Tukifanikiwa na hayo tutajenga uwezo wa kutekeleza mipango yetu ya maendeleo kwa ustawi wa wananchi na taifa kwa ujumla.Ndugu wananchi wenzangu, napoendelea kusisitiza umuhimu wa kulipa kodi,natambua kwamba kulipa kodi ni uzalendo na heshima na kukwepa kodi ni usaliti na si jambo la fahari hata kidogo.
Hata dini zetu zinahimiza ulipaji wa kodi.Sio tu kama wajibu kwa mwananchi bali pia ni uungwana na tendo la imani.Wanasema kulipa kodi za saved duty as well as moral and spiritual obligation kwa wakristo mafundisho ya bwana yesu kwenye luka 2025 na matthew1727 yote yanahimiza waumini kulipa kodi pale inapohitajika kwa hiyo kwa waumini wa dini hii wende wakaangalie huko kwa waislamu hadithi iliyoelezwa na Ibn
Maja hadithi namba 1991 na Ibn Umar na bibi Aisha ni kwamba mtume Muhammad sallallahu alayhi wasallam alikuwa akichukuaDinari 20 au zaidi kutokana na mauzo ya mazao ya kilimo kuendana na aina ya kilimo mtu anachofanya kama ni kumwagilia au kusubiri mvua.Kwa hiyo alikuwa akichukua fedha kwa viwango tofauti kutokana na aina ya kilimo unayofanya.
Lakini matumizi ya fedha hizo yalikuwa ni kwa ajili ya matendo ya imani na kutimiza mahitaji ya jamii sawasawa na tunavyochukua kodi ni kutimizahuduma za jamii nchini lakini pia kujenga maendeleo ya nchi yetu.Vile vile katika sheria za kiislamu kumetajwa aina nne za kodi.Nazo ni kodi ya mali property tax.
Kodi ya maduka, kodi ya ardhi lakini pia kuna kodi ya kichwa ambapo hapa kwetu hatufanyi.Kilichosisitizwa zaidi kwenye dini zetu ni kutokuwa na kodi ya dhulma au dhuluma ya kodi.Kodi ya dhulma ni pale mamlaka ya mapato inapopiga kodi kubwa kwa mfanyabiashara bila kuzingatia uhalisia wa kodi anayotakiwa kulipa.Na dhuluma ya kodi ni pale mfanyabiashara anapodanganya makusudi ili asilipe kodi inayotakiwa.
Kwa hiyo tunakatazwa kodi ya dhuluma na dhuluma ya kodi.Yote yanakatazwa kwenye dini zetu.Ndugu zangu napoendelea kuhitimisha hotuba yangu niendelee tena kuwapongeza walipa kodi mliopokea tunzo ya rais leo.Hongereni sana.Ni imani yangu kwamba mtaendeleza uadilifu mliouonyesha na kwa wale ambao hawakupata tuzo leo tutarekebisha yale mapungufu machache yaliyopo na kuweza kuingia kwenye mkondo
wa akina mzee Bahresa mwakani.Aidha nirejee tena kuipongeza mamlaka ya mapato Tanzania na Watanzania wote kwa kutimiza miaka 30 ya huduma za ukusanyaji mapato yaliyotufikisha kiwango cha maendeleotulicho nacho leo.Wote tujipongeze na tuhong sana.Nawapongeza pia makamishna wakuu waliopita ndani ya mamlaka hii bodi management watumishi wote wa TRA wizara ya fedha na walipa kodi wote nchini.
Kila mmoja kwa nafasi yake amechangia kujenga taasisi hii na kuifanya iwe sehemu muhimu ya ujenzi wa taifa letu.Hata wale wanaokaidi kulipa kodi wamechangia ndani ya taasisi hii kwa sababu imewafanya sasa watafute mbinu za kuwafanya waweze kulipa kodi.Ingekuwa kila mtu analipa kodi yake kama inavyotakiwa wangerelax wasingezaa maarifa mengine haya ya teknoloji na mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa kodi.
Kwa dhati ya moyo wangu nashukuru kwa kunipatia tuzo inayotambua mchango wangu katika kuimarisha mifumo rafiki ya ulipaji kodi nchini.Kazi hii ni ya pamoja tumeifanya sisi wote kila mmoja kwa nafasi yake.Basi mafanikio haya pia tusharehekee kwa pamoja na tunzo ile ni tunzo ya Watanzania wote.La mwisho lakini sio kwa umuhimu naomba kila mmoja wetu aondoke na tafakari hii kuwa kodi si fedha inayotoka kwa wananchi kwenda kwa serikali
tu ni dhamana inayorudi kwa wananchi kupitia huduma na maendeleo.Tukilitambua hilo tutaona kwamba kulipa kodi ni kitendo cha kizalendo na kishujaa.Kusimamia ukusanyaji wa kodi kwa haki na uadilifu na matumizi sahihi ya kodi hizo za wananchi kutimiza wajibu wa hutimiza wajibu na kulinda maslahiya wananchi na kulikuza taifa.Kwa hiyo wote tuna wajibu wa kulipa kodi zetu.
Baada ya kusema hayo niwashukuru sana kwa kunisikiliza.Nawashukuru kwa kuhudhuria hafla hii.Na wale wanaotutazama kwenye vyombo vya habari.Nawashukuru pia kwa kuchukua muda wao kutuangalia au kufuatilia tukio hili.Miaka 30 ya mamlaka ya mapato Tanzania.Oye >> Mungu aibariki nchi yetu Tanzania Mungu aibariki mamlaka ya mapato Tanzania asanteni sana kwa kunisikiliza.>>
Kwa vile amezungumza mambo mengi, kwenye PNA yangu, nitachagua machache na kukuwekea
SSH = Samia Suluhu Hassan
PNA = PPR News Analysis
My Take:SSH: Hakika shughuli hii imefana.Hongereni sana.Nitumie nafasi hii pia kutoa pongezi na shukrani zangu kwa walipa kodi wote nchini kwa uzalendo na ushirikiano wenu mnaoendelea kuutoa katika kutimiza wajibuwa kulipa kodi kwa hiari.Nawashukuru sana.Nyinyi ni sehemu muhimu ya safari hii ya mafanikio tunayoyadhimisha leo.Kwa namna ya kipekee niwapongeze sana walipa kodi bora waliotambuliwa na kutunukiwa tuzo ya rais kwa mwaka huu.
PNA: Hapa amewashukuru walipa kodi, huku ni kuonyesha huyu ni mtu wa shukrani, ki kawaida kulipa kodi ni wajibu wa lazima, mtu hashukuriwi kwa kutimiza wajibu wake!, Baba hapongezwi kwa kuleta mkate nyumbani au kumlipia mtoto ada, huo ni wajibu wake!, sikumbuki kumsikia rais mwingine yeyote sio tuu akiwashukuru walipa kodi, bali huyu sio tuu amewashukuru, amewapa tuzo walipakodi bora, hivyo amewathamini sana na kuwaheshimisha sana.
Watu wa shukrani wakitaka kitu, wanaomba, na wakipewa huwa wanashukuru, baadhi ya makabila likiwemo kabila langu, kuna baadhi ya vitu kama ni mali yako mwenyewe, unajichukulia tuu, huombi anasema leta!, na ukipata husemi asante, nimewafundisha watu humu tuwe watu wa shukrani, tushukuru kwa yote, tukipata mema na mazuri, tushukuru, ila pia hata tukipata majanga, pia tushukuru!.
SSH: Hapa nawiwa kuwashukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kukubali pendekezo langu la kukuza hadhi ya tuzo hizi zilizokuwa zikitolewa na Mamlaka na sasa zinakuwa Tuzo za Rais. Wafanyabiashara wanaotekeleza wajibu wao wa kisheria na kizalendo wa kulipa kodi kwa uaminifu na kwa wakati wamejijengea heshima hii nami sikuwa na budi kuwapa heshima hii.Tuzo hii inatolewa kwa mara ya kwanza ikiitwa Tuzo ya Rais kwa Mlipaji Kodi bora hivyo basi tunapowatunuku walipa kodi bora leo tunatuma ujumbe kwa walipa kodi wengine wote nchini kwamba serikali inatambua,inadhamini na kuheshimu mchango wenu katika kulijenga taifa letu.
PNA: Kumbe kuanzishwa kwa Tuzo hizi ni Rais Samia mwenyewe ndie alipendekeza. Tuzo hizi zitawahamisha watu wengi zaidi wenye vipato vikubwa, nao pia waingie kwenye walipokodi bora, tutaishauri TRA, hizi tuzo za walipakodi bora, zishushwe chini ki sekta, unaweza kukuta, kwenye tasnia ya habari, kwenye kondi la waandishi wa habari wa kujitegemea, Pasco Mayalla, ndie anayeongoza kwa kulipa kodi nyingi, ukimshindfanisha na Bakhresa, ni kumuonea bure!, kuwepo na Tuzo za DC kwa mlipa kodi Bora, tuje Tuzo za RC kwa mlipa kodi Bora ndipo tuje kitaifa.
SSH: Tunahitaji mfumo wa kisasa unaotenda haki na unaoeleweka.Akumbuka kuwa mwezi Julai mwaka juzi 2024 tuli tume ya kufanya tathmini ya mfumo wa kodi nchini ambayo imetoa mapendekezo kadhaa ambayo yakitekelezwa tutaundamfumo unaohamasisha na kurahisisha ulipaji wa kodi na kuwafanya walipa kodi kutambua kwamba kulipa kodi ni wajibu, ni uzalendo na ni kutunza heshima ya taifa letu yaani kuelekea kwenye kujitegemea
Na hapa nataka nikubaliane na kauli mbiu ya tukio hili inayosema kulipa kodi ni uzalendo na ushujaa kwa maendeleo na kujitegemea kwa taifa letu.Ila uzalendo huu lazima uwe wa pande zote.Mwananchi au mfanyabiashara au mwekezaji alipe kodi kwa uaminifu. Mamlaka ya mapato ikusanye kwa haki na serikali itumie kodi hiyo kwa uadilifu. Hapo ndipo kodi inakuwa ni nguzo imara ya maendeleo na kujitegemea kama ambavyo kauli mbio hii inatuambia.Kuna msemo unaosema imani huzaa imani.Hapa nataka nisitize kwamba mamlaka ya mapato Tanzania ikijenga imani na kumhudumia mlipa kodi kwa haki, heshima na weledi, vivyo hivyo itajenga imani ya mlipa kodi kwa TRA, na serikali inapotumia kodi hizo kuwaletea maendeleo wananchi wake inajenga imani kwa wananchi hao kuendelea kulipa kodi. Kwa hiyo imani huzaa imani.
PNA: Hapa rais amezungumzia jambo kubwa la kuihusianisha kodi na mambo ya imani, jambo ukiliamini unalifanya kwa moyo mkunjufu.
SSH: Ndugu wananchi wenzangu, napoendelea kusisitiza umuhimu wa kulipa kodi,natambua kwamba kulipa kodi ni uzalendo na heshima na kukwepa kodi ni usaliti na si jambo la fahari hata kidogo. Hata dini zetu zinahimiza ulipaji wa kodi.Sio tu kama wajibu kwa mwananchi bali pia ni uungwana na tendo la imani.Wanasema kulipa kodi za saved duty as well as moral and spiritual obligation kwa wakristo mafundisho ya bwana yesu kwenye luka 2025 na matthew1727 yote yanahimiza waumini kulipa kodi pale inapohitajika kwa hiyo kwa waumini wa dini hii wende wakaangalie huko
SSH: kwa waislamu hadithi iliyoelezwa na Ibn Maja hadithi namba 1991 na Ibn Umar na bibi Aisha ni kwamba mtume Muhammad sallallahu alayhi wasallam alikuwa akichukuaDinari 20 au zaidi kutokana na mauzo ya mazao ya kilimo kuendana na aina ya kilimo mtu anachofanya kama ni kumwagilia au kusubiri mvua.Kwa hiyo alikuwa akichukua fedha kwa viwango tofauti kutokana na aina ya kilimo unayofanya.
PNA: Nimependa jinsi Rais Samia alivyohusianisha kulipa kodi na imani za dini, hiki alichokisema Rais Samia hapa, mimi nilitangulia kukisema humu, TRA Yatimiza Miaka 30 ya Mafanikio!, Je Wajua Kutolipa Kodi ni Dhambi?. Mpeni Kaizari, Yaliyo ya Kaizari ni Kodi!. WaTZ Tulipe Kodi
Injili ya Mt. Luka 20:25 "Kuhusu Kulipa Kodi
20 Kwa hiyo wakawa wanamvizia. Wakawatuma wapelelezi waliojifanya kuwa wana nia njema ya kujifunza. Walitumaini kumtega kwa maswali ili wamkamate kwa lo lote atakalosema, walitumie kumshtaki kwa Gavana. 21 Wale wapelelezi wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua kwamba maneno yako na mafundisho yako ni ya haki, kwamba huna upendeleo, na kwamba unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. 22 Je, sheria ya Musa inaturuhusu au haituruhusu kulipa kodi kwa Kaisari?”
23 Lakini Yesu akatambua kwamba wanamtega, kwa hiyo akawaambia, “Nionyesheni sarafu ya fedha. Je, picha hii na maandishi haya ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” 25 Aka waambia, “Basi, mpeni Kaisari vilivyo vyake na mpeni Mungu vilivyo vyake.”
Injili ya Mt. Matayo 17 27 "“Unaonaje Simoni’ wafalme wa ulimwengu hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Unadhani kutoka kwa jamaa zao au kutoka kwa wageni?” 26 Petro akamjibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akam wambia, “Kwa hiyo jamaa zao wamesamehewa. 27 Lakini ili tusi waudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemkamata; mfungue kinywa chake nawe utakuta fedha zinazo tosha kulipia kodi yangu na yako; ichukue ukawalipe.”
Mwisho wa PNA ya Hotuba.
Kwa vile katiba yetu imetoa msamaha kwa baadhi ya viongozi kutolipa kodi kwenye mishahara yao, viongozi hawa, wanapohimiza watu walipe kodi, huku wao hawakatwi kodi, hii inakuwa ni just like paying lip services only, hivyo nimeshauri Kuepuka Double Standards ya Kodi, Nashauri Rais Uongezwe Mshahara, Ili Alipe Kodi, Wote Tulipe Kodi!
Kauli huumba, angalia jinsi kauli zinavyoumba
Conclusion.Kauli huumba, enzi za yule Blaza wangu, mtu wa kwanza humu kumuita ni dikiteta, ni mimi, GE2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli Baada ya kuchaguliwa, nikaandika humu GE2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! ila pia nikasema kwa mahali nchi yetu ilipofika, Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba! bila mimi kujua, kumbe ni kauli kama hizi, zimechangia kumfanya Blaza kuwa dikiteta kweli.
Baada ya kugundua nguvu ya kauli umba, "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia, I changed the rethorics
Nikaanza kumnenea kauli njema, Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana! na Rais Magufuli, so far, is the best president this country has ever had. Msikivu, ana upendo na huruma. Atabarikiwa sana. Tanzania itabarikiwa! na "Mimi ni Mwenzenu Hapa, Sijabadilika ni Yule Yule "KaJoni" - Ni Maneno Simple, Humble and Down to Earth Yenye Maana Kubwa! amini usiamini, Blaza alibadilika na nikawahakikishia Watanzania Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya! by the time anakuja kutwaliwa, he was almost a saint!, na kwa vile ni Mkatoliki, ukipokea sekrament ya upako mtakatifu, dhambi zako zote zinafutwa, Blaza alipokea sacramenti hiyo, iliyotolewa na Paroko wa St. Peters, Fr. Makubi, hivyo kupokelewa moja kwa moja mbinguni!, hili mimi nilielezwa Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
The same applies to Rais Samia, kilichotokea October 29, kwa nchi yetu, ni kitu kibaya sana kuwahi kutokea, na kwa vile waliotenda yale sio Rais Samia, kwanza niliwasisitiza watu humu, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda, ila kwa vile baadhi ya watendaji ni wasaidizi wake, nilishauri Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe hivyo niliuliza The Voices From Within:Kilichotokea Oct. 29 Japo Anayeonekana ni Yeye Kumbe Si Yeye Kuna Watu Hawakutimiza Wajibu Wao Ndio Wamemponza, Tumsamehe Tuu?