Lissu ni Dikteta, anamshawishi Rais Samia kutozingatia Utawala Bora na kuingilia Mihimili mingine

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Lissu ni Dikteta kwa kuwa anamshawishi Rais Samia kutozingatia utawala bora na kuingilia mihimili mingine.

Lissu anataka Samia avunje Ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuingilia Bunge la JMT kwa kuwaondoa wabunge wanaowawakilisha wananchi tena jambo baya zaidi wabunge hao ni wa chama cha upinzani ambao Rais hana mamlaka nao kwani yeye anatoka chama kingine.

Lissu anataka Rais Samia avunje Ibara ya 107A na 107B ya katiba kwa kuingilia uhuru wa mahakama pale alipomtaka Rais kufuta kesi ya Mbowe.

Kwa kufanya hivyo Rais atakuwa ameingilia Mhimili wa Mahakama ambao upo katika mchakato wa kutoa maamuzi kuhusiana na suala la Mbowe.

Inasikitisha mno kwamba Lissu kama kiongozi wa Chama Cha Upinzani anahimiza matendo ya uvunjifu wa katiba wazi wazi tena akiwa mtaalam wa sheria.

Lissu anafanya yote haya akiwa hana mamlaka.

Je akiyapata? Nina imani kabisa kabisa kwamba endapo mtu kama huyu akipewa mamlaka tutashuhudia uvunjifu mkubwa wa katika kuwahi kutokea katika historia ya Taifa letu.

Ni hitimishe kwa kusema kwamba Lissu ametukosea sana watanzania kwa kuweka pembeni taaluma yake ya sheria kwa kuhimiza matendo ya uvunjifu wa katiba wazi wazi.

Watu wa aina hii hawapaswi kuaminiwa kupewa mamlaka ya nchi.
 
Hakika wachaw wa cku hiz ni vjana wadogo tu
 
Mtatapika sana Duniani watu kama nyinyi waliachwa huko
Enzi za ujima...mawazo ya kimaskini ..EU Mhimili wa Dunia
 
Andiko la hovyo sana.

Kwani nani asiyejua wabunge feki wale waliingizwa kwa mchongo wa serikali?

Nani asiyejua kesi ya Mbowe ni mchongo. wa watu wa idara za serikali?

Kama ni michongo ya serikali na watu wake nani yupo kwenye nafasi ya kusahihisha kama sio yenyewe?

Mwiba hutolewa pale ulipoingilia.
 
Mtoa mada, ametafakari kwa kuangalia maslahi ya Tumbo badala ya maslahi ya Taifa .Ninani mwenye akili timamu atasema Wale wabunge wapo pale wapo kihalari? Ni yule mwenye akili ndogo mfano wa sisimizi tu!!
 
Lissu ni Dikteta kwa kuwa anamshawishi Rais Samia kutozingatia utawala bora na kuingilia mihimili mingine...
Basi andamaneni pamoja na wanalumumba wenzio, kupinga Hilo, roho mbaya zitawavuruga akili😃
 
Ukapimwe haja kubwa na kinyeo
 
Hii mada ni moto hakuna bavicha mwenye akili timamu atatia mguu wake.


rudi nenda kajielimishe tena. una uelewa mdogo kiasi cha kutojua kama DPP ana uwezo wa kufuta kesi mahakamani. Huna akili za kujua tume ya uchaguzi inaweza kuiandikia bunge juu ya sintofahamu ya Covid 19 kwa sababu yenyewe ndio inaowateua.

Natamani Mods watufichie hii aibu sababu JF wote tunaonekana hamnazo kumbe ni jinga moja tu
 
Lisu hakuzungumza na DPP kazungumza na Rais.
 
Hawa watu ni hatari, kwa kweli Mimi nimetafakari na kugundua Lissu ni dikteta, tena hatari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…