Uchaguzi 2020 Lissu tumia nafasi hii, Ikulu mapema sana

Uchaguzi 2020 Lissu tumia nafasi hii, Ikulu mapema sana

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Amani kwako.

IIfahamike kuwa kwa sasa mgombea wa CCM ndg John anatumia nguvu kubwa kwenye kampeni zake huku akijua alio nao ndani asilimia kubwa hawana urafiki naye.

Kuna wana CCM wengi walishaamua liwalo na liwe na ndiyo ambao leo Katibu Mkuu wa CCM anaita media kuwachimba mkwara, mpaka hapo kuna kitu unaelewa.

Kuna kina mzee, Kinana, Januari, Nape nk wamekaa mkao wa kula, najua kushirikiana nao waziwazi haiwezekani hasirani ila kama ikitumika secret work inawezekana sana.

Kuna mifumo ambayo mpaka sasa inaandaliwa, ni jinsi ya kutunza, kulinda, kufuatilia na kusimama kidete dhidi ya kura zote zitakazopigwa siku hiyo, hapo kuna ile ngome nimeitaja pale juu kwa kushirikiana na IT Expert in/out basi mchezo wa 2015 utakuwa umepata mbereko.

Ndg. Lissu, usidharau hii kitu hao wanaCCM wanaochimbwa mkwara kwako ni turufu kubwa sana, wape nafasi ili kuondoa kile wengi wanasema udhalimu huu.

Povu kwa wanaCCM ruksa, ila ujue nina kadi ya CCM toka 1989.
 
2015 kulikuwa na wanaCCM kibao mlikuwa nao huko wakaona hamna muelekeo.
 
Wakati Lowasa anagombea Chadema mlisema maneno kama haya lakini mwisho wa siku mlikimbia thread zenu.
 
Moja ya mambo yanayosababisha Jpm kuendelea kuwasumbua CCM wasiomtaka ni ku underestimate timu yake ya mipango na figisu za siasa.
 
Halafu ukitoka hapo unasema umetoa ushauri wa kitaalamu cdm majanga ndiyo maana mzee wa anga kawatosa mhangaike wenyewe yakiwashinda aje achukue SACCoS yake.Mlidhani kuendesha chama mchezo chini ya huyo mlopokaji wenu
 
Wakati Lowasa anagombea Chadema mlisema maneno kama haya lakini mwisho wa siku mlikimbia thread zenu.

Usinganishe uwezo wa Lowassa na Lissu wewe!
Isitoshe lowasa alibebwa na vyama zaidi ya viwili.
Ona lissu, chama kimoja tu nchi imesimama.
Ccm ndembendembeeee! Urojoooo
 
Hiyo ni kauli yako, hakuna para nimetaja hicho kitu.
Halafu ukitoka hapo unasema umetoa ushauri wa kitaalamu cdm majanga ndiyo maana mzee wa anga kawatosa mhangaike wenyewe yakiwashinda aje achukue SACCoS yake.Mlidhani kuendesha chama mchezo chini ya huyo mlopokaji wenu
 
Serikali dhalimu na Dikteta huwa wanafanya nchi na wao kama serikali na kiongozi kuwa kitu kimoja Eti ukimkosoa dikteta umekosoa nchi Ukipinga sera za serikali, we msaliti wa nchi Kiuhalisia unaweza kupinga serikali, kiongozi na kwa kufanya hivyo ukawa mzalendo
 
Usinganishe uwezo wa lowasa na lissu wewe!
Isitoshe lowasa alibebwa na vyama zaidi ya viwili.
Ona lissu, chama kimoja tu nchi imesimama.
Ccm ndembendembeeee! Urojoooo
Akuna jipya,ni yaleyale tu.Lissu atashinda kama tume ni ya wakwe zake Mbowe mwenye chama.
 
CCM bwanaa! ... waliposikia ndege mjanja hunaswa na tundu bovu Sasa wanaandaa tundu bovu ili ...!!?
BARARUKA LISSU!
😅
👊 ✌✌✌💥
 
Back
Top Bottom