Uchaguzi 2020 Lissu: Nikichaguliwa, ndani ya siku 100 za kwanza masheikh wa Uamsho wataachiwa huru

aisee kiukweli binadamu tunatofautiana uwezo wa kuelewa. Hivi mtu unaelewa nini mtu akisema ndani ya siku mia? Akiapishwa leo kesho akawaachia au wakapewa dhamana haitakuwa ndani ya siku mia? Halafu kwa akili yako unadhani Lissu ataeleza mchakato woooote akiwa kasimama jukwaani? zile zinakuwa dondooo tu
 
"Nikishinda... na kule Bara nna uhakika atashinda Lissu... atanrudishia watu wangu" Maalim Seif. Hao Masheikh hakuna mtu ndani ya sisiemu anawazungumzia!
Wana kesi mahakamani, Sasa CCM inahusika hapo? Kama chadema wanahusika wakawatoe miaka yote huyo Lissu mwanasheria kakaa kimya Sasa anatafuta kura anajitoa ufahamu eti Hadi awe rais, kwani rais Magufuli ndo kawaweka mahabusu?
Yeye lissu ni mwanasheria aende akafungue kesi awatoe.
 
Lissu anadhani anagombea uenyekiti wa kamati ya sendoff; kuomba kura jambo moja, unaweza kuhadaa watu kwa kila ahadi, ila ukishatangazwa na kuapishwa kuwa rais utakutana na utaratibu wa namna ya kuongoza nchi, na sio kila jambo utalipayuka jukwaani. Kuna mambo utayakuta na kuyaacha hivyohivyo.
 
Kura yako ni sawa na kuweka sukari ziwa victoria ukitegemea utakunywa chai Lissu hawezi kushinda hata viti maalum[emoji3][emoji28][emoji1787][emoji1787]
 
Hapa kateleza.

Ni matumaini yangu kwamba atajirekebisha makosa kama haya.

Hao Mashekh ni waTanzania.

Ni ndugu wa waTanzania wote na sio wa waislam pekee. Ni wajibu wa waTanzania wote kupaaza sauti kila mTanzania wa aina yoyote anapoonewa.

Akianza kuweka watu katika makundi, hata yeye hatakuwa tofauti na huyo anayetafuta kumng'oa kwenye kiti.

Uonevu kwa mTanzania yeyote ni lazima ukataliwe na umma wa waTanzania bila kujali dini, kabila au jinsia zao.
 
Anayewashikilia hao Mashehe ni Serikali/executive na siyo Mahakama.
Serikali kupitia DPP inaweza kuifuta kesi hiyo muda wowote.
 
Anayewashikilia hao Mashehe ni Serikali/executive na siyo Mahakama.
Serikali kupitia DPP inaweza kuifuta kesi hiyo muda wowote.
Ni kweli lakini wote tunajuwa DPP ni nani na anafanya kazi za nani, akipewa kimemo anafanya tu sio DPP wa wenzetu huko hata Rais anaweza kushitakiwa huku wote ni walewale tu.
 
Mgombea wetu anatetea magaidi? Maana wanatuhumiwa kufanya ugaidi Zanznibar, mwaka huu chama chetu kimechemka sana.
Nadhani huyo ni mgombea wenu kifamilia unafurahia utawala usiojali sheria tafakari kama ndio Baba,baba mdogo wako yuko huko jela bila kesi yoyote huo unaoita ugaidi nenda kaprove mahakamani.
 
Nadhani huyo ni mgombea wenu kifamilia unafurahia utawala usiojali sheria tafakari kama ndio Baba,baba mdogo wako yuko huko jela bila kesi yoyote huo unaoita ugaidi nenda kaprove mahakamani.
Kwani suala lipo wapi? Halipo mahakamani.
 
Mkashitaki kwenye Jumiya Za Kinataifaa tuwekewe Vijwazo... Maana Tukiwaambia Hakuna Cha Jumuiya za Kimataifaa Wala Nini KUNA JAMUHULI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SHERIA ZAKE...
 
Kwanini siku mia moja? Si utamke tu mara baada ya kuapishwa? Au unajua kuna 'formalities' za kufuatwa na hapa unawafurahisha wasiojua?
 
Hapana.

Lissu katumia mfano wa kesi kubwa.

Hao Watanzania wa dini fulani, ni Watanzania pia. Dinibyao haiwaondolei uTanzania wao.

Tena kasema na wengine, wala hajaishia kwa hao.

Ukiona dini hapo, wewe ndiye mdini.

Serikali ya CCM imejamba. Imewafunga watu miaka mingi bila kuwashitaki.

Lissu katema mate, kasema huu ushuzi unanuka tusiukubali.

Sasa wewe badala ya kumlaumu aliyejamba, unamlaumu aliyetema mate na kusema huu ushuzi unanuka tusiukubali?
 
🤣😂🤣😂 Ukitakaa kuamini Wafuasi Wa CHEDEMA WENGI NI WAHUNI ni Leo Sugu kapita Sokoni Anaiimbiwa Rais, Rais, Rais🤣😂🤣 Nimecheka sana Sijui CHADEMA URAIS WANAUCHUKULIAJE ... Hiki chama Kinahitajii Neema ya Mungu kuwepo mpka 2025 maana Kinaongozwa Na Wahuni wapiga deal. Ila Safarii hii kimekutana Na CHUMA mwisho wake umefikaaa

HATUWEZI KUKABIDHI NCHI KWA WAHUN💪🏽
 
"Nikishinda... na kule Bara nna uhakika atashinda Lissu... atanrudishia watu wangu" Maalim Seif. Hao Masheikh hakuna mtu ndani ya sisiemu anawazungumzia!
Masheikh waliwaunganisha wazanzibar kupitia dini..hapakua na ccm wala cuf..walikuwa wanasepa na kijiji..mwishowe watu wangebinuliwa na masheikh kushika hatamu..ndomana wale hawasemi chochote..ni mwiba kooni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…