Uchaguzi 2020 Lissu na Urais 2020: Fursa na Changamoto

Uchaguzi 2020 Lissu na Urais 2020: Fursa na Changamoto

Mleta maada, ni lini Dr. Slaa alikutangazia kuwa kawa mwanachama wa ccm? Tatizo mods hawako strict na suala la umri. Kuna vitoto humu vinajaza servers.
 
Kaka unataarifa na mswada was kuongeza Kinga zaidi kwa viongozi wa mihimili ya nchi??
Ushapata mda ukatafakari nn kipo nyuma yake??

Tuache siasa tuamke kuilinda nchi yet!
Inchi ipo salama usihofu na kwenye mikono salama!
 
CCM ni chama Cha siasa chenye kujenga watu na si kikundi cha upatu chenye kujengwa na watu kwa maslahi binafsi. Wenye sifa, uwezo na uzoefu wa uongozi CCM wapo wengi sana.

Tujiulize, mtu Kama Msingwa ambaye hajawahi kushika nafasi yoyote ya uongozi wa kitaifa, anafaa kushika nafasi ya urais ?
 
Humjui vizuri Zitto wewe, mwaka huu atawaachia sababu mjanja hataki aibu ya kupata chini ya 5% dhidi ya JPM, 2025 lazima mumuunge mkono la sivyo atasimama pekeake.
 
Akili za nyumbu wanazijua wenyewe. Tulizungushiwa mikono mwaka ule mpaka tukaamini Ccm inaondoka. Safari hii sijui mazingaombwe gani yanakuja.

Ila issue ya ushoga na corona zitakuwa mkuki balaaa.

Nchi hii watu wamejaa ubinafsi na kamwe hawajayaishi maneno yao.
 
Ina miaka zaidi ya kumi .Threats inataka ukimbie challenge unatakiwa kukabiliana nayo kilichobadikika Ni kuondoa threat na. Kuweka challenges kwa waliosoma zaman wanafanya SWOT analysis modern management inatumia SWOC analysis
Basi hapa kuna vyuo na vyuo mkuu,, nilikuwa chuo mwaka Jana tu na tulitumia hiyo unayosema imepitwa na wakati! Ajabu iliyoje hii?!!!
 
Yule anataka hela za ruzuku yq uchaguzi

Anataka ubunge wa kuteuliwa na chama chake

Anataka attention

Ila ashapotezewa na raia, achilia mbali watawala watakavyodeal nae

Alikojua kuna haki na justice wameua ngozi yetu nyeusi

Anaelea hewani!!! Technically kapoteza sana

Ataongea maneno yote mabovu, makali, ya hasira ili mradi awe kwenye headlines.Ila hataweza kamwe kufika ikulu


Miaka 5 ijayo kwake yeye na chama chake watapotea kabisa kwenye siasa, chukua hii kma ufunuo

Tatizo sio CCM, tatizo wamw betray raia wa kawaida kabisa, wako insta, twitter na fb...hawako kwenye mioyo ya watanzania ambayo wameshuhudia hawa jamaa wakisema tusideal na madini, wakiangalia mawazo yao kwenye covid-19 na wakitamani tusipate hata mikopo tu!!!!


Loosers hawa ukweli sio hata wa kuwawazia

Kuna mwenzako anapanga vina kama ww, alipiga mahesabu akaona kujidanganya hakulipi maana anajua fika Lissu ni game changer, na kura atapata za kutosha. Yeye akasema hata akipata kura, hakuna kuzitangaza zote. Sasa kama Lowasaa aliitwa fisadi miaka dahari na bado akapata kura zaidi ya milioni 6+, huku akiwa domo zege jukwaani, tena kwa tume tusiyo na uhakika nayo, itakuwa huyo Lissu anayeweza kuongea? Ukiona kuna kundi linachezea katiba ili kuzuia kushitakiwa, basi ujue kazi ipo.
 
Niliwahi kuandika kuhusu nia ya Lisu kuutaka Urais wa Tanzania 2020. Huenda
chama chake kikampitisha 2020 badala ya Msigwa. Huyu ni msomi mzuri, ni mwanaharakati na ni mpinzani haswa haswa. Kwa sifa hizo anatosha sana kupeperusha bendera za Chadema Kwa sasa.

TWENDE SAWA

Huyu hakuwahi kushika nafasi kubwa za kiuongozi ila ni mwanasiasa mkubwa sana kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki.. angelikuwa CCM huyu ni dhahiri angeliteuliwa kushika nafasi kubwa kabisa za Kiuongozi.

Ili nimzungumzie kwa haki kabisa Lisu nitatumia SWOT analysis ambayo itatupatia mambo makuu matatu (Strength,Weakness, na threats) hii ni kanuni ambayo haidanganyi na ambayo hutumiwa sana kupata uhalisia wa kitu kabla ya kuamua kufanya jambo. SWOT ya Lisu itaisaidia Jamii ambao ni walengwa wa huduma na nafasi anayoitaka Lisu kwa maana ya kwamba jamii itamfahamu kwa undani kabla ya kumchagua au kutikumchagua, itamsaidia yeye peke yake kujijua na itakisaidia Chama chake mwenyewe.

STRENGTH

1. Ni mzuri katika kujenga hoja, ukikutana naye kwenye hoja hasa zilizo na uelekeo wa fani yake ya Kisheria atakupoteza kabisa. Tuneshuhudia Bungeni mara nyingi akitoa somo la kutosha kuhusu kanuni za bunge na matumizi yake.

2. Akiwa kama wakili ameshinda kesi nyingi sana zake binafsi na zile alizosimamia watu wengine. Lisu ni mojawapo ya mawakili ambao wakisimamia kesi yako unakuwa na uhakika wa kushinda.

3. Ana jiamini sana katika kile anachokiamini, hata kama wengine wote watakataa kumuunga mkono yeye atapambana mwenyewe.

4. Ana ujasiri wa aina yake, Lisu sio mtu mwoga anaweza kupambana na yeyote yule bila kujali status kwenye jamii. Kwa hali ya kawaida ni vigumu kumshambulia Rais wa nchi lakini Lisu alijitoa kufanya hivyo. Ni watu wengi toka mataifa mbalimbali ambao hawawezi hiki kitu.

5. Hutimiza majukumu yake kisiasa sio kiutendaji ipasavyo, kuna wakati watu walimtilia Shaka kuwa Lisu si Mzalendo lakini kwa nature ya kazi yake ndani ya Upinzani alikuwa sahihi kutukosoa. Kilichotakiwa kufanywa kilikuwa ni kuchukua alichokuwa anakisema na kukifanyia kazi.

WEAKNESS

1. Kipingamizi cha kwanza cha lisu hana agenda ya msingi ya Kiuchumi ya kumpeleka Ikulu zaidi ya kuwa mkosoaji mkubwa. Lisu anapaswa sasa kuanza kuonyesha Plan B zake katika maswala ya kitaifa yaani kama jambo limefeli yeye kama yeye angelifanyaje.

Naamini na ndivyo ilivyo kiongozi mzuri ni yule mwenye maono yake juu ya mambo flan yaani mawazo yake binafsi na sio ya kuandikiwa (Ilani) na ndio maana hata Rais wetu kuna saa anaweka ilani Pembeni na kunyoosha kwa namna anavyoamini yeye.
Lisu anatakiwa sasa atuonyeshe nje ya Ukosoaji wake nini plan na Dira yake kwa taifa hili.

2. Tundu Lisu ni mojawapo ya wanasiasa ambao wanapatwa na jazba kwa haraka hasa pale wanapotaka kuzidiwa na hoja.

Amekuwa akitamka maeneo ambayo mara nyingi huleta ukakasi masikioni mwa watu. Mara nyingi na kiutamaduni huwa tunasema Marehemu huwa hashambuliwi lakini Lisu bila kujali aliwahi kumshambulia Mwl Nyerere kipindi cha bunge la Katiba. Kwa heshima ya Mwl Nyerere Lisu hapa alikosea.... na anapaswa kujirekebisha.

3. Udhaifu mwingine wa Lisu ni makundi na urafiki usioeleweka alio nao na mwenyekiti wa chama chake. Kwa ufahamu wa sheria alionao Lisu alishindwa kuonyesha ni wapi kina Mwigamba, Kitila na Zitto walikosea hadi akasimamie kesi zao za kufukuzwa Chadema. Lisu ana Urafiki mkubwa sana na nwenyekiti na mwenyekiti amekuwa akimtumia Lisu kwa maslahi yake binafsi kuliko kukisaidia Chama.

Kama Lisu angelisimama katikati bila kutekwa na kundi la Mwenyekiti huenda angelinusuru kina Zitto kufukuzwa na angelikuwa amekisaidia sana chama kwa kuwabakisha watu muhimu sana kwenye chama. Lisu anaonekana kama anamwogopa sana Mwenyekiti na ushauri anaompa mwenyekiti ni lazma uwe na manufaa kwa Mwenyekiti.

OPPORTUNITY

1.Lisu bado ana fursa inayomzunguka na fursa kuu ni Tukio lililomtokea. Yaani tukio la kupigwa marisasi kwake ni fursa number moja. Kwa lugha ya malkia tunasena CONFLICT has two sides one At the best it Provides an opportunity to learn and a chance for innovation. And second At the worst it destroys individual, block up families and halts production Within organisation. Kwa tafsiri isiyo rasmi Mgongano na Misuguano INA pande mbili unaweza kutumia kujijenga na unaweza kukuharibia kabisa. Kama Lisu atachanga karata zake vizuri tukio like litamjenga zaidi na limeshaanza kumjenga.

2. Fursa ya pili ni kuwa watu wenye age yake kisiasa ndani ya Chama wameanza kupotea kwa Hoja. Watu kama Mnyika walikuwa wanaweza kumletea Upinzani ndani ya Chama ila siku hizi Mnyika ni Togwa.

THREATS

1. Jimboni kwake mambo si mazuri sana, yaani kwa umaarufu alionao haulingani na maendeleo aliyoyapeleka kwenye jimbo lake. Bado jimbo lake ni mojawapo ya majimbo maskini kimiundombinu na hata kipato cha mtu mmoja mmoja. Hii inatokana na yeye kutumika mno Kitaifa na kusahau jimboni kwake. "Kuna msemo unaosema Charity begins at Home" Lisu anatakiwa afanye mambo makubwa ambayo yatafanya kila mtu Jimboni kwake amkubali na hata Singida yote.

2.Kipingamizi kikubwa cha Lisu kwa sasa ni Afya yake. Lisu anatakiwa kwa sasa apiganie zaidi Afya yake kuliko kitu kingine kile.
3. Lisu yupo kama Mwigulu Ndani ya CCM kuwa haamini kuna mawazo Productive njee ya Chama chake. Yaani yeye anaamini kila siku CCM Inakosea hii si sifa ya kiongozi mzuri.

4. Hatari nyingine kwa Lisu ni kitendo chake cha kupenda kuattack Personalities badala ya kujikita kwenye hoja za nchi hii inatakiwa iende wapi. Tuliona alivyokuwa anamkosoa Personally Rais Magufuli badala ya kukosoa Sera na kuonyesha njia. Hata juzi juzi alikuwa anaongelea kitu personally sana kuhusu Kiingereza cha Rais. Mtu anayetaka urais anatakiwa kuwaza mbali sana sio vitu vidogo kama hivyo.

5. Ukaribu unaotaka kujitokeza kati yake na Zitto, who knows Zitto katumwa? Mara nyingine tu hata Upinzani wenyewe wamekuwa wakimtuhumu Zitto kuwa haaminiki. Zitto anaweza kutumia pia yeye Lissu kama ngazi yake ya kisiasa. Kwa sasa ACT wameshalisoma gape na hata Chadema wenyewe wameshaanza Minongono kuwa Zitto hapaswi kuunda ushirika na Lissu. Kwa sasa Brand ya Lisu ni Kubwa kuliko Zitto hivyo hatujui Hesabu za Zitto zipoje. Makachero wa Chadema wanapaswa kufuatilia hili kwa umakini mkubwa.

6.Mwisho kabisa hatari aliyonayo Lisu ni CCM, sio kwamba CCM imelala kutaka kuzima ndoto za Lisu kuendelea kushine kwenye Siasa. CCM bado ina Deal naye kwa umakini mkubwa kuhakikisha Lisu hachanui zaidi ya hapo Bali anazidi kufifia kisiasa.
View attachment 1470417
Shule hizi!!!
 
Back
Top Bottom