Uchaguzi 2020 Lissu na Urais 2020: Fursa na Changamoto

Mungu ndie ajuaye dhamira yake na visasi vilivyomsonga moyoni mwake hawezi pata hata kura mil 2,atajuta na atakuwa amepotea kisiasa.
Mshaurini vizuri hatokuja kuamini!
Unataka kusema,waliomuminia risasi 36 ni hawa hawa wanaojifanya wapenzi wa Mungu?
 
Umenena vema,hii ndiyo Great Thinking tunayoihitaji hapa.Natamani hizi nondo kungekuwa na namna ya kuwafikishia Watanzania wote ili watambue uhalisia.Watawala wanatuongopea,wakosoaji wanakiona cha moto na washangiliaji wakipew tuzo.
Jamii Forum fikirieni namna ya kutengeneza vipindi vya elimu kwa umma.Watu wetu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Lissu ni Presidential Material kwa vigezo vyovyote vile.Tuwape Watanzania wenyewe wataamua kama wanamhitaji au LA.Mengine ni porojo na hofu.
 
Nakubaliana na mtoa mada kwa upande mkubwa hasa strength za Lissu ila kwenye kuleta maendeleo jimboni napingana na wewe. Serikali ndo inaleta maendeleo na sio mbunge. Lissu kwa uzuri wake asingeweza kuleta maendeleo jimboni kwake vyovyote vile kwa sababu yeye ndo mkosoaji mkuu wa Serikali ya magufuli.

Niliwai kusema mahala kati ya kosa kubwa lililofaanywa katika awamu hii ya tano ni kujaribu kumuua Lissu. Kiukweli lile jambo limemjenga Lissu mara 100 kuliko kawaida. Vyovyote vile hata asingekuwa na hoja, kitendo tu cha kujaribu kuuawa ni mtaji mkubwa sana kisiasa kwa Lissu. Binadamu pamoja na uovu wao hawapendi sana mauaji hasa ya uonevu Ndo mana hata leo Marekani hapakaliki kwa sababu tu ya mauaji ya mtu mweusi George Floyd.

Lissu anasema I survived to tell the tale . Na ni kweli watu wengi sana watampenda Lissu si kwa sababu ya sera Nzuri Bali kwa sababu alipona jaribio baya la kuuawa.

CCM na Serikali hivi karibuni walikosa watu strategist wazuri hasa katika kupanga vizuri jinsi gani ya kukabiliana na hoja za wapinzani wao. Walitakiwa wamtulize magufuli na wapambane kisayansi zaidi. Walishindwa kufanya hivi na Ndo mana mwaka huu kuna uwezekano wakapata shida sana.
Mwaka 2015 CCM walipambana na adui mkubwa waliyemjua vizuri(Lowassa) ila mwaka huu CCM watapambana na adui mkubwa wasiyemjua vizuri(Lissu)

Hatari ya kupoteza mpambano kwa CCM kwa mwaka huu 2020 ni kubwa zaidi.
 
Hoja
Hoja uliyoileta inafikirisha zaidi.Sisi Watanzania kama wote kwa kutumia akili zetu,nguvu zetu na weledi wetu tukakubaliana kuwa tumekwama kwa sababu tunaongozwa kwa mifumo iliyokwama na kuanza upya tungeweza kusonga mbele kwa kasi kubwa.Ndiyo maana pamoja na raslimali lukuki bado nchi imekwama tunatumia nguvu nyingi bila matokeo chanya.
Hatuna Sera na agenda ya Kitaifa,tunatakiwa kutengeneza Katiba Mpya ambayo tutaweka Sera na Dira ya Taifa ambapo vyama au
wagombea watakuwa wanatuletea ilani/mikakati ya utekelezaji na tuweze kuwapima kila Mara,kama hawatoshi tunapiga kura watupishe.
 
Kuna maswali kidogo ya kumuuliza ndugu lissu je katika yale mambo aliyokuwa anautangazia uma kila mara kwenye nyaraka zake yametekelezwa
1. Mara kadhaa alisikika hawezi kurudi nchi hii mpaka ahakikishiwe usalama na serikali ya nchi hii kwa kuwa walitaka kumuua na ameihirisha mara kibao na hata kusamehe ubunge,sasa ameamua kurudi kuja kugombea uraisi kama atapitishwa na chama chake.

Je amehakikishiwa usalama na serikali au wale aliokuwa hana imani nao wote wameondolewa pamoja na serikali ya awamu ya tano!

2.Katiba mpya imepatikana,alisikika mara kadhaa katiba mpya ndio suluhu je imeshapatikana mpaka imempa msukumo wa kugombea si hii ya zamani

3.Tume huru,je kumeundwa tume huru itakayo muhakikishia yeye kushinda mara kadhaa amenukuliwa akisema tume hii kwa upinzani ni ndoto je kuna nyingine inayomuhakikishia yeye kushinda?.

Najua atachelewa kujibu ila ruksa kwa wafuasi watiifu kumjibia hapa sabuni imetiwa nyingi ili povu nalo liwe jingi!
 
Kuandaika tu tabu vijana wa hungumalwa bhana mkipata pakulia tu mnakuwa kama misukule
 
Kaka unataarifa na mswada was kuongeza Kinga zaidi kwa viongozi wa mihimili ya nchi??
Ushapata mda ukatafakari nn kipo nyuma yake??

Tuache siasa tuamke kuilinda nchi yet!
 
Ni hakika na kweli ndani ya ccm akiondoka mgombea wao huyu 2025 hawana mtu wa kushindana na Tundu Lissu zaidi ya Dr Slaa.

Kama yupo mtajeni

Najua ntatajiwa mtu kam simbachawene wingiru nchemba au Dr kigwangara au nani sasa?

Jipangeni chadema mbaya wenu hiyooo 2025.
 
Eti kuna mambo anakamilisha kisha aje kugombea,
Mi nadhani anatafuta mabeberu wamdhamini ili akipata uraisi awauzie nchi
Watu wataanza kutongozana wanaume kwa wanaume kama akishinda,
Ni mawazo tu. Ila hatashinda.
 
Typing errors kibao halafu unataka tujadili thread yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…