Kwahiyo hapo wewe ndo unaona elimu yako iko vizuri na kwahiyo unaelewa sana?!
Hoja ya Lissu ilikuwa kwamba, tukifanya mambo kwa mihemuko Acacia watatupeleka mahakamani kwa sababu hawa watu wanalindwa na mikataba ya Kimataifa! Akazungumza wazi kwamba, ikama kweli serikali ina nia ya dhati ya kupambaba na dhuluma ya hawa watu, basi serikali ijiondoe kwanza kwenye hii mikataba! Ukisjajiondoa, Acacia anakuwa hana pa kukimbilia except kwenye mahakama zetu za ndani! Hawawezi tena kwenda kwenye mahakama za Kimataifa kwa sababu kujiondoa kwetu ni kusema hatuzitambuia hizo mahakama!
Mleta mada na watu aina yako mnaotamba kuwa ni waelewa wakati hamuelewi; anamkejeli Lissu kwamba mbona hao Acacia wenyewe hawajatushitaki!
Ndipo nami nikaja na hoja kwamba kwa sasa Acacia hawana sababu ya kutushitaki! Hawana sababu hiyo kwa sababu mtake msitake; hadi sasa Acacia ndie mshindi! Serikali imesema Acacia tunawadai zaidi ya Trillion 400 lakini hadi sasa hawajalipa hata sent 5 na tunaenda mwaka wa 3 sasa! Katika kupoteza muda, Barrick wakaahidi "Kishika Uchumba" cha US$ 300 Million! Nadhani inaenda miaka 2 sasa lakini hizo nazo hawajalipa hata sent 5! Sasa waende mahakamani wakafanye nini wakati wenyewe wanatuchezea danadana kama mazuzu?! Na kama umeshindwa kuunganisha dots kwanini nimeleta hoja ya malipo halafu bado unajigamba kuwa muelewa; basi una safari ndefu!!
Assumption ya Lissu ni kama alitarajia serikali ingewabana Acacia kisawasawa kiasi kwamba wasingekuwa na pa kupumulia kama ambavyo iliwahi kutokea kwenye makampumi ya mafuta huko Amerika ya Kusini! Hata hivyo, Acacia hajabanwa mbavu kihivyo kwa sababu pamoja na kuzuia makinikia lakini wanaendelea na shughuli zao kama kawaida! Na ndio maana ingawaje miaka 3 imeshafika; lakini bado wanaendelea kudunda tu!! Na kiburi chote hiki cha Acacia ni kwa sababu wanafahamu wanalindwa na mikataba ya kimataifa! Na ni kutokana na huo ukweli ndio maana hata serikali wenyewe wanashindwa kuchukua hatua kali dhidi ya Acacia! Lakini lau kama serikali ingesikiliza ushauri wa TL wa kuanza kwanza kujitoa kwenye hizi mahakama kabla ya kuwang'ang'ania Acacia; hivi sasa Acacia wasingekuwa na hiki kiburi kwa sababu wangefahamu hawana pa kukimbilia!