Uchaguzi 2020 Lissu: Tutatengeneza nchi ya watu walio huru

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA: Tundu Lissu amesema watatengeneza nchi huru na yenye haki. Nchi ambayo hakuna kiongozi atakayeogopwa kuliko Mungu.

Amesema kia mtu anahitaji haki na kila mtu anastahili kupata haki, awe askari mfanyabiashara, mkulima, mfugaji, mama lishe, bodaboda au kazi yoyote ile.

Ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa Kampeni Bukombe mkoani Geita, ambako pia amewasisitiza wananchi wote kwenda kupiga kura Oktoba 28, 2020.

Your browser is not able to display this video.
 
Kwani kaambiwa watz wako utumwani?
 
Mmmh, kuna watu wengi Tanzania, pamoja na mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa, polisi, wakuu wa wilaya, wasimamizi wa uchaguzi, wakurugenzi nk, wanamuogopa kiongozi fulani zaidi sana ya wanavyomuogopa Mungu!

Dhambi watafanya bila hofu ya kumkosea Mungu, lakini wakifikiria kumkasirisha jamaa magoti yanagongana kwa woga!
 
Ivi wewe hujioni
Kwani kaambiwa watz wako utumwani?
Kwamba upo utumwani?
Mkulima aliyepokwa KOROSHO zake kifedhuli hayupo utumwani?
Mwalimu ambaye hawajaongezewa mishahara kwa miaka 5 hawapo utumwani?

Wakinamama wanaotozwa pesa akienda kujifungia hayupo utumwani?
Mfanyakazi aliyeongezewa makato ya mkopo wa elimu ya juu toka 8 hadi 15% huku akiwa anaendelea kulipa mkopo na tena wenye riba hayupo utumwani?
HUJUI MAANA YA UTUMWA WEWE PIMBI LA LUMUMBA KAA KIMYA
 

Wakulima wa korosho waliokuwa wabadhulumiwa miaka nenda rudi kupitia kangomba na utapeli mwingine mwingi ndio mnawaona wajinga na hawsba akili ya kurlewa kuwa JPM anadhamira nhena kwao.

Nyie ndio maadui wa ndani ya nchi mliozuiliwa kuibia wakulima kwa utaratibu wa kilanguzi mmebakia kupika majungu yasiyo na kichwa wala miguu. JPM ashukuriwe kwa kufungua akili za Watanzania zilizokuwa zimewekwa kwenye vibuyu.

Vipi Mburahati leo? Pamoja na mvua kubwa lakini watu wakamua acha waloe lakini wasimame imara bega kwa bega na mkombozi wa wanyonge JPM.
 
Kangomba sio ulanguzi wewe ni utaratibu wa kawaida kwenye biashara yeyote kasome vizuri commerce ya form 3.

Watu wanaporwa KOROSHO zao unaleta habar za mburahati hapa?

Watu hawajaongezewa mishahara for 5 years bila sababu za msingi toka kwa huyo kuhani unabwabwaja nn?

Watu wamebomolewa nyumba zao huko Kimara kwa ubabe wa kishamba kabisa unaleta matapishi hapa?

Wamachinga wanakatishwa vitambulisho havina hata majina?

Watu wameuliwa na kutupwa baharini huko RUFIJI .wewe unaongea utumbo hapa.
 

Sasa kama anataka uhuru mbona ana walaani wanao mpopoa na mawe?
 
Acha ujinga JPM si laghai na tapeli wa kuongezea mshahara wafanyakazi wa shs 10,000/-. Yeye kadhibiti mfumuko wa bei kwa umahiri mkubwa. Hakutaka kuwa tapeli wa kudaganya watu wazima na familia zao kwa kuwaongezea tu elfu kadhaa kwenye mshahara. Wakati ulichowaongezea hakiendani na kupanda kwa gharama za maisha

Hata uchumi wachekechea acha form 3 haulekezi kununua maua ya mkorosho shambani kwa kilo shs 100/- Huu ulikuwa uuaji, wewe fikiria uzito wa maua na bei 100/-. Kwa kilo 1. Shetani na mawakala wake tu ndio wenye uthubutu na roho ya dhulama kubwa ya aina hii.


 
Nilipataa wasaa wa kuwa na mazungumzo na mjeda fulani hiviii mwaka huu, akasema hakuna mtu duniani ambaye anaweza kuishi bila kupingwa.

Akatolea mfano kuwa hata Bwana Yesu Kristu alipingwa sembuse huyo magufuli mpiga madeal tu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ayeeeee 😂 😂 kmmk
 
Mtu anapokuja na hoja za Uhuru karne hii nakua simuelewi kabisa naona kama vile anaishi zama za mawe huko.

Yaani jamaa kachekecha sera kaamua kuja ni hiki kituko.
 
Upuuzi mtupu, ameshidwa kutengeneza Ufipa ndio itakuwa nchi?. Mbowe, Slaa, Lowasa walishindwa hata na wewe itakuwa vilevile Oct 28. Ninyi Chadema mnadhani kuongoza nchi ni sawa na kukusanya michango kwenye mikutano yenu ee, wananchi hatuwezi kubali uzandiki wenu pelekeni huko Ubelgiji kwa beberu zenu. Tunahitaji maendeleo, Magufuli ndio baba wa maendeleo kwa watanzania wote bila kubagua. Poleni saccos ya Mbowe.
 
Kama anataka nchi ya kutengeneza a aende huko kwenye sayari zingine nae awe mungu wao.
Sisi tulishatengenezwa tayari na mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…