Uchaguzi 2020 Lissu na Urais 2020: Fursa na Changamoto

Mmegeuka mnatoa miaka mitano, kimekufa imepotelea wapi?
 
Naona makada mnatifuana humu bila shaka hamjuani [emoji23][emoji23][emoji23]
MATAGA hata haeleweshani kabla ya kupost. Hii inatokana na Magufuli kuwa na roho ya aina hiyo ya visasi sasa TAGA limoja limemwandika Lissu huku TAGA lingine likikurupuka likajua aliyeandikwa ni Magufuli. Kumbe TAGA la kwanza linakiri kuwa Magufuli ndiye muhusika mkuu wa lile tukio hivyo linahofia kuwa Lissu ana kisasi naye.

Sasa nyie MATAGA hata kama ingekuwa ni wewe ungemchekea mtu aliyedhamiria kuutoa uhai wako? MATAGA hovyo kabisa takataka.
 
Akili zake ndiyo kikwazo kwake mkuu
 
Mlitaka kumtoa roho yake kisa anawakosoa bila kuwaogopa
 
Mungu ndie ajuaye dhamira yake na visasi vilivyomsonga moyoni mwake hawezi pata hata kura mil 2,atajuta na atakuwa amepotea kisiasa.
Mshaurini vizuri hatokuja kuamini!
Acha kumshirikisha Mungu kwenye mambo ya kipumbavu wewe. Kitu gani umemfanyia Lisu hadi uhisi kuwa anataka kulipiza kisasi? Kumbe mnajua kabisa kuwa mmefanyia matendo ya kinyama halafu baadae na nyingi mnaanza kujishtukia kuwa atalipiza kisasi!! Tendeni mema hata Mungu atakuwa pamoja nanyi badala ya kuwafanyia wenzenu unyama.
 
Uchambuzi wako uko vizuri kwakuwa na yeye lisu anapita humu atachukua anayopaswa kuyafanyia kazi ila lisu ndiye mwanasiasa pekee anayefaa kuwa rais kwa kipindi hiki ili arekebishe mifumo ya sheria na utawala
 
Kisasi gani na kwa nani?
Mbona wasiwasi ni mwingi wa kuogopa kulipizwa kisasi?...
Hujamtendea mtu kosa, unaogopaje kisasi...?
Huo wasiwasi mlionao inaonyesha ni kweli kabisa kuna maovu mengi mno yamefanywa, hasa lile la area d!
Watanzania tunafahamu jinsi mlivyomtendea Mh Lissu,lakini kuhusu hofu ya kisasi mliyonayo inatokana na nafsi zinavyowasuta.
Mh Lissu kwa jinsi ninavyomfahamu wala hana hiyo nia,ni mtenda haki na hivyo kama kuna wahalifu au uhalifu umetendeka atazingatia sheria za nchi.
 
Nimesema Mungu ndie anaejua dhamira ya huyo mtu!
Halaf hapo hao ukasema hatopata kura million mbili.
Na kwamba visasi vimejaa moyoni mwake.
Ok ww ndio Mungu kuwa unajua future ya huyo mtu na yaliyoko moyoni mwake? Au msemaji wa Mungu?
 
Mungu hapigi kura bali anatupa busara za kuchagua kiongozi bora wa nchi hii.
Na tayari tunae hadi 2025!
Mungu ndie anachagua kiongoz wa watu wake.
Anafanyaje mm sijui.. ni nani atamchagua sijui.
Ila ww kusema tayari tunaye? Sorry unaish na Mungu nyumba moja au umekuwa msemaji wake?
Na pia jisemee nafsi yako. Usiseme tunae.. sema unae ..hujui yaliyomo nafsini mwa watu wengine ila Mungu pekee ndie ajuae.
 
Kama Mungu ndiye anayejua Wewe hizo kura milioni mbili umezito wapi? Mbona unajichanganya?
Mwaka huu kitu kitakachowapiga kura watakuwa wachache sana hata milion tano hawatafika kwakuwa hakuna uhuru wa mawazo ukipendelea sana yanga mashabiki wa simba hawatajitokeza kadhalika na wayanga nao watahudhuria wachache mwisho mchezo hautanoga"
 
Mwaka huu kitu kitakachowapiga kura watakuwa wachache sana hata milion tano hawatafika kwakuwa hakuna uhuru wa mawazo ukipendelea sana yanga mashabiki wa simba hawatajitokeza kadhalika na wayanga nao watahudhuria wachache mwisho mchezo hautanoga"
Nipo hapa dukani nimekutana na mama mmoja mwana CCM anasema CCM ni chama chake lakini kwa wanayotenda safari hii hapigi kura
 

Asante sana nami nakubaliana nawe kabisa...

Na hiki kinachoitwa huyu ni "presidential material" na huyu siyo "presidential material" ni cha kushangaza kidogo...

Na maana ya hawa ni kuwa "all presidential material personnels" wapo na lazima watokane na CCM tu. Ndiyo hoja yao....

Huu ni upogo mwingine was kimawazo na hapa ndipo lilipo tatizo letu na kukwama kwetu kama taifa kwa kuwa na watu wenye mawazo na dhana hizi potofu na ndiyo wenye dhamana ya utawala na mamlaka kisiasa.....

Tangu Uhuru 1961 hadi leo (kama miaka 60 sasa) Tanzania imeongozwa na "the so called presidential material personnels" wanne na huyu aliyepo ni watano na wote toka chama kilekile - CCM...!

What did they do? How much did they do to change Tanzania from worse to better?

Kwa maoni yangu wamefanya kidogo sana. Tunaogelea mlemle. Tunaenda mbele hatua kumi na kurudi nyuma hatua 15. Kila aliyekuja alifuta mengi ya mwenzake na kuanzisha yake mapya. Yaani tunaanza moja tena...!

Hawa ambao tunaambiwa walikuwa ni "presidential materials" ni watu wa chama kilekile lakini hawana "connectivity" na "continuity" ya kilichoanza na huyu kiendelezwe na huyu. Vipi kama wakiwa toka vyama tofauti?

Likely, kuna hatari ya mambo kuwa mabaya zaidi. Ndiyo maana inahitajika mabadiliko ya mfumo mpya wa kisheria na kikatiba kuweka utaratibu usiobadilika wa mambo haya yasiwe hivi yalivyo....!

Tanzania kwa umri wa miaka 60 sasa ya uwepo wake kama taifa huru, hatukupaswa kuwa hapa tulipo kimaendeleo, KIJAMII na KIUCHUMI....

Hii Tanzania ya leo kama tukiifananisha na binadamu kwa umri wake wa miaka 60 maana yake huyu MTU kwa sasa eti ndo tu anaanza kujifunza kutembea badala awe ameshaoa, kuzaa na kupata na wajukuu.....!!

Maana yake na tafsiri yake ni kuwa, huyu mtu - mtoto lazima atakuwa ana tatizo la kiafya linalopaswa kushughulikiwa na madaktari bingwa hasa. Tanzania ina tatizo hili. Inahitaji kiongozi atakayeliona na kulishughulikia..!!

Tatizo la nchi yetu siyo MTU kuwa "presidential material" ama kutokuwa.....

Tatizo ni mfumo wetu wa kikatiba na kisheria ndiyo kikwazo cha kupiga hatua za haraka za maendeleo yetu ya kijamii na kiuchumi....

Tukikubali na kukaa pamoja kama taifa kufanya reforms za nguvu za kisheria na kikatiba, tutaona Tanzania mpya ktk kipindi kifupi sana...

Tundu Lissu ni mwanasheria kitaaluma. Magufuli ni mwalimu wa somo la Chemistry kitaaluma...

Tumeona akitumia taaluma yake ya ualimu wa Kemia na matokeo yake kila mtu anaona....

Hebu tuone Tundu Lissu kama atatumia taaluma yake ya sheria kutuletea mabadiliko ya mifumo ya kiutawala kisheria na kikatiba kwa ajili kufungua milango ya maendeleo ya taifa hili ambalo ni kama limesimama, limedumaa.....
 
Mungu ndie ajuaye dhamira yake na visasi vilivyomsonga moyoni mwake hawezi pata hata kura mil 2,atajuta na atakuwa amepotea kisiasa.
Mshaurini vizuri hatokuja kuamini!
Yaani huyu mheshimiwa Mungu amepanga agombee na matokeo yatampa picha halisi. Naamini anaenda potea rasmi ktk siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…